ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,436
- 4,756
Katika historia ya dunia huwa daima kunakuwa migungano kati ya watawala na watawaliwa.Kwa kawaida watawala huwa wanakuwa tayari na JESHI lenye zana kali ila watawaliwa wengi huwa hawana uwezo wa kuwa na silaha wala kuzitumia.Inapofikia hatua kwamba watawaliwa wanataka kuchukua hatua dhidi ya watawala wao huwa wanakuwa na sila kubwa tatu:
Haki inapokosekana ndo matokeo huwa kama hayo.Kaulu za dharau,kiburi zinapotamkwa ndo huleta hali hii.Uonevu wa wazi unapotamalaki ndo hupelekea hali hii.Tunaona Jinsi serikali ya CCM inavokaza kulazimisha kama taifa tufkie hatua hii.Tuanona kauli zao unyonyaji wao na upokaji wao wa haki unavosababuisha maumivu na chuki.
Je Tanzania itavuka SALAMA?au ni sehemu ya mpango wa serikali kuhakikisha kwamba tunaingia katika vita?
Tujadili
- Silaha ya kwanza ni wingi wao.Kadiri wanavyokuwa wengi wanaoamini katika mabadiliko basi nguvu yao huwa kubwa.Ili kuhakikisha hawawi wengi serikali uhakikisha inawagawa kwa misingi mbalimbali ikiwamo,dini,itikadi,ukabili,hali za kiuchumi n.k.Lengo kubwa la kufanya hivi ni kuhkiksha kunakuwa na migogoro ya kimaslahi baina ya watawaliwa ili kuruhusu serikali iendelee kuwanyonya bila kuwajibika
- Silaha ya pili ni huruma ya wenye Nguvu na uwezo.Hii utokea aghalabu pale ambapo wachache wenye uwezo wa kuwaunganisha na kuwatetea wengi wanapoamua kujitoa muhanga ili kuwatetea hawa wanyonge.Wachache hawa huwa na uwezo wa kupata na kutumia silaha,huwa na uwezo wa kuzungumza na kuelewa mambo nje ya mgawanyo wa kitabaki na hujali maslahi ya wengi.Hapa watawala hutumia mabandiko kama ya magaidi,mawakala wa mabeberu,wahaini na majina mengine ya kutisha ili kuhakikisha kwamba wachache hawa wanavunjika moyo na kukosa uungwaji mkono wa wengi
- Silaha ya tatu inaitwa MOLOTOV COCK TAIL.hii hutumika wakati nyingine zote zimeshindwa na wananchi wamekata tamaa na kuamua lolote liwe.Silaha hizi hutumika pamoja na mawe,marungu,mapanga,vilipuzi vya kienyeji,sila za kienyeji,n.k.Kwa kawaida silaha hizi husababisha uharibufu wa mali,vifo na ulemavu wa wtu wengi.Adui huwa ni yeyote ambaye haungi mkono watu wengi katika harakati zao.Hivyo huanza kwa majirani kuuana kwa sababu ya tofauti za kiitikadi,kitabaka kidini,kikabili etc na baadae hukuwa na kufikia mashambulizi dhidi ya miundo mbinu ya serikali na ya umma,mashambulizi dhidi ya vyomba vya usalimu na kufikia hatua ya kuitwa mauaji ya halaiki
Haki inapokosekana ndo matokeo huwa kama hayo.Kaulu za dharau,kiburi zinapotamkwa ndo huleta hali hii.Uonevu wa wazi unapotamalaki ndo hupelekea hali hii.Tunaona Jinsi serikali ya CCM inavokaza kulazimisha kama taifa tufkie hatua hii.Tuanona kauli zao unyonyaji wao na upokaji wao wa haki unavosababuisha maumivu na chuki.
Je Tanzania itavuka SALAMA?au ni sehemu ya mpango wa serikali kuhakikisha kwamba tunaingia katika vita?
Tujadili