Dkt. Gwajima D
Minister
- Nov 28, 2015
- 966
- 6,019
Wasaalam.
MTAKUWWA kirefu chake ni Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (wa kike na kiume).
Awamu ya kwanza ulikuwa 2017/18-2021/22.
Awamu ya 2 ni 2024/25-2028/29 ambapo, tulizindua tarehe 15 Mei, 2029.
Kwa kifupi, ziko Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto kuanzia ngazi ya Kijiji, Mtaa, Kata, Halmashauri, Mkoa hadi Taifa. Kwenye ngazi ya Kijiji, Mtaa na Kata, wajumbe ni pamoja na wananchi yaani jamii.
Aidha, kamati imesheheni wadau wa sekta zote ikiwa ni pamoja na sekta binafsi, NGOs, viongozi wa kidini, watu maarufu wanaoheshimika na wenye msaada kwenye jamii, wawakilishi wa makundi ya kijamii wakiwemo vijana, wenye ulemavu, watoto, wanawake (kifupi makundi yote yamewakilishwa) (mpango utapandishwa online tutatangaza).
Katika kuongeza Kasi ya utekelezaji na elimu kwa jamii ili jamii imiliki programu hii na kushirikiana na Serikali, kesho tutakuwa na ziara ya baadhi ya mawaziri wa kisekta katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam ambapo, tutafuatilia hali ya utekelezaji, kupokea changamoto na kubadilishana maoni na wananchi Ili kuendelea kujenga kwa uimara zaidi kamati hizi.
BAADHI ya malengo mahsusi ya ZIARA YA 27 JULAI, 2024.
1. Kujionea mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Kamati za MTAKUWWA pamoja na kupokea maoni na kutoa mwelekeo.
3. Kuinua sauti kuhusu nafasi ya jamii kwenye utekelezaji wa MTAKUWWA kwani Wananchi wawakilishi wa jamii ni Wajumbe wa Kamati hii.
MATARAJIO YA ZIARA;
1. Mafanikio yanatambuliwa na changamoto zinatambuliwa na mwelekeo mpya unatolewa.
2. Wananchi wengi zaidi wanapata elimu kuhusu nafasi yao kwenye utekelezaji wa MTAKUWWA kama wajumbe wa Kamati.
3. Wananchi wanaongeza Kasi ya ushiriki wao na mchango wao kwenye utekelezaji wa Kamati.
4. Ulinzi wa Wananawake na Watoto unaimarika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kijiji na Kata kwa wananchi kushirikiana na Serikali kwa kasi zaidi
5. Nchi nzima inaongeza Kasi zaidi ya utekelezaji wa MTAKUWWA hivyo, Kasi ya udhibiti wa ukatili wa kijinsia na kwa watoto inaongezeka.
ZIARA itaendelea nchi nzima.🇹🇿
Kwa pamoja, Serikali na Wananchi, tunatekeleza na mwisho tutakuwa na upimaji endelevu wa ufanisi na utambuzi kulingana na ufanisi Ili kuchochea zaidi hamasa na ushirikiano kwenye utekelezaji wa mpango huu.
Elimu itaendelea kutolewa. Unapopata elimu, tafadhali mpe mwingine, ndiyo ushirikiano wenyewe huo, tunaita LeMaChU yaani Lete Mabadiliko Chanya Ulipo 🤝 🇹🇿 🙏🏽
Endelea kufuatilia taarifa zaidi.....