Ijue MTAKUWWA Awamu ya 2

Ijue MTAKUWWA Awamu ya 2

Ni jambo jema sana kuwa na mikakati kama hii. Na kwa sasa kuna wimbi la ukatili kati ya watoto wenyewe. Yaani watoto wanalawitiana sijui hata tunaelekea wapi? Elimu itolewe zaidi kwa jamii ya tabaka la chini.

Wazazi, walezi wengi wako busy sana kutafuta maisha badala ya kutoa malezi kwa kizazi chao. Wengi wao wanatoa matunzo na sio malezi
Mkuu hili zuri lakin empowerment hasa kiuchumi ndo msingi. Mana kumekuwa na maisha duni sana hukj uswahilin.. haiwezkan baba n mama na mtoto wa miaka juu ya 7 wallet chumba kimoja. Vyakula vya wakubwa watoto wanaona.

Wanaenda kujaribiana wao kwa wao.. chanzo ni kuona yanayoendelea kwa kulala chumba kimoja na wazazi! Yote ni umaskin tu. Kumbe ilitakiwa mtoto yule alale chumban kwake asione sehem. Nadhani sheria ziwambe kweli kweli pia kwenye matumizi ya simu janja kwa watoto ase
 
Namba 4 na 5 naona ni matarajio ya ziara hii, japo napata wasiwasi wa effectiveness na efficiency ya ziara hii kwenye kuacha impact katika mkakat mzima wa community engagement. Hasahas kuzingatia utekelezaji wake kwenye kuacha...
Ahsante Sana kwa maoni yako. Mpango huu kama ilivyo mingine, unatekelezwa kupitia ugatuaji madaraka kwenda karibu na wananchi.

Yaani mamlaka za serikali za mitaa zinamiliki ajenda, wanajadili vipaumbele na hizi ajenda zinakuwa sehemu, wanaweka mipango na mikakati, wanaingiza kwenye Baraza la Maendeleo Kata, wanaingiza kwenye kamati za baraza la madiwani kisha Baraza, baraza la maendeleo wilaya na mkoa (DCC na RCC) na hapo ndiyo ajenda inakuwa imekamatwa na mfumo mzima wa utekelezaji DxD. Tunaendelea kuelimisha na kujenga uwezo wa kisekta ngazi zote.

Ahsante Sana kwa maoni yako.
 
Tuchukue kesi ya ushoga, anazuia vipi kwa mfano?

Atafungia mitandao yote watu wasione maudhui ya huko nje, mashoga watahukumiwa jela au atafanyaje?
Ushoga kwq moral standards za muafrika ni deviations. Mashoga ni deviants lakin pia, hilj suala ni mtambuka mana linachagizwa na usasa na kuna biological explanation ya hii kitu. Mm naona kuna haja ya kuongeza privacy tu mana kinachopingwa kwa mashoga ni kile kitendo cha me kwa me, right?

Kile kitendo chenyew kiafrika pia ni private issue, ndo mana watu huwa hawatangazi. So, hizi kwa kuzuia ni kupunguza ukali wa tafsiri za baadhi ya mambo. Leo hii mtamzania akiona rangi nyingi nyingi kwenye nembo moja unamchabganya kwelikweli.. hii ni misinterpretation
 
Ni jambo jema sana kuwa na mikakati kama hii. Na kwa sasa kuna wimbi la ukatili kati ya watoto wenyewe. Yaani watoto wanalawitiana sijui hata tunaelekea wapi? Elimu itolewe zaidi kwa jamii ya tabaka la chini.

Wazazi, walezi wengi wako busy sana kutafuta maisha badala ya kutoa malezi kwa kizazi chao. Wengi wao wanatoa matunzo na sio malezi
Hakika, inabidi kupeleka elimu huko huko kwenye jamii. Na kwa kuwa mpango huu una maeneo 8 ya kimkakati na unahusisha sekta karibu zote, eneo la Uwezeshaji kiuchumi pia lipo, sambamba na eneo la malezi na makuzi kwa watoto chini ya umri wa miaka 8 na pia vijana balehe. Vyote hivi vikimilikiwa na jamii, ufanisi unaongezeka. Ahsante Sana kwa maoni yako na ushirikiano
 
Wasaalam.

MTAKUWWA kirefu chake ni Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (wa kike na kiume).

Awamu ya kwanza ulikuwa 2017/18-2021/22.
Awamu ya 2 ni 2024/25-2028/29 ambapo, tulizindua tarehe 15 Mei, 2029.

Kwa kifupi, ziko Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto kuanzia ngazi ya Kijiji, Mtaa, Kata, Halmashauri, Mkoa hadi Taifa. Kwenye ngazi ya Kijiji, Mtaa na Kata, wajumbe ni pamoja na wananchi yaani jamii.

Aidha, kamati imesheheni wadau wa sekta zote ikiwa ni pamoja na sekta binafsi, NGOs, viongozi wa kidini, watu maarufu wanaoheshimika na wenye msaada kwenye jamii, wawakilishi wa makundi ya kijamii wakiwemo vijana, wenye ulemavu, watoto, wanawake (kifupi makundi yote yamewakilishwa) (mpango utapandishwa online tutatangaza).

Katika kuongeza Kasi ya utekelezaji na elimu kwa jamii ili jamii imiliki programu hii na kushirikiana na Serikali, kesho tutakuwa na ziara ya baadhi ya mawaziri wa kisekta katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam ambapo, tutafuatilia hali ya utekelezaji, kupokea changamoto na kubadilishana maoni na wananchi Ili kuendelea kujenga kwa uimara zaidi kamati hizi.

BAADHI ya malengo mahsusi ya ZIARA YA 27 JULAI, 2024.

1. Kujionea mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Kamati za MTAKUWWA pamoja na kupokea maoni na kutoa mwelekeo.
3. Kuinua sauti kuhusu nafasi ya jamii kwenye utekelezaji wa MTAKUWWA kwani Wananchi wawakilishi wa jamii ni Wajumbe wa Kamati hii.

MATARAJIO YA ZIARA;

1. Mafanikio yanatambuliwa na changamoto zinatambuliwa na mwelekeo mpya unatolewa.
2. Wananchi wengi zaidi wanapata elimu kuhusu nafasi yao kwenye utekelezaji wa MTAKUWWA kama wajumbe wa Kamati.
3. Wananchi wanaongeza Kasi ya ushiriki wao na mchango wao kwenye utekelezaji wa Kamati.
4. Ulinzi wa Wananawake na Watoto unaimarika kuanzia ngazi ya Mtaa, Kijiji na Kata kwa wananchi kushirikiana na Serikali kwa kasi zaidi
5. Nchi nzima inaongeza Kasi zaidi ya utekelezaji wa MTAKUWWA hivyo, Kasi ya udhibiti wa ukatili wa kijinsia na kwa watoto inaongezeka.

ZIARA itaendelea nchi nzima.🇹🇿

Kwa pamoja, Serikali na Wananchi, tunatekeleza na mwisho tutakuwa na upimaji endelevu wa ufanisi na utambuzi kulingana na ufanisi Ili kuchochea zaidi hamasa na ushirikiano kwenye utekelezaji wa mpango huu.

Elimu itaendelea kutolewa. Unapopata elimu, tafadhali mpe mwingine, ndiyo ushirikiano wenyewe huo, tunaita LeMaChU yaani Lete Mabadiliko Chanya Ulipo 🤝 🇹🇿 🙏🏽

Endelea kufuatilia taarifa zaidi.....
Muheshimiwa ni lini mtaanzisha kampeni ya kulinda ukatili dhidi ya wanaume!!?

Wanaume tunapitia stress nyingi kwenye maisha na Sheria hazipo upande wetu coz Sheria zinalinda watoto na mama zao sisi tunalindwa na Sheria zipi!!?

Au mnamuachia Mungu pekee !!?sisi hatuna haja ya kulindwa dhidi ya ukatili wa wanawake!!?

Hivi unajua kununiwa na kunyimwa unyumba Kwa sababu zozote zile ni ukatili wa kijinsia!!?

Hivi unajua sisi wanaume kufanywa kuwa ATM machine za Hela na Hawa mabinti ni ukatili kwetu!!?

Hivi unajua tukiwatongoza wanawake wanaumwa na njaa wakti huo huo,Kodi ya pango huisha wakati huo huo,pia mama yake mzazi huumwa wakati huo huo na bill husoma hasta laki tatu !!!?hata kabla ya tendo lenyewe !!!?Huo sio ukatili Muheshimiwa waziri!!!?

Tunaomba kampeni ya ukatili wa wanaume ianze rasmi na Sheria za kutulinda zianze rasmi!!
 
Tarajio
Mpango mzima umekaa ki- nadhalia zaidi kuliko uhalisia..Kwa mfano Usalama wa watoto sasa ni tete na matukio ya utekaji yanaendelea.4 na 5 Waziri anasema usalama umaimarika..Polisi wana kanusha.Rais anasema ni maigizo tu.Ziara hiyooo...wanaenda kutathimini mafanikio ..yapi.? Mbona ni kama namna tu ya upigaji?Na anakazia ziara zitafanyika nchi nzima na utekwaji nao umetamalaki kila mahali? Sasa ni nini..
Hayo ni mategemeo! Expecting results.. sio achievement ya mradi uliotoka (phase 1)
 
Pele limepata mkunaji 🤣
 
Muheshimiwa ni lini mtaanzisha kampeni ya kulinda ukatili dhidi ya wanaume!!?

Wanaume tunapitia stress nyingi kwenye maisha na Sheria hazipo upande wetu coz Sheria zinalinda watoto na mama zao sisi tunalindwa na Sheria zip...
Ahsante Sana kwa maoni, hizi kamati zitakuwa kitovu cha kujadili ajenda zote zilizo changamoto kwenye jamii. Aidha, sera mpya ya maendeleo ya Jinsia na Wanawake tuliyozindua Machi 2024, ukurasa wa , 22 imeeleza kuhusu ushiriki wa wanaume hivyo, ni wakati wa kusogeza sera na miongozo ya kisera kwenye jamii Ili wawakilishi wa wananchi wabebe ajenda za jamii zote zikiwemo hizi za mmomonyoko wa maadili na ukatili wa kijinsia na kwa watoto.

Tunashukuru Sana kwamba, awali kabla ya wizara hii kuundwa, mijadala kuhusu ajenda hizi ilikuwa michache hata maswali pia. Sasa tunataka mijadala na maswali yaamke kuanzia kwenye Majukwaa ya serikali za mitaa na mabaraza ya madiwani badala ya kusubiri bungeni tu na huo ndiyo utakuwa utekelezaji wa DXD imara zaidi.
 
Tarajio

Hayo ni mategemeo! Expecting results.. sio achievement ya mradi uliotoka (phase 1)
Taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa Awamu ya kwanza ipo, ndiyo imeunda mpango wa Awamu ya pili. Tusichanganye matarajio ya ziara ya kesho na mafanikio ya utekelezaji wa MTAKUWWA Awamu ya kwanza tafadhali
 
Ushoga kwq moral standards za muafrika ni deviations. Mashoga ni deviants lakin pia, hilj suala ni mtambuka mana linachagizwa na usasa na kuna biological explanation ya hii kitu. Mm naona kuna haja ya kuongeza privacy tu mana kinachopingwa kwa mashoga ni kile kitendo cha me kwa me, right?

Kile kitendo chenyew kiafrika pia ni private issue, ndo mana watu huwa hawatangazi. So, hizi kwa kuzuia ni kupunguza ukali wa tafsiri za baadhi ya mambo. Leo hii mtamzania akiona rangi nyingi nyingi kwenye nembo moja unamchabganya kwelikweli.. hii ni misinterpretation
Unaona unavyojing'ata ng'ata?

Maadili ni suala gumu ndo maana nikasema hakuna kiongozi anaweza kudhibiti maadili

Zamani kuoa binti wa 16 ilikuwa sawa, sasa hivi je?

Jamii ikiamua kubadilisha mtazamo juu ya jambo fulani, ni ngumu kuingilia.
 
Hizi muwape vijana sasa, ajira au volunteering, mbona mapambano yake ni mepesi mkihusisha wananchi wengi zaidi.
Na ndiyo lengo la program kwamba, wananchi wahuishwe kuanzia Kijiji, mtaa, kata. Na seti ya wajumbe ipo, na sasa ni kuchochea Kasi ya utendaji. Na Kila mmoja humu ajiulize kuhusu kamati ya mtaa wake, kata yake na Kijiji chake na atoe ushirikiano. Shukrani
 
Hivi unajua mshamba_mwingine tatizo la ushoga kwa kadri linavyozungumzwa ndivyo linavyozidi kuwa kubwa zaidi?. Hii kitaalam ni social constructionism... dah! 🥹 nishasahau na jina la muandishi. Uwinga kariakoo unaninyima muda
 
Muheshimiwa ni lini mtaanzisha kampeni ya kulinda ukatili dhidi ya wanaume!!?

Wanaume tunapitia stress nyingi kwenye maisha na Sheria hazipo upande wetu coz Sheria zinalinda watoto na mama zao sisi tunalindwa na Sheria zipi!!?

Au mnamuachia Mungu pekee !!?sisi hatuna haja ya kulindwa dhidi ya ukatili wa wanawake!!?

Hivi unajua kununiwa na kunyimwa unyumba Kwa sababu zozote zile ni ukatili wa kijinsia!!?

Hivi unajua sisi wanaume kufanywa kuwa ATM machine za Hela na Hawa mabinti ni ukatili kwetu!!?

Hivi unajua tukiwatongoza wanawake wanaumwa na njaa wakti huo huo,Kodi ya pango huisha wakati huo huo,pia mama yake mzazi huumwa wakati huo huo na bill husoma hasta laki tatu !!!?hata kabla ya tendo lenyewe !!!?Huo sio ukatili Muheshimiwa waziri!!!?

Tunaomba kampeni ya ukatili wa wanaume ianze rasmi na Sheria za kutulinda zianze rasmi!!
Aaarghaa . (Kwa sauti ya yule paka )
 
Mnafanya kazi kizmani na kijinga sana, ziara za nini? Mliandika maandiko yenu bila kufanya utafiti? Kuelimisha watiu karne hii kunategemea ziara kwa ana kwa ana? mnajitafutia ulaji tu.

Mnachotakiwa muwe nachoi ni Research center s ya/za kudumu na muwe mnafata ushauri wake.

Mimi nashangaa katika fagio lililopita wewe Gwajima kubakishwa licha ya maadili ya Mtanzania kushuka na kuwa kiwnago cha chini kabisa. Ushoga umeenea kila sehemu, kuanzia majumbani mpaka mashuleni.

Mtajingaisha sana, kinachotakiwa nchi isiwe mawakala wa shetani. Nje ya hapo hata mfanye nini mtaangukia pua.
Wacha ufala na wewe! Mbona unataka kukosa heshima?
 
Mabadiliko na mafanikio ya awamu ya kwanza ni kushuhudia kuibuka kwa wimbi la utekaji wa watoto ambalo halijawahi kuwepo kabla ya mpango huo kuanza:Kuna nini zaidi sasa..
Usisahau na wimbi la ushoga na usagaji linalotapakaa kama moto wa makumbi.

Rejea mikutano ya Mwakyembe.
 
Hii wizara ni muhimu sana kwa kila Mtanzania kwa kuwa inagusa maisha yetu ya kila siku, lakini watu wanaowekwa kuiendessha hawalioni hilo, wao kazi yao kuamuwa kesi za "singo maza" tu.
 
Unaona unavyojing'ata ng'ata?

Maadili ni suala gumu ndo maana nikasema hakuna kiongozi anaweza kudhibiti maadili

Zamani kuoa binti wa 16 ilikuwa sawa, sasa hivi je?

Jamii ikiamua kubadilisha mtazamo juu ya jambo fulani, ni ngumu kuingilia.
Hapo hili tatizo la mashoga limekuwa kubwa sabab hata publi figures wanaliongelea na kulikemea kila siku. Ni too overrated.. yani mashoga zaman walikuwepo ila kipindi hiki imekuwq kama fashion mana manabii, wabunge, mashehe kila kona ni hilo tu..

Juzi kuna mtu alimtuhum fally ipupa kuwa ni shoga eti sababu ya miuno yake ile ya eloko oyo. Sasa we unamuelewa huyu?
 
Mpango mzima umekaa ki- nadhalia zaidi kuliko uhalisia..Kwa mfano Usalama wa watoto sasa ni tete na matukio ya utekaji yanaendelea.4 na 5 Waziri anasema usalama umaimarika..Polisi wana kanusha.Rais anasema ni maigizo tu.Ziara hiyooo...wanaenda kutathimini mafanikio ..yapi.? Mbona ni kama namna tu ya upigaji?Na anakazia ziara zitafanyika nchi nzima na utekwaji nao umetamalaki kila mahali? Sasa ni nini..
Usipofanya ufuatiliaji wa jambo lako, litalala. Ufuatiliaji ni sehemu ya utekelezaji wa sekta zote ndiyo maana unaona viongozi mbalimbali wanafuatilia na kuelimisha na kutia moyo na kupokea maoni na changamoto... Kwa hiyo ni shughuli ya sekta zote tu na taasisi zote Tanzania na duniani yaani ni component ya utekelezaji. Hata huku kwenye familia unagawa kazi na unafuatilia, unatibu mgonjwa na unamfuatilia.... Unalima shamba na unafuatilia maendeleo kwa kwenda shambani.

Ahsante Sana kwa maoni yako
 
Back
Top Bottom