Ijue Ngerengere Air Base, ngome iliyofichwa milimani inayolinda anga la nchi yetu

Ijue Ngerengere Air Base, ngome iliyofichwa milimani inayolinda anga la nchi yetu

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
11,999
Reaction score
24,328
1000111383.jpg

Kambi ya Jeshi la Anga ya Ngerengere (Ngerengere Air Force Base - HTNG) ni kituo kikuu na cha kimkakati cha kijeshi chini ya Kamandi ya Jeshi la Anga. Kambi hii ipo katika kata ya Ngerengere, Wilaya ya Morogoro vijijini, Takriban kilomita 120 magharibi mwa jiji la Dar-Es-Salaam. Inatambulika kama ngome kuu ya ulinzi wa anga wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokana na jinsi ilivyofichwa katikati ya safu za Milima.

Kambi ya anga Ngerengere ilianza kujengwa mwishoni mwa miaka ya 1960 na kukamilika mapema miaka ya 1970 kwa ushirikiano mkubwa kutoka kwa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Lengo kuu la Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, lilikuwa kuunda kambi kuu ya kimkakati ambayo ingelinda anga la nchi dhidi ya maadui wa ndani na nje, Hasa kipindi ambacho nchi ilikuwa mstari wa mbele kuunga mkono harakati za ukombozi Kusini Mwa-Afrika.

Kambi hii ilikuwa kitovu kikuu cha kimkakati wakati wa Vita vya Kagera (1978–1979) dhidi ya Mtawala wa Uganda, Idi Amin Dada.

Wakati wa Vita hivi vikiendelea, tishio la mashambulizi ya anga yalipamba moto katika Mji wa Musoma. Katika hofu hiyo Jeshi la Tanzania lilituma ndege tatu kwenda kuongeza nguvu vitani na kundi hilo la ndege aina ya MiG lilikuwa likipaa angani kuelekea Uwanja wa Ndege wa Mwanza, likipita juu ya anga la Musoma.

Bila kujua kilichokuwa kikiendelea, Vikosi vya ulinzi wa anga vya Tanzania vilivyokuwa vikilinda eneo hilo vilibaki katika tahadhari kubwa. Kwa kuwa havikuwa vimepewa taarifa zozote kuhusu safari ya ndege hizo rafiki, Viliamini kwa dhati kuwa lilikuwa ni shambulio kutoka kwa adui.

Katika pigo la kusikitisha la kujipiga wenyewe (friendly fire), Makombora hatari ya SAM-2 yalirushwa mfululizo na kuzitungua ndege zote tatu tukio hili lililoacha alama ya huzuni na kielelezo cha changamoto kubwa za mawasiliano katika uwanja wa mapambano kwa Majeshi yetu.

Licha ya kutokea kwa makosa hayo lakini Kambi ya Ngerengere ilitoa mchango mkubwa sana wa kuendelea kurusha ndege za kivita kuelekea kagera na ubora wa marubani na Mafundi kutoka kwenye kambi hiyo kulilifanya taifa letu la Tanzania kuibuka kidedea kwenye vita hiyo.

Kati ya mwaka 2013 na 2015, Kambi ya Ngerengere ilifanyiwa ukarabati mkubwa sana uliogharimu zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 68.5, Mradi uliofadhiliwa na China ili kurefusha na kuimarisha barabara ya kurukia ndege (runway).

Kambi hii inahifadhi na kuendesha ndege za kivita, ndege za mafunzo na ndege kubwa za usafirishaji wa wanajeshi na mizigo.

Kambi ya anga Ngerengere Ina mifumo ya kisasa ya rada inayoweza kufuatilia chombo chochote kinachoingia kwenye anga la Tanzania kwa ushirikiano na vikosi vya ulinzi wa anga. Kuna mifumo ya makombora ya kutungulia ndege kwa ajili ya ulinzi wa dharura.

Pia, Kuna njia ya kimataifa ya Kurukia Ndege (Runway 02/20) Njia hii yenye urefu wa futi 7,900 na lami imara inayoruhusu hata ndege kubwa sana za kijeshi na mizigo kutua na kuruka bila shida.

Majukumu makuu ya Ngerengere Air base yanaenda sambamba na majukumu ya Kamandi ya Anga ya Jeshi la Wananchi waTanzania:

i. Kuzuia, kugundua na kuharibu chombo chochote cha adui kinachoingia kwenye anga la Tanzania bila kibali.

ii. Kusaidia vikosi vya nchi kavu (Infantry) na majini kwa kushambulia ngome za adui kutokea angani wakati wa operesheni za kivita.

iii. Kufanya mazoezi ya kimkakati ya kivita na kutoa mafunzo ya juu kwa marubani wapya (Fighter Pilots) pamoja na mafundi wa mitambo ya anga.

iv. Kusafirisha misaada na kufanya doria wakati wa majanga ya kitaifa kama mafuriko au dharura nyingine nchini na kikanda.

🇹🇿Tuna jeshi Imara sana na lipo tayari mda wote.

___________________________
Imeandikwa na Alfred Julius Kanyamala
Namba ya simu: 0744 367 973
Barua Pepe: [email protected]
 
Tena wamshukuru Kikwete alijenga hii njia ya ndege juzi juzi tu
Palikuwa zamani ni kama pori tu
View attachment 3679404
Watanzania tunapendaga sana kujisifia ufala kumbe hakuna kitu.

Stori za vijiweni huko utasikia JWTZ ni jeshi hatari sana, kumbe hamna kitu.

Juzi kati hapa wameenda Congo huko kutuliza vurugu za waasi M23. Wamepelekewa moto vibaya mno!

Na wengine wameuwawa. Lakini wamepiga kimya. Ili wasizue taharuki kwa Watanzania.
 
Back
Top Bottom