Usihukumu ukaja kuhukumiwa
..je wewe ni nani katika dunia hii hadi uhukumu au utoe muongozo wa kwamba fulani atahukumiwa..sio kazi yako...angali ya kwako kwanza ambayo utahukumiwa wewe peke yako..
Kila kitu kipo wazi na sisi sio kwamba tunaoteshwa haya mambo tunasema haki ile aliyokuja nayo mtume wetu na haya mambo madhara yake makubwa.
Allah anasema :
“Enyi Mlioamini! Bila shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli ni uchafu katika kazi za shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa” (5: 90).
Na Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza jambo hilo, hivyo inatakiwa tujiweke kando kabisa.
Mambo yote haya ni haramu na yeyote mwenye kuamini kuwa jambo fulani limetokea kwa sababu ya nyota kadhaa na kadhaa amemkanusha Allaahkama Alivyosema katika Hadiyth ifuatayo:
(Yeyote atakayejimai (kufanya kitendo cha ndoa) na mwanamke mwenye hedhi, au kwa kutumia njia ya nyuma, au kumkaribia mtabiri na kuamini aliyoambiwa, basi amekufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad))
[Hadiyth Sahiyh imesimuliwa na AsWhabus-Sunnan na wengineo]
Na kufanya hivyo ni kuingia katika elimu ya ghayb (mambo yaliyofichika ya Allaah) ambayo hakuna aijuwae ila Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) na humpeleka mtu kuingia katika shirk. Na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) humghufuria mtu dhambi zote ila shirk kama Alivyosema:
"Hakika Mwenyezi Mungu Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilokwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa"
(An-Nisaa: 48)
Sasa kwa maneno haya ya Allah na mtume wake hivi vitendo vinafaa kufumbiwa macho ? Jibu ni kinyume chake.