Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Mkuu hli swali ni zuri lakini kumwaga mtama kwenye kuku wengi kuna shida mkuu
Rakims
Mkuu sisi hatutachafua nyota yako....kwanza unajua namna ya kuisafisha!! Tupe mfano tu tangu umejua nyota yako pamoja na uhalisi wake.
 
Mwanaume ni Mizani, na Mwanamke ni Mshale, vipi khabari za maisha yao wanaweza kaa sawa ???
Mizani mara nyingi huamshwa na mshale kwa mambo yake ya maajabu na uwezo wake na mshale huwa anavutwa na mshale kwa ustaarabu wake wote ni wema kwa mmoja na mwenziwe ingawaje usawa wa maisha huletwa na mwenye mizani, mizani hupenda kufanya mipango kabla ya kukurupuka kwa mshale. la hukerwa kidogo na mikurupuko ya mshale japo kuwa mwisho wa siku couple hii hukaa sawa. wema na ustaarabu wa mizani humfanya huyu mwenye nyota ya mshale kutuliza mizuka yake na kufurahia maisha na mapenzi vema kutoka kwa mwenzi wake, kila mmoja kati yao hufurahia mapenzi ya furaha na utani pamoja na uchokozi lakini huwa ni watu wapo wazi sana kuingiza mahusiano mengine kuweza kuwapiga company.

Rakims
 
Rejea kwenye mapacha mkuu lakini tutataka kufahamu na iliyochomoza wakati anazaliwa

Rakims
Kiongozi kama ulipozaliwa ulipeowa jina fulani lakini baadae ukabadilisha jina ukaitwa jina jingine! Inakuaje hapo kwa suala la nyota?
 
🐮 = 🎨 × 🎶 🎹 🎬 🎸 🎺 🎻 🎵 🎥 🎨 ⚽💻 ⌨ 👚 💡 📜
 
Mfano na swali :
Kama nyota ya kaa ni july 21 na 20 au jina Herufi A,
Je akizaliwa 21 july na jina herufi Q atafuata ipi?
Herufi au tarehe?
 
Mkuu naomba nyota ya mizani uiekezee vya kutosha kama hizo nyingine!
 
Sasa nielewe mkuu huyu Nyota yake ni mapacha nyota liyochomoza wakati anazaliwa ni samaki, nyota ya ndani yake ni mapacha yaani huyu ni mapacha thabiti isipokuwa anavitabia vya samaki na pia nyota ya jina lake ni Simba maana yake nini sasa kwa sababu
Huyu teyari nyota yake ni upepo na tabia zake ni samaki teyari mkosi wake ni yeye mwenyewe mambo yake atakuwa hadi ayalazimishe sana na pia atakuwa ni mtu mwenye kuudhika kirahisi sana kutokana na kuzaliwa kwake chini ya combination zisizo elewana pia ni mtu ambaye ana bahati sana isipokuwa kitakachomuharibia kwenye mapenzi ni mkali sana na mwenye ghadhabu hawezi kuishi na mke au mume kwa amani hadi apate pete ya kupunch huyo nyota ya samaki ili awe gemini kamili na pia kinachokuja kumsumbua ni kwamba akipata pesa huwa anatumia hovyo inayayuka kama moto vile vile watu humuogopa hasa jinsia tofauti na yeye humkimbia na kumuona yeye kama kisiriri hivi, na anamatumizi ya fujo sana hasa kwa starehe na umalaya pia huwa anamajungu na fitina

Huyu pia tunampata kuwa huyu ni mtu wa kujihisi kuwa yeye tu peke yake ndio huonekana mkosefu na asiye na muelekeo lakini pia hujihisi kuonewa siku zote na huona kutengwa na dunia lakini pia kwa uwazi ni mtu mzuri..

mkuu naishia hapo kuna mengi ya kusema lakini nitakuwa kama vile nimetengeneza thread ndani ya thread kama kwa mkuu Bujibuji hapo

Rakims
 
Back
Top Bottom