Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Rakims ebu dadafua vizuri jinsi ya kujua nyote yako kama tarehe ya kuzaliwa na jina zipo makundi tofauti, dafafua kuwezesha mtu kucalculate na kupata nyota hasa ni ipi.
 
Mkuu nimelieleza hili mwanzoni mwa thread ya kwamba ili uweze kujua nyota yako lazima ufahamu mambo manne na kuweza kuyalinganisha ndio unapata nyota yako sahihi sio wewe tu wengine huona hata maelezo yake ni batili na walivyo kwa sababu mtu unakuta anaangalia nyota ya mwezi wakati inakinzana na nyota iliyochomoza saa na siku anayozaliwa. narudia ili kuweza kujua nyota yako sahhi hivi details lazima uwe nazo kama hauna kuna njia za kutumia ukazipata

Rakims
Nilitaka kuuliza hili swali uliloulizwa bahati nzuri likaulizwa mapema.

Naomba kufahamu namna ya kutambua nyota yangu kwa usahihi japo sijui tarehe yangu ya kuzaliwa
 
Mimi nyota yangu nimeijua kupitia tarh na mwezi niliozaliwa. Lkn herufi ya jina langu ni tofauti na ulivyoandika. Hii inaweza kuleta shida gani? Mimi ni simba lkn jina langu limeanzia herufi M
 
Yaani hiyo nyota ya punda umenipatia kabisa
Ugonjwa mimi huwa ni kichwa tu hata leo nimetoka hospital kujitibu kichwa lakini maumivu yake nayo sikia ni balaa.!
Nyota haipo vizuri mkuu ikiwa vizuri utakuwa mwenye raha na hisia sana kichwani

Rakims
 
Hivi vitu sio vya kishetani? Yaani nimeangalia yangu na ya mr wangu yaani ni kama vile wametustudy sisi kuandika waliyoandika
 
Rakims ebu dadafua vizuri jinsi ya kujua nyote yako kama tarehe ya kuzaliwa na jina zipo makundi tofauti, dafafua kuwezesha mtu kucalculate na kupata nyota hasa ni ipi.
Hapo inachohitajika ni kujua jina la mhusika na mama yake, kisha unapiga hesabu baada ya hapo unaitafuta kwenye mwezi kisha mwaka kisha siku kisha majira kisha saa kisha unapata uwiano kamili kama saa huifahamu basi ujue ilikuwa usiku au mchana

Rakims
 
Nilitaka kuuliza hili swali uliloulizwa bahati nzuri likaulizwa mapema.

Naomba kufahamu namna ya kutambua nyota yangu kwa usahihi japo sijui tarehe yangu ya kuzaliwa
pole mkuu lakini haina shida ni details zipi unazozifahamu kuhusu wewe? mwaka wa kuzaliwa? jina lako na mama yako? mwezi wa kuzaliwa ukitaja hivyo nitakurudisha kwenye nyota yako sahihi

Rakims
 
Mimi nyota yangu nimeijua kupitia tarh na mwezi niliozaliwa. Lkn herufi ya jina langu ni tofauti na ulivyoandika. Hii inaweza kuleta shida gani? Mimi ni simba lkn jina langu limeanzia herufi M
mkuu shida huja pale ambapo unazaliwa ilikuwa mchana au usiku na ilichomoza nyota gani hiyo ndio shida zaidi

Rakims
 
Mwanaume ni Mizani, na Mwanamke ni Mshale, vipi khabari za maisha yao wanaweza kaa sawa ???
 
Hivi vitu sio vya kishetani? Yaani nimeangalia yangu na ya mr wangu yaani ni kama vile wametustudy sisi kuandika waliyoandika
hapana mkuu hamna ushetani hapo ni ukweli ndio upo hapo kwa sababu hii imeanzia siku unazaliwa hadi leo inatunza record

Rakims
 
Back
Top Bottom