Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako

Nyota ya mapacha na kaa zinaendana kwenye mahusiano ya kimapenzi
Mapenzi aliyonayo kaa humfanya mapacha akidhi mahitaji yake ya kimapenzi, utulivu wa maneno ya mapacha nao humfanya Kaa kutuliza na kuliwazika sana. lakini mapema tu nyota ya Mapacha hugeuka kimapenzi na kuanza kusababisha majeraha ya moyo kwa kaa ambaye yeye huwa busy na kujenga au kupangilia familia yake. Tabia za mapacha kutongoza au kutongozwa hovyo huwa zinamkosesha amani kaa na kumuweka katika hisia za maumivu hawa wawili wanaweza kukaa kwa muda mrefu kwa kuwa tu kaa huwa mvumilivu lakini pale ambapo kaa atataka kufuata hisia zake na kufunga nyota hii kichomi ya mapacha wakati huo yenyewe huwa inahitaji uhuru wa kujiachia basi maneno mabaya ya Mapacha na kero humfanya Kaa kujiengua na Mapacha hujihisi uhuru nae kaa huhisi katoka kifungoni.

Rakims
 
Naomba unifafanulie kuwa; tarehe niliyozaliwa ni 27/Jan. na Jina langu
Lina anzia na herufi "M" .

Hivyo basis; katika maelezo yako nyota yangu ni IPI? Kwani ukiitafuta kwa herufi ya mwanzo wa jina "M" ni nyota ya "Punda"
Na ukiitafuta kwa tarehe ya kuzaliwa INA angukia "Ndoo" 27/January

Nipe ufafanuzi Mkuu.
 
Ndoo ndio nyota yako thabiti lakini hii punda ni tabia ya nyota yako umeelewa?
 
Vipi kuhusu mwanamke wa punda na mwanaume wa nge, couple hiyo vipi
Mapenzi kwao huwa ni moto hasa ukizingatia wote hawa ni nyota zenye muhemko mkubwa kimapenzi hasa katika ngono kila mmoja humuona mwenzie anayaweza zaidi mapenzi kuliko mwingine hasa ukiangalia sihemu za hisia za punda ni kichwa na ng'e ni sehemu za siri basi hawa hawawezi kukaa muda mrefu bila kutaka kukutana kimapenzi, nyota hizi ni zenye kupendeza katika ufanyaji ngono lakini kwenye hisia za mapenzi ya kweli hapo watakuwa wanatapeliana. Kila mmoja atataka kuwa mfalme au malkia wa mapenzi kwa mwenzie ambapo roho ya wivu ya nge itasimama thabiti kuhakikisha hili halifanikishiki kwa Punda. Punda nae kwa kawaida ni kiongozi na Jeuri hata kubali kuwa chini ya Ng'e hata lisaa moja hivyo couple hii haita chukua muda zaidi ya kufurahia uhawara na sio maisha ya ndoa hasa ukiangalia punda ni moto na ng'e ni maji ya moto. hivyo Punda atamchemsha Ng'e na Ng'e atamzima punda hamna Heri hapo kwanza hawa watu huwa kukaa karibu muda mrefu hawawezi

Rakims
 
Nyota yangu kupitia maelezo jina halisi lina anzia H nimefatilia kiukweli hii kitu ni kweli nimekua kiongoz tokea msingi mpaka chuo nilikua rais ,alafu nimesomea afya saiz natibu raia,alafu nikimpenda manzi nikiweka nia lazima ni mle hata kama amenizidi kila kitu mambo ni mengi ambayo yamenigusa binafsi mtoa mada ,bravo uko vizuri [emoji860]
 
Mkuu Rakim mimi nyota yangu ni mshale, sijaona kama umeichambua pale kwenye post #1.

Tuchambulie tafadhali.
 
Shukran mkuu, pamoja sana.

Rakims
 
Kuichambua vipi sijaelewa, mkuu
Niambie nikuchambulie wapi?
Kati ya zile nyota 12 umeorodhesha 11 tu. Kwa hiyo nyota ya mshale haipo hapo kwenye post yako no 1, hivyo hujaitolea maelezo kama hizo nyingine 11.
 
Ndoo ndio nyota yako thabiti lakini hii punda ni tabia ya nyota yako umeelewa?
Sijaelewa!, naomba majibu Haya;

Punda siyo nyota ?

Inakuwaje nyota nyingine inakuwa na tabia ya nyota nyingine?

Nyota ya ndoo aina tabia zake mpaka ipewe tabia za nyota ya punda ?

Ninapofuatilia nyota nifuatilie tabia zipi kati ya ndoo na punda ?

Kipi chenye nguvu kati ya tabia ya MTU zisizotoka nyota take na nyota take katika kufuatilia mienendo ya kila Sikh ya elimu Hui?


Ufafanuzi wako mkuu.
 
Hakuna uhalisia wowote, inakuwaje herufi ya kwanza ya jina iwe nyota nyingine na mwezi aliozaliwa uwe nyota nyingine, sasa ina maana mtu huyo huyo mmoja ana nyota mbili tofauti??
 
Hakuna uhalisia wowote, inakuwaje herufi ya kwanza ya jina iwe nyota nyingine na mwezi aliozaliwa uwe nyota nyingine, sasa ina maana mtu huyo huyo mmoja ana nyota mbili tofauti??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…