hongera mkuu kw bandiko lako mm ni miongoni mwa watu wanaokufatilia sana kwenye nondo zko ukianzia kule google mpaka tovuti mbalimbali wacha tuje kwenye point ebwna mim tarehe yangu ya kuzaliwa ni 23 sept ,nlizaliwa jumatano kiukweli mengi uliyoyadadavua kuhusu huo mwez na tarehe ni kama ulietabir ukianzia maradhi ,tabia n.k ila nlibata bahati ya kuoana na bint ambae yeye alizaliwa ndani ya mwezi wa july 31 bila shaka atakua anahusiana na nyota ya simba sasa vipi mafahari hawa kati ya mizani na simba kuna mafanikio gani labda au mikosi ambayo yatakayoweza kujitokeza kwenye maisha?uwanja wako mkuu rakims kwa faida ya wote elezea
Tuanza kwa mtizamo wake kinyota kwako na jinsi mnavyoendana kwa upande wake ni kwamba yeye kwako anakuwa ni mwenye kwenda vizuri na wewe jinsi unavyoonekana mwenye sanaa ya ubunifu na kutumia vema kipaji ulichonacho.
Yeye ni mwenye kuonekana zaidi kuvutika katika upande madhubuti wa mapenzi au mwenye mapenzi zaidi na wewe
kuliko wewe mwenyewe, lakini mtindo wake mara nyingi unaweza kukushinda.
Kwake wewe ni mtu usie na uamuzi na yeye ndio mwenye kupenda kuchukua majukumu ya utawala wa mahusiano
mnaonekana ni watu ambao mnaweza msiendane kwa sababu nyote ni wenye fujo na hupenda mazingira mazuri ambayo
yenye kung'ara yaani usafi. Kila mmoja pia atajaribu kumshinda mwenzake kwa utaratibu wake ni kama mahusiano ya ushindani.
Lakini chumbani yeye anakuzidi, na yeye ni simba hivyo huwa ni malikia wa mambo hayo na mwenye kupenda sifa katika tendo la ndoa.
MTIZAMO WAKO KWAKE:
ajabu,kasi na nguvu yake pamoja na jinsi alivyo mkarimu, katika mapenzi basi huwasha moto wa mapenzi kwako, na kama ungekuwa unapimwa kwa kipima joto huenda hadi mwisho.
Wewe unaonekana ni mwenye kuonekana kupumbazika nae kijinga, lakini hilo halitakuwa shida kwako kutokana na busara.
Kiukweli mahusiano haya kama ni mzozo basi ni kidogo, Wewe unaonekana ni mwenye kujua jinsi ya kujitolea kwake kwa uzuri.
Pamoja mnaonekana ni wenye kushiriki upendo wa anasa,
kwenda kwenye tafrija, na kuunda nyumba nzuri ambayo hutumika kama hatua ya kuweka hizi nyota mbili katika upendo kwa hivyo mnaendana.
Rakims