Baba Kisarii
JF-Expert Member
- May 7, 2024
- 1,844
- 3,089
Nyumba Ntobhu maana yake ni "nyumba bila mwanamume" ni aina ya muungano wa jadi usio wa mapenzi ya jinsia moja miongoni mwa wanawake wa kabila la wajaluo Mkoani Mara - ushirikiano huundwa kati ya wanawake wakubwa kiumri na wanaojiweza kiuchumi, ambao kwa kawaida wanawake hao huwa ni wajane au wanawake wa kawaida wasio na uwezo wa kuzaa watoto ambapo hushirikiana na wanawake mabinti wadogo wasio na watoto, wanaojulikana kama mokamööna (mabinti wakwe).
Ni nyumba inayoongozwa na mwanamke kama baba na huwa hakuna mwanaume katika familia hiyo japo kuna watoto wanazaliwa.
Iko hivi....
Mwanamke mwenye uwezo na umri mkubwa anaoa mdada kijana ili ampatie uzao
Mdada akiolewa na huyo mwanamke mwenzie atatafuta mimba kwa mwanaume yeyote... yaani anakuwa anaenda kufanya ngono na mwanaume yeyote hadi apate mimba na kuzaa. Mwanamke aliyemuoa mdada ndiyo anakuwa 'baba' wa kulea mtoto au watoto watakaozaliwa na huyo mdada.
Hapo huyo mwanaume mtia Mimba hatatambuliwa kwa hiyo familia na wala hatajua kama alimtia mimba huyo mdada maana jambo hilo huwa ni siri kwa mdada na mwanamke aliyemuoa.
Kwa kutiwa mimba na wanaume mbalimbali mdada atazaa watoto kadri awezavyo na hao watoto watatumia ubin wa huyo mwanamke.
Hiyo ndiyo Nyumba Ntobhu ujaluoni.
Aliyebuni Nyumba Ntobhu apewe heshima yake kwa ubunifu huo wa kijadi.