Nawakaribisha wapenzi wa Singeli,Wanazuoni wa sanaa ,watoto wa kitaa ,Ma itteligentsia wote na wataalamu wa codes.
Hebu tuambieni hizi namba zinazotajwa kwenye muziki wa singeli zina maana gani??
#32
#26
#45
n.k
TAHADHARI:UKITAKA KUIELEWA NA KUIPENDA SINGELI SIKILIZA KATIKATI YA MISTARI (BETWEEXT THE LINE)
Naweza elezea 26 Kwa uchache kidogo.
Hii namba ya 26 ni mzaliwa wa namba 27 kutoka gerezani south Africa.
Wenye asili ya 26 walikuwa ni wacheza Kamali gerezani wakati huo hakuna habari Za namba kwenye magereza ya south Africa na wakati huo kulikuwa na utawala wa kimabavu tu yaani mwili mkubwa ndio mtawala.
Sasa ndio wakaingia jela ndugu wawili Kwa kosa la kumuua baba yao mzazi.
Hapa panazaliwa 28 na 27.
Kipindi Wapo jela walikuwa wote ni wababe na pia walianza kujibebea wafuasi.
Huyu 28 ndio mkubwa anaitwa Nongoloza.
27 ni mdogo mtu.
Majukumu ya kikazi yakaanza.
28 anafanya Kazi usiku yani jua linapozama USHONALANGA.
27 anafanya kazi jua linapochomoza MPUMALANGA.
Huyu 28 alikuwa na itikadi za kishoga.Yaani kuwaingilia wanaume wenzie gerezani na 27 Hana mambo hayo.
Sasa katika harakati za hapa na pale 28 akaona kundi la watu wanacheza Kamali na MTU anapigwa biti anatoa hela hii.Sasa 28 akaanza kuwaletea namba yaani kujitambulisha na kutaka kuwalawiti madogo,27 akaingilia kutetea msala na Jambo likaisha.
Baada ya uchunguzi wa 27 aliufanya Kwa wale magogo akagundua Hawa kupata kwao kitu gerezani humpandishia mtu biti Hadi anakuwa mnyonge Sasa rasmi namba 26 ikazaliwa na pia wakajiita MPUMALANGA mana wengi wao katika kundi like walikuwa wanatokea jimbo la Mpumalanga.
28 kuna Aina mbili kuna ya kuchanua na yakufunga.
Ili upate namba ya kufunga 28 lazima ufanye Jambo yaani uue mfungwa au Askari au upewe kitu ufiche na usitaje hata Askari gereza wakupige nusu ya kufa usitaje.Hapo Sasa unapewa cheo kidogo na kuanza kukontrol baadhi ya maeneo.Kwahiyo unakuwa upewe namba Kwa maumivu makali na pia unaweza kutunza Siri za jeshi la namba hata iweze.
Ukishindwa kuvumilia kipigo na bado unataka namba basi ni lazima uinunue namba Kwa Hela au Kwa kulawitiwa.
27 wao ni namba moja tu na siraha zao kubwa ni bunduki visu vioo ya vitu vyenye ncha Kali.
Hapo nimeelieza Kwa ufupi wakuu.
Kwahiyo namba kubwa ni mbili Tu.
28
27
Ukijiita wee ni namba basi wakubwa wako watakuuliza umeifanyia nini namba yako na ukishindwa basi adhabu Kali utapata pengine hata kifo.
Kwahiyo nawaangaliwa wadogo zetu wanaojiita hizi namba na hawajui nini maana.