Ijue sayansi ya chanjo hizi na chimbuko la wasiwasi wake. Hata Ulaya ni 5% tu ndiyo wamechanja katika miezi 3. Je, wanatusubiri sisi?


Kwamba?



Au nasema uongo ndugu zangu?
 

Hata Israel kwa makusudi haimo kwenye list kwamba hakuiona.

Mijamaa hii ina maslahi makubwa na vifo vya watu.

Yumkini ndiyo hii inayosemekana kuwa ilichanjiwa chattle.
 
Yani hata neno akili hujui linavyoandikwa lakini unamwambia mwenzako atumie akili!! Sasa watu kama wewe ndiyo washauri wa jiwe hapo unategemea nini cha maana?

Hiyo mijamaa bure kabisa. Kila mafanikio ya Chanjo au tiba inapopatikana dhidi ya ugonjwa huu kwao ni msiba mkubwa.

Inajifanya yenyewe kuwa na mamlaka ya uamuzi wa juu ya wengine kufa au kuishi.

Kusikia kwao ni kwa kenge!

Hiiiiii bagosha!
 
Hizi chanjo kwa watanzania waishio huko Ulaya na Marekani na nchi zingine za mashariki ya mbali, hizi chanjo zitakuwa ni lazima.

Sababu kuu ni kwamba ukitaka kusafiri kwa wale wanosafiri mara kwa mara , cheti maalum cha chanjo kinaandaliwa baina ya nchi za Ulaya na kwingine ili kusaidia sekta ya usafri wa anga ambayo ipo ICU.

Mashirika ya ndege yote yatapewa mwongozo na serikali mbalimbali kuhakikisha waangalia hicho cheti na kama huna basi ndege hupandi.

Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba kama chanjo zinatolewa ziwe ni kwa ajili ya kuwachanja wale wote wenye matatizo ya kiafya underline conditions kama pumu, na HBP lakini sio wale walo na magonjwa ya kuelekea kaburini.

Pia wale wote wanohitaji kusafiri kwenye Ulaya na kwingine ambako kwahitajika uthibitisho wa kwamba msafiri amedungwa sindano ya chanjo ni lazima wapigwe chanjo.

Hivyo hii michezo ya kutumia akili au "mind games"ipitiwe upya na serikali iangalie ni chanjo ipi yafaa kununuliwa au kupewa bure au kuwa ni sehemu ya mkopo.

Mwisho wa siku ni lazima kutakuwa na watanzania wanotaka kusafiri kwenda nje (wakiwemo viongozi wa serikali) na ni lazima wawe wamechanjwa na pia wananchi ambao wa matatizo ya kupumua ambao pengine wangepatiwa chanjo basi wangeepushwa na vifo.
 
Germany's vaccine commission has approved the use of the Oxford-AstraZeneca jab in people aged over 65.
 
Takwimu za kweli na zinazoeleweka kuhusu masuala ya afya zinapatikana WHO. Hizo za akina John Efflein na wengineo zitakupoteza, hasa kama hujui kuzitafisiri kitaluma.

Chanjo zinatolewa kwa utaratibu maalum wa doses zake. Dose ya kwanza ni ya kusituwa tu (activate or prime) hizo seli za askari wa kinga (T memory & B memory cells). Dose ya kwanza haikupi kinga yo yote. Unahitaji doses zingine baada ya kipindi fulani (booster doses). Kwa hizi chanjo za covid-19 unahitaji dose ya pili baada ya wiki 4 kwa Moderna na AstraZeneca na wiki 3 kwa zile chanjo za aina nyingine. Hapo ndipo tunasema umepata chanjo (fully vaccinated) itakayoweza kukukinga usipate ugonjwa huo kwa kipindi fulani - kipindi hiki kwa kawaida ni miezi 6 ambapo utalazimika kupata booster dose nyingine etc

Hivyo takwimu tunazo ongelea hapa ni za wale waliopata full vaccination hasa huko ulaya, kwa wazungu na amerika ambao ni miezi 3 sasa tangia waanze kuchanjana. Hatuongelei takwimu za idadi ya doses zilizotolewa kwani hilo ni la wahasibu, sisi halituhusu. Tunaongelea ni watu wangapi wamepata dose ya kwanza na wangapi wamekamilisha chanjo:

1. Israel: Hii si nchi ya ulaya wala watu wake si wazungu bali ni waarabu. Halafu ni kainchi kadogo sana kenye watu million 9 tu kanpitwa na Burundi yenye watu million 12. Hivyo takwimu zake haziwezi kubadili cha maana huo wastani wa uchanjaji. Takwimu za sahihi za Israel toka WHO hadi tarehe 5 March 2021 ni:
- At least 1 dose 4,901,162 people sawa na 54.14%
-Full vaccinated 3,654,820 peopĺe sawa na 40,3%

2. United Kingdom:
Huyu ndiye alikuwa wa kwanza huko ulaya kuanza kuchanja watu wake tarehe 8 December 2020. Tena alianza kwa mbwembwe nyingi akifurahia uhuru wa kujitoa kwenye Umoja wa ulaya. Kwamba halazimiki kusubiri maamuzi ya EU kuanza uchanjaji. Hadi tarehe 5 March takwimu zake ziko hivi:
  • At least 1 dose 21,358,815 =32%
  • Fully vaccinated 3,660,333 = 1.5%

Yaani watu wake wengi baada ya kudungwa hiyo sindano ya kwanza waliingia mitini. Walikataa kurudi kukamilisha chanjo baada ya wiki 3 kama masharti ya chanjo ya AstraZeneca yanavyotaka. Yaani ni aibu. Full vaccination rate yake ni 1.5% tu. Halafu katuletea machanjo yake hayo bure sisi waafrika. Wewe unataka tumweleweje huyu mzungu tajiri na ugonjwa huu unatesa sana wananchi wake?

3. Haya takwimu za full vaccination coverage za WHO za nchi za wazungu na waarabu hadi tarehe 5 March hizi hapa:

One dose Full vaccination
Russia 3.4% 1.2%
France 5.1% 2.7%
Italy 5.9% 2.6%
Germany 5.7% 2.8%
Belgium 4.9% 2.9%
Greece 6.5% 3.4%
Spain 6.7% 2.8%
Turkey 9.1% 2.8%
Bulgaria 3.3% 0.7%
Hungary 9.7% 3.1%
United Kingdom 32%. 1.5%
Israel 54.1% 40.4%
Morocco 10.6% 1.4%
USA 16.9% 8.7%

World 2.2% 0.8%


Hizo ndizo takwimu za kweli zizoko WHO. Efficacy inayooneshwa kwenye hizo chanjo ni ya baada ya kupata full vaccination. Hiyo dose moja ya kwanza haikupi kinga yo yote bali ni ya maandalizi tu ya immune system yako. Unahitaji dose ya pili (booster) baada ya wiki nne au tatu kutegemea na aina ya chanjo. Hapo ndipo tunasema umepata full vaccination. Na badoinawezekana ukahitaji booster dose nyngine baada ya miezi sita na kila mwaka baada ya hapo.

Tukisema Efficacy ya chanjo ya AstraZeneca ni 62% maana yake ni kuwa katika watu 100 waliopata full vaccination, watu 62 kati yao watakuwa miili yao imepata kinga (immunity) ya ugonjwa huo, hao 38 waliobaki hawatapata kinga yo yote dhidi ya ugonjwa huo yaani wako sawa tu na wale ambao hawakuchanja kabisa. Hakuna cha kinga kidogo. Tatizo huwezi ukawatambua au kwa vipimo kujua katika hao 100 nani kafanikiwa mwili wake kupata kinga. Kipimo pekee ni kukutana na kirusi hicho - kama hakitakugalagaza basi wewe utajua uko kwenye kundi hilo la watu 62. Full vaccination haimaanishi full immunization. Yaani kati ya watu 100 wanaopata full vaccination ya Astrazeneca vaccine ni 62 tu ndiyo wanapata full immunization against CoV-2.

Lengo kuu la chanjo dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ni kupata angalao 60% ya watu wawe na kinga (fully immunized) ili kupata herd immunity to cut off transmission. Kwa mwendo huu wa matokeo ya chanjo kama hii ya AstraZeneca tusahau kufikia hiyo 60% herd immunity.
 
Nenda kenya au rwanda ukachanjwe
 
Nenda kenya au rwanda ukachanjwe

Hata huko chanjo zilizopo haziwatoshi wananchi wao tu. Si leo na labda wala mwaka huu kuwa watakuwa wamepokea zakuwatosheleza, sembuse na za kuchanja makapuku toke usengeremani?

Kila chanjo iliyopo katika nchi iko tagged kwa namba yake ya NIDA.

Ila huyu hapa:




Kwa anayotufanyia sisi tunaoihitaji mno hii chanjo, ana kesi ya kujibu angalau kwa kila kifo tangia pale alipogoma kuzipokea tu chanjo za ugonjwa huu.

Si umewasikia japo Padre wa Kilimanjaro na yule msomi wa Dar achilia mbali huku mitaani. Hao ni leo tu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
All mass medias will propagate biological war for certain states survival as super powers, in this war the majority will die both the ignorant and innocents,, and they will come with solution under the so called problem-reaction-solution plan(prs), in the name of humanity the ignorant wll be forced to receive their achieved solutions, and in that way a world will be controlled very simple by the builders.
666



Sijuii huyu mtu asiye julikana alisema kisichojulikana na kikapotelea kusiko julikana!!!!!?
 
Mkuu hizo huwa ni kelele za mitandaoni tu,unaweza ukaleta chanjo na kuwaita huko mitaani na asitokee hata mmoja.
 
Tangu nigundue wewe ni taahira, sijawahi kupata tabu

Kama ambavyo tangu nigundue kuwa katika mataahira wewe ni mama lao, katu haijawahi kabisa kunipa taabu tena:



Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Tunaomba version za wanasayansi wetu. Kama hakuna chanjo kutoka Afrika basi huakuna haja ya kupinga hizo chanjo.Miaka yote tumekuwa tukichanjwa chanjo ila ya corona tumejifanya tunajua huku hatuna ugunduzi wa dawa yoyote ya maana.
 
Yaani mnasema as if mtu anaenda tu kupata chanjo akiamua, kama vile mtu anaenda sokoni, mnashindwa kuelewa zinatolewa chanjo kwa prioritization, wazee na wale at risk ndio walianza kuwa vaccinated, sasa uhesabu hesabu yao hao wazee ni wangapi in total UK population?
 
Umezungumza kiutaalam Sana, shida ni hawa watu wa bavicha. Subiri uone
Kama bavicha ndiyo walileta corona na chanjo kaa hivyo hivyo,,
Ndiyo maana kwa baadhi ya nchi za Africa kuendelea ni ndoto,,toka uhuru mpaka sasa mnaongoza wenyewe mmeshindwa hata kutengeneza chanjo,, mtaendelea kulamba miguu ya watu weupe mpaka mtoke madarakani, maana hamjui hata kuongoza wananchi zaidi ya misafi tu na ubinafsi
 
Hili ndiyo tatizo. Yaani watu wanadhani elimu inapatikana kwenye kampuni ya wamarekani inayoitwa google badala ya shuleni na vyuoni. Wao ni ku google tu na cho chote watakachokipata huko google wanaamini ndiyo ukweli.
Hata walimu wa vyuo huwa wanampenda sana MR.GOOGLE.Vitabu vyote vipo google, yani chuo kikaizidi google we! umesomea wapi ndugu mbona unatia mashaka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…