Ninarudia kusema, wewe kama siyo mtalaamu wa mambo utanukuu takwimu ambazo hujui zinachomaanisha.
Tuchukue mfano wa United Arab Emirates kwenye takwimu ulizozinukuu. Yeye takwimu zake alizopeleka WHO ni kuwa: Dose given to 6,235,316 people
Hence doses per 100 people = 63.82%
Kwa takwimu hizo wewe unazichukulia kama waliopata chanjo UAE ni asilimia 63.82%. Ni layman tu wa sayansi hii ndiye atazichukulia hivyo. Kwa msomi takwimu hizo haziko kamili kwani hatuwezi kujua kiasi cha watu ambao miili yao imepata kinga dhidi ya CoV-2. Inawezekana hao watu wote 6,235,316 wamepata dose moja moja tu ya hiyo chanjo, kitu ambacho hakiwapi kinga yo yote.
Sisi tunataka takwimu za watu waliopata chanjo kamili - yaani fully vaccinated. Si wale wanaochoma sindano moja ya kwanza halafu wanaingia mitini wakitusubiri sisi waafrika.
Mfano wa pili ni wa United Kingdom: Yeye kama zilivyo nchi nyingi kawakilisha takwimu zote zinazohitajika ambazo ziko hivi:
- At least 1 dose given 21,358,815 people equal to 32% of the population
- Full vaccinated 1,034,068 people = 1.55% of the population.
Hizi ndizo takwimu tunazosema kwamba kuanzia Dec 2020 UK ni 1.55% tu ndiyo amefanikiwa kuwapa chanjo (full vaccination) na kwamba wengi waliopata dose ya kwamba hawakurudi kupata hiyo dose ya pili. Sasa wewe unachukua hiyo takwimu ya dose ya kwanza kwamba ndiyo ya maana.
Israel takwimu zake ni:
-At least 1 dose 4,903,857 people = 54.17% as per 5 March 2021
-Full vaccinated 3,660,333 = 40.43
Ikumbukwe Israel ni nchi ndogo sana yenye population ya 9 million tu inapitwa na Burundi yenye watu million12. Israel karibu kila mtu mzima ni mwanajeshi.
Kuhusu China: China haipeleki takwimu zo zote WHO kwani walishaiuzi. FDAs za wazungu zilishakataa kutoa hata hizo emergency approval ya vaccines za kutoka Uchina na Urusi. Hivyo usitegemee kupata takwimu ya maana hapo WHO kutoka China.
Ninakunakilia hapa nilichomjibu Ayb kwenye thread # 66 maana munaendelea kubishi mambo msiyo na ufahamu nayo wa kutosha. Mnaendelea kuhoji na kukosoa mambo ambayo nilishayatolea majibu:
Takwimu za kweli na zinazoeleweka kuhusu masuala ya afya zinapatikana WHO. Hizo za akina John Efflein na wengineo zitakupoteza, hasa kama hujui kuzitafisiri kitaluma.
Chanjo zinatolewa kwa utaratibu maalum wa doses zake. Dose ya kwanza ni ya kusituwa tu (activate or prime) hizo seli za askari wa kinga (T memory & B memory cells). Dose ya kwanza haikupi kinga yo yote. Unahitaji doses zingine baada ya kipindi fulani (booster doses). Kwa hizi chanjo za covid-19 unahitaji dose ya pili baada ya wiki 4 kwa Moderna na AstraZeneca na wiki 3 kwa zile chanjo za aina nyingine. Hapo ndipo tunasema umepata chanjo (fully vaccinated) itakayoweza kukukinga usipate ugonjwa huo kwa kipindi fulani - kipindi hiki kwa kawaida ni miezi 6 ambapo utalazimika kupata booster dose nyingine etc
Hivyo takwimu tunazo ongelea hapa ni za wale waliopata full vaccination hasa huko ulaya, kwa wazungu na amerika ambao ni miezi 3 sasa tangia waanze kuchanjana. Hatuongelei takwimu za idadi ya doses zilizotolewa kwani hilo ni la wahasibu, sisi halituhusu. Tunaongelea ni watu wangapi wamepata dose ya kwanza na wangapi wamekamilisha chanjo:
1. Israel: Hii si nchi ya ulaya wala watu wake si wazungu bali ni waarabu. Halafu ni kainchi kadogo sana kenye watu million 9 tu kanpitwa na Burundi yenye watu million 12. Hivyo takwimu zake haziwezi kubadili cha maana huo wastani wa uchanjaji. Takwimu za sahihi za Israel toka WHO hadi tarehe 5 March 2021 ni:
- At least 1 dose 4,901,162 people sawa na 54.14%
-Full vaccinated 3,654,820 peopĺe sawa na 40,3%
2. United Kingdom:
Huyu ndiye alikuwa wa kwanza huko ulaya kuanza kuchanja watu wake tarehe 8 December 2020. Tena alianza kwa mbwembwe nyingi akifurahia uhuru wa kujitoa kwenye Umoja wa ulaya. Kwamba halazimiki kusubiri maamuzi ya EU kuanza uchanjaji. Hadi tarehe 5 March takwimu zake ziko hivi:
- At least 1 dose 21,358,815 =32%
- Fully vaccinated 3,660,333 = 1.5%
Yaani watu wake wengi baada ya kudungwa hiyo sindano ya kwanza waliingia mitini. Walikataa kurudi kukamilisha chanjo baada ya wiki 3 kama masharti ya chanjo ya AstraZeneca yanavyotaka. Yaani ni aibu. Full vaccination rate yake ni 1.5% tu. Halafu katuletea machanjo yake hayo bure sisi waafrika. Wewe unataka tumweleweje huyu mzungu tajiri na ugonjwa huu unatesa sana wananchi wake?
3. Haya takwimu za full vaccination coverage za WHO za nchi za wazungu na waarabu hadi tarehe 5 March hizi hapa:
One dose Full vaccination
Russia 3.4% 1.2%
France 5.1% 2.7%
Italy 5.9% 2.6%
Germany 5.7% 2.8%
Belgium 4.9% 2.9%
Greece 6.5% 3.4%
Spain 6.7% 2.8%
Turkey 9.1% 2.8%
Bulgaria 3.3% 0.7%
Hungary 9.7% 3.1%
United Kingdom 32%. 1.5%
Israel 54.1% 40.4%
Morocco 10.6% 1.4%
USA 16.9% 8.7%
World 2.2% 0.8%
Hizo ndizo takwimu za kweli zizoko WHO. Efficacy inayooneshwa kwenye hizo chanjo ni ya baada ya kupata full vaccination. Hiyo dose moja ya kwanza haikupi kinga yo yote bali ni ya maandalizi tu ya immune system yako. Unahitaji dose ya pili (booster) baada ya wiki nne au tatu kutegemea na aina ya chanjo. Hapo ndipo tunasema umepata full vaccination. Na badoinawezekana ukahitaji booster dose nyngine baada ya miezi sita na kila mwaka baada ya hapo.
Tukisema Efficacy ya chanjo ya AstraZeneca ni 62% maana yake ni kuwa katika watu 100 waliopata full vaccination, watu 62 kati yao watakuwa miili yao imepata kinga (immunity) ya ugonjwa huo, hao 38 waliobaki hawatapata kinga yo yote dhidi ya ugonjwa huo yaani wako sawa tu na wale ambao hawakuchanja kabisa. Hakuna cha kinga kidogo. Tatizo huwezi ukawatambua au kwa vipimo kujua katika hao 100 nani kafanikiwa mwili wake kupata kinga. Kipimo pekee ni kukutana na kirusi hicho - kama hakitakugalagaza basi wewe utajua uko kwenye kundi hilo la watu 62. Full vaccination haimaanishi full immunization. Yaani kati ya watu 100 wanaopata full vaccination ya Astrazeneca vaccine ni 62 tu ndiyo wanapata full immunization against CoV-2.
Lengo kuu la chanjo dhidi ya magonjwa ya kuambukiza ni kupata angalao 60% ya watu wawe na kinga (fully immunized) ili kupata herd immunity to cut off transmission. Kwa mwendo huu wa matokeo ya chanjo kama hii ya AstraZeneca tusahau kufikia hiyo 60% herd immunity.