Ijue Sheria ya Ardhi ya Tanzania ya mwaka 1999

Ijue Sheria ya Ardhi ya Tanzania ya mwaka 1999

sio Mali ya raisi ni Mali ya nchi ya Tz maana ata raisi anaweza fukuzwa vilevile

Ndiyo anaweza kufukuzwa kwa nguvu lkn kama mkimzidi nguvu na atakayekuja bado atakuwa ni Raisi wa JMTZ ambaye pia ardhi itakuwa ni Mali yake kama kila kitu kikibakia kama kilivyo, na pia ataweza kufukuza yoyote yule!
 
Haya ni mambo ya kisheria,usiyazungumze kikasuku. Usitafsiri sheria kikasuku,ndio maana watu wanaingia darasani miaka minne kusoma.
Wee uliyesoma inasemaje,natamani aanze na suli abaki huko huko aliko.
 
Katiba ndiyo inayompa Raisi wa JMTZ huo uwezo, unajua kwamba Mbezi beach yote kuanzia njia panda ya Kunduchi mpaka Tangi bovu lilikuwa shamba la Katani la Mgiriki, Nyerere akamnyang'anya na kupima viwanja ambavyo leo hii watu wamejenga?
Iliyomnyang'anya shamba mgiriki ni serikali, Nyerere alikuwa mtekelezaji tu!
 
Unachanganya mambo naona tuko frequency mbili tofauti, mimi naongelea Raisi wa JMTZ na sijamtaja Raisi xyz bali naongelea cheo cha Risi wa JMTZ, naona wewe uko kwingne!
Naona jamaa dish lake liko mbele kwa dada Mange Marekani...!!
 
Ardhi sio mali ya rais ila rais anamanage ardhi yote kwa niaba ya wananchi.Kwa hiyo ardhi ni ya UMMA.
 
kwa nn almashauri haziwashauri watu kuacha 150cm kila kwenye bacon kwa ajili ya uchochoro Au wanapenda kuja kubomoa baada ya watu kujenga
Uchochorowqa kazi gani wakati barabara ipo mbele yako?
Au una kikundi cha vibaka unawaandalia mazingira?
 
All land in Tanzania shall continue to be public land and remain vested in the President as trustee for and on behalf of all the citizens of Tanzania. Section 4(1) of the Land Act No 4 of 1999
Ardhi yote iliopo Tanzania itaendelea kuwa ardhi ya umma na kubaki chini ya usimamiz wa Rais kwa niaba ya wananchi wote wa Tanzania.
 
Hii mada ni nzuri sana,wanatakiwa wajitokeze wanasheria ama watu wenye taaluma ya mambo ya Ardhi waje watufafanulie vizuri
 
Wazungu watu wabaya sana. Wanawawekea mipaka alafu wanaweka mfumo wa mtu mmoja kuwa na nguvu.

Haya sasa. Akishakufukuza unaenda wapi na hapa ndo ulipozaliwa

Huo siyo mfumo wa wazungu. Mfumo wa mtu mmoja kusimamia ardhi ya jamii furani umekuwepo tangu zamani. Machifu walikuwa na kitu kilichoitwa ardhi ya chifu au mfalme (grand title). na wenyeji au raia waliokuwa chini ya mfalme walipaswa kulipa kodi kwa mfalme. hiyo ilikuwa ni uthibitisho wa kuwa raia ni wapangaji kwenye ardhi ya mfalme.
 
kwa nn almashauri haziwashauri watu kuacha 150cm kila kwenye bacon kwa ajili ya uchochoro Au wanapenda kuja kubomoa baada ya watu kujenga
Vichochoro vya kwenda wapi tena mdau wakati viwanja vikipimwa vinakuwa na barabara kwa mbele na vile vya nyuma vinakuwa na barabara yaani mtaa mmoja unaangalia mashariki na unakuwa na barabara na mtaa wa nyuma, nyumba zake zinaangalia magharibi na kunakuwa na barabara yake hivyo sidhani kama uchochoro unahitajika tena ...sana sana unatakiwa nyumba yako uhakikishe unapoijenga usimalize kiwanja chote yaani ndo hiyo 150cm unayoisema inakuwa kati ya ukuta wa nyumba na mpaka wa kiwanja ambapo unaweza ukapiga fence. Kwa mbele sasa ndio unaweza ukaacha hiyo 150cm kwa ajili ya huduma za kijamii kama nguzo ya umeme ama kujenga mtaro wa maji maana ukikimaliza kiwanja chote alafu wanajenga mtaro unakuwa usawa fence hapo ni hatari (ninavyoelewa mimi, unless kama viwanja vimepimwa kwa upimaji shirikishi ambapo tayari watu walikuwa wanaishi)
 
mm nimesema uchochoro nikimaanisha space kwajili ya hizo huduma au ikatokea moto nyumba moja pakiwa na nafasi basi ni vigumu moto kuamia nyumba za nyuma
 
mm nimesema uchochoro nikimaanisha space kwajili ya hizo huduma au ikatokea moto nyumba moja pakiwa na nafasi basi ni vigumu moto kuamia nyumba za nyuma
Okay mkuu nimekuelewa...tatizo lingine watu wanajenga nyumba bila building permit maana ukichukua permit lazima mtu apeleke ramani ya nyumba yake ambayo kimsingi na size ya kiwanja chake hivyo hata watakapoipitisha wataonyesha nyuma ibaki ngapi, mbele na pembeni hali kadhalika (of course mnashauriana)
 
Mtoa mada ametoa mada akiwa na lengo zuri tatizo wachangiaji baadhi yetu hatujaipenda mada alivyoiwasilisha lakini pia kumsaidia kurekebisha/kuweka sawa pia hilo nalo limetushinda. Ndio maana tumebaki kuponda kama ilivyo desturi yetu wabongo.
 
Wakuu naombeni msaada wenu wa sheria ya arthi kwani kuna wataalamu wengu humu wa sheria.
Ni habari refu ila nafupisha sisi watoto tulikuwa wadogo na tuliishi kijijini na familia kutokana na hali ya maisha kipindi hicho 1996 mzee alishindwana na Mama akabadilika vibaya akaanza kuleta unyayasaji kalini Mama alichofanya tuliondoka mzee akachukua hatua ya kumwachia mtu kijijini pale pale nusu ya arthi ya shamba letu bila sahihi ya ushahidi wa wanandugu lakini tetesi zilizopo mtaani ni kwamba alichukua kiasi cha pesa kwa makubaliano ya kukaa na lile eneo miaka saba na mpaka kipindi kile alifanya chochote alichopenda kwenye lile eneo aliclear kila kitu na akapanda humo majani ya ng, ombe bila shaka haikupita muda mzee alichanganikiwa akawa kama kalogwa so alikuwa hafanyi mambo kiukawaida toka kipindi chote miaka ile ilipita mpaka mzee alizidiwa na akaja akafariki 2006 kipindi cha msiba ndugu wa upande wa Mama walimwomba huyo mzee wamrudishie kiasi alichompatia arejeshe shamba kwani sisi ndio tegemeo letu pale alikubadi pale pale lakini mke wake alikataa kabisa akasema shamba halirudi kwa sasa hivi hali ndivyo ilivo na huwa anajaribu kuleta miti anapanda kama vile anaweka mipaka naombeni msaada wenu kwani amekaa na shamba sasa zaidi ya miaka 20 sasa na sisi tumekua
 
Kazi kubwa ya sheria zote zinazoshughulika na masuala ya ardhi ni kuratibu na kutoa mwongozo katika miamala mbalimbali ya masuala ya ardhi katika maisha ya kila siku. Miamala hiyo ni kama uuzaji na ununuzi wa ardhi, masuala ya mikopo na rehani, upangaji na upangishaji, masuala ya fidia, kuhamisha umiliki binafsi, umiliki wa pamoja, ujenzi , Haki ya kuitumia kama barabara au njia, haki na wajibu wa mmiliki ardhi, haki na wajibu wa serikali katika ardhi yote, upimaji na ramani, namna ya kutatua migogoro ya ardhi, n.k.

Makala yatagusa kwa mtindo wa dondoo baadhi ya mambo ya msingi yaliyo katika sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 sura ya 113.

1.SHERIA NAMBA 4 YA MWAKA 1999.

Sheria hii ilipitishwa na bunge la Jamhuri ya Muungano mwaka 1999. Hata hivyo ilianza kutumika rasmi mwezi mei mwaka 2001.

( a ) MDHAMINI WA ARDHI YOTE NI RAIS.

Sehemu ya pili ya kifungu cha 3 cha sheria hii inaanza kwa kueleza sera ya taifa ya ardhi. Kubwa linalotajwa ni kuwa ardhi yote ni mali ya umma ambayo mdhamini wake ni rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania. Huu ndio msingi mkuu wa ardhi yetu.

( b ) WASIMAMIZI WAKUU WA ARDHI.

Sehemu ya iv kifungu cha 8 mpaka 18 kinaeleza watumishi wakuu na wasimamizi wa ardhi kitaifa. Waziri wa ardhi ndiye mwenye dhamana kuu akifuatiwa na kamishna mkuu wa ardhi kabla ya kutajwa kamishna msaidizi na baadae maafisa ardhi . Wajibu, kazi na majukumu yao yameainishwa katika vifungu hivyo. Sambamba na hilo mipaka katika utekelezaji wa majukumu yao ni jambo jingine lililoainishwa.

( c ) KUMILIKI HATI.

Sehemu ya vi kifungu cha 24 mpaka 30 yameelezwa masuala ya hakimiliki. Taratibu za kupata hakimiliki na umilikishwaji . Wakati huohuo vifungu vya 31 mpaka 35 vimeeleza vyema masharti yanayoambatana na hakimiliki ,muda wa hakimiliki pamoja na kodi za ardhi.

Kifungu cha 76 mpaka 78 kimeongelea uuzaji wa ardhi hasa zenye hati miliki.

( d ) UPANGAJI NA UPANGISHAJI.

Sehemu ya ix kifungu cha 77 mpaka 93 kimeeleza kwa urefu masuala yote ya upangaji katika ardhi. Haki na wajibu wa mpangaji vimeelezwa. Pia aina ya mikataba ya upangaji imeainishwa sambamba na yale mambo ambayo yakifanyika yanaathiri upangaji.

( e ) MASUALA YA MIKOPO .

Sehemu ya x ya sheria hii ni sehemu muhimu sana. Ni sehemu inayoeleza masuala ya mikopo. Imeeleza haki na wajibu wa mkopaji halikadhalika haki za mtoa mkopo. Eneo hili zimejadiliwa rehani pia. Rehani zote yaani zile zitokanazo na hati za kimila kwa ardhi za vijijini na zile zitokanazo na hati zisizo za kimila kwa wenye ardhi mijini.

Haki za mtoa mkopo pale pesa yake inaposhindwa kurejeshwa imeelezwa. Nini afanye,kwa kutumia njia zipi na kwa wakati gani ni sehemu ya maelezo hayo. Wakadhalika hatua anazoweza kuchukua mkopwaji baada ya kushindwa kurejesha .

( f ) HAKI YA NJIA.

Kifungu cha 151 mpaka 156 kimeongelea masuala ya haki ya njia. Hii ni hasa kwa yale maeneo ambayo baadhi ya watu wamejenga kwa kuziba njia. Vifungu vimeeleza haki ya njia kama haki ya msingi katika masuala ya ardhi.

( g ) NGUVU YA MAHAKAMA.

Sehemu ya xiii kifungu cha 187 sambamba na kifungu cha 157 na 158 vimeeleza uwezo na nguvu ya mahakama katika masuala ya ardhi. Mahakama inaweza kutumika mda wowote kwa yoyote anayehisi haki haikutendeka katika ardhi yake. Mahakama ndicho chombo kikuu cha kufafanua sheria hii na kutoa mwongozo kwa pande zinazobishana
Somo zuri.
 
Wakuu naombeni msaada wenu wa sheria ya arthi kwani kuna wataalamu wengu humu wa sheria.
Ni habari refu ila nafupisha sisi watoto tulikuwa wadogo na tuliishi kijijini na familia kutokana na hali ya maisha kipindi hicho 1996 mzee alishindwana na Mama akabadilika vibaya akaanza kuleta unyayasaji kalini Mama alichofanya tuliondoka mzee akachukua hatua ya kumwachia mtu kijijini pale pale nusu ya arthi ya shamba letu bila sahihi ya ushahidi wa wanandugu lakini tetesi zilizopo mtaani ni kwamba alichukua kiasi cha pesa kwa makubaliano ya kukaa na lile eneo miaka saba na mpaka kipindi kile alifanya chochote alichopenda kwenye lile eneo aliclear kila kitu na akapanda humo majani ya ng, ombe bila shaka haikupita muda mzee alichanganikiwa akawa kama kalogwa so alikuwa hafanyi mambo kiukawaida toka kipindi chote miaka ile ilipita mpaka mzee alizidiwa na akaja akafariki 2006 kipindi cha msiba ndugu wa upande wa Mama walimwomba huyo mzee wamrudishie kiasi alichompatia arejeshe shamba kwani sisi ndio tegemeo letu pale alikubadi pale pale lakini mke wake alikataa kabisa akasema shamba halirudi kwa sasa hivi hali ndivyo ilivo na huwa anajaribu kuleta miti anapanda kama vile anaweka mipaka naombeni msaada wenu kwani amekaa na shamba sasa zaidi ya miaka 20 sasa na sisi tumekua
Hilo shamba kisheria ni lake kama hakujitoKeza mtu kudai kwa muda was miaka 12 hivyo hamna jinsi zaidi ya kuongea Na mzee kwakua alionesha kutotaka kudhulumu, ardhi ikikaliwa miaka 12 pasipo kujitokeza mdu kudai inakuwa mali ya mkaazi alie iendeleza nje ya ardhi yenye hati
 
Watu wako chini ya Raisi wa JMTZ, huu ni urithi kutoka kwa Ufalme wa Uingereza na hatukubadilisha kitu, kama vile tulivyokuwa chini wa Ufalme wakati wa Ukoloni ndivyo leo hii tulivyo kuwa chini ya Raisi wa JMTZ, na Sheria zetu hazimuhusu, hizo ni kwa ajili yetu tu!
Kumbe ndio maana anatuburuza atakavo kumbe ana mamlaka yote hayo

*A good wife is from God, but a good husband is from Kigoma*
 
Back
Top Bottom