Ijue siri na sababu za malalamiko ya Teuzi kwa hoja za Udini katika Awamu hii ya Sita

Last...
Mimi si mtu wa kubishana.
Tatizo linafahamika na viongozi wetu.

Zamani watu wakiogopa kusema kweli.
Leo mambo yote yako hadharani.

Agenda iko juu ya meza sasa ni wakati wa kusubiri.
Mzee achana na Mitandao, LEA WAJUKUU.
 
Mzee achana na Mitandao, LEA WAJUKUU.
Mkaruka,
Unapoleta mashambulizi katika maisha binafsi ni dalili kuwa umeghadhibika.

Hii inakuwa bahati mbaya kwetu sote kwako na kwangu.

Kwako kwa kukasirishwa na niliyoandika ambayo naamini sijakushambulia binafsi katika maisha yako lakini bahati mbaya nimekuchoma kwa kile nilichoandika.

Bahati mbaya kwangu kwa kuwa sikutarajia kwanza kukejeliwa kuwa sifai hapa ila nafaa katika ulezi wa wajukuu.

Pili kauli yako imenitia simanzi kwani nimeona umenitukana pasi na sababu.

Tujadiliane kwa heshima na adabu huu ukumbi ni mahali pa elimu si uwanja wa matusi.
 
Kitali,
Pengine ni namna unavyotafsiri kitabu changu.

Hapa unaweza ukanieleza kipi nilichokosea na hapana sababu ya kuhamaki.

Mimi nimeandika historia ya maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama alivyosilimu na kuwa Muislam.

Akajenga msikiti na shule na ndiyo ikawa madrasa ya kusomesha Qur'an kijijini kwake Machame Nkuu.

Sheikh Rajabu Kirama akaenda Zanzibar akawaleta walimu wanne wawili akawapeleka Upare na wawili wakawa Nkuu.

Kuanzia hapo Uislam ukaanza kuenea Uchaggani.

Kuna mengi katika historia hii kufikia Sheikh Rajabu Kirama kuwa mtu maarufu Upare na Uchaggani kote.

Yote haya yapo kitabuni kwa ushahidi wa nyaraka na picha.

Sijui nini kimekukasirisha kiasi unanita mimi mvivu nk.

Nakuwekea picha ya msikiti mpya unaojengwa mahali Mzee Rajabu Kirama alipojenga msikiti wa kwanza Machame Nkuu zaidi ya miaka 90 iliyopita.

 
Na sijawah kuona katika kusoma soma kwangu biographies mbalimbali iwe kwamba mtu anapinga maisha ya muhusika kwa mchango wake katika jamii.mleta hoja anabisha kuwa Rajab Kirama hakuyafanya hayo? Anabishia maisha binafs ya mtu na harakat zake? Nadhan kuna historia nying za watu wa kaskazini na ya Rajabu Kirama nayo mojawapo.sio kwamba mwandish amesema eti hakuna historia ya wachaga isipokuwa ya Rajab Kirama,ila na Ya Kirama katika harakat mbalimbal imo tena kwa ushahid wa nyaraka
 
Julai...
Historia yoyote nzuri ya Waislam itapingwa.

Inamchoma moyo anatamani kama Rajabu Ibrahim Kirama asingekuwapo na historia ya maisha yake isingeandikwa.

Baba yake Rajabu Kirama Muro Mboyo alimpa mmeshionari Bruno Gutman ardhi ajenge kanisa lake.

Watu hawa walikuwa marafiki wakubwa Kidia, Old Moshi na Gutman aliwabatiza Wachagga wengi ila Mboyo alimshinda hakutaka kutoka katika Upagani.

Ili kumfurahisha rafiki yake ndiyo akampa kipande cha ardhi ajenge kanisa.

Kanisa hili lipo hadi leo.
 
Mpeni salamu mama yenu kwamba 2025 tutampa salamu kwa vitendo kutoka baraza ka maaskofu Tanzania. Hapo akili itamkaa sawa...
Walisema waswahili "mkamia maji hayanywi", ulipaswa kutoa salam kwa jamaa zako mtaani kabla ya huyo ambae hata babu yako hatafikia hadhi yake "The Commander in chief", tuwe na ustaarabu wa kujizuia na hasadi za kitoto waafrika
 
Last...
Mimi si mtu wa kubishana.
Tatizo linafahamika na viongozi wetu.

Zamani watu wakiogopa kusema kweli.
Leo mambo yote yako hadharani.

Agenda iko juu ya meza sasa ni wakati wa kusubiri.

..lakini Waislamu mmezidi kuiunga mkono Ccm pamoja na kwamba haiwathamini.
 
Kwa jinsi nilivyokusoma na kukuelewa ndugu Mohamed, inaonekana harakati za kupigania uhuru wa tanganyika kwa mujibu wa waisilamu ilikuwa ni uhuru kwa ajili ya uisilamu, bahati mbaya iliyotokea ni kwamba Nyerere aliushtukia huu mchezo hivyo akautengenezea dawa ila akaifucha akasubiri uhuru upatikane ndipo akaiachia.

Nashukuru kwa elimu hii sikuwahi KUFIKIRIA hivyo.
Na kwa hali ilivyo nadhani mna haja ya kukubali yaishe kwamba Nyerere aliwadhibiti sana kwa namna ambavyo ni ngumu sana kunasuka kama jamii ya kiisilamu.

Ukifanya sensa ya vyuo vikuu vinavyomilikiwa na kanisa hapa nchini ukalinganisha na idadi ya vyuo vikuu vinavyomilikiwa na waisilamu utagundua kuna pengo kubwa sana, maana hadi sasa chuo kikuu cha waisilamu kinachofahamika sana ni mum.

Kwa mantiki hiyo ningeomba acheni kufikiri wakristo wanapendelewa fikirini kwamba waisilamu hawajaandaliwa. Waombeni wafadhili wenu wajenge vyuo vikuu Kila mkoa pia waweke hela ya kufadhili watoto wa kiisilamu wasome bure ikibidi wapewe na ruzuku juu. Ili kuwapiku wakristo Kwa idadi ya wasomi.

Jambo lingine ni namna unavyomuongelea nyerere, yaani unamzungumzia kana kwamba ni kamtu tu ambako waisilamu walikaokota wakakaweka pale Kwa huruma zao. Ukweli ni kwamba waongoza harakati za kupigania uhuru walipokutana na Nyerere waliona hawana sifa hata nusu za kumkaribia hivyo ikabidi wasalimishe harakati zote kwake.
Na kuonyesha kwamba aliwazidi parefu ni namna alivyowageuka na kuwabana vilivyo, na ndiyo maana nakumbuka miaka ya nyuma kulikuwa na makongamano ya kupinga mfumo kristo Tanzania yakiratibiwa na mum redio na tv Iman na wanazuoni wa kiisilamu walikuwa wakifikia kumtaja Nyerere basi utasikia wanasoma dua ya kumlaani.
 
Mtaje sheikh walau mmoja aliyekula zile hela za Tegeta Escrow tukutajie wachunga kondoo wenye heshima kubwa walipewa ule mgao

Au ulikuwa bado uko primary
Mkuu hongera sana kwa kuwabana hawa mashoga, waambie mwaka huu mpaka wasilimu wote au wahame inchi waende kwa mashoga wenzao
 
Big up mzee wangu, hakika kila jema litalipwa na utalikuta kwenye mizani yako, naomba kama umeweka au bado basi uweke hizi habari na nyingine kwa ajili ya vizazi vijavyo, hawa jamaa wanadanganya sana vizazi vyetu

Kama tayari nielekeze jinsi ya kupata nami nisupply au nihifadhi kwa ajili ya vizazi vijavyo
 
Pye...
Kipo kitabu cha maisha ya Abdul Sykes nimeeleza yote unayosoma hapa.
 
The...
Umeandika kinyume cha ukweli.

Historia yote kwa ukweli na ukamilifu wake iko katika kitabu cha Abdul Sykes (1989).

Kuhusu mengine uliyotaja kuhusu Nyerere kuwadhibiti Waislam soma Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002).

Utajifunza mengi.
 
Ni rahisi sana adui wa Tanzania kupitia hapo trust me.
 
Sheikh huyu mimi cjaanza nae huku
 
Hili bandiko lako mtu akilisoma akiwa na free mind atakuelewa sana. Ila sasa mtu akisoma huku tayari yuko katika kundi au fikra mojawapo ya ulizotaja basi atakupinga.

Yaani ili mama awaridhishe hao basi aendelee na utaratibu ule ule wa kuweka watatu katika 20 ndio kwao wataona sawa.
 
Kwa nyie waislamu sawa Lakin kwa wachagga wala hajulikani.
Kitali,
Nitakueleza kitu.

Kwa miaka mingi sana watu waliamini kuwa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ni historia ya Julius Nyerere.

Nilipoandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes ndipo ilipojulikana kuwa baba yake Abdul, Mzee Kleist ndiye muasisi wa African Association 1929 na Abdul Sykes kadi yake ya TANU ni No. 3 na No. 2 ni ya mdogo wake Ally na ndiye aliyesanifu kadi na kuchapa kadi 1000 kutoka mfukoni kwake.

Ally Sykes ndiye aliyemwandikia Nyerere kadi yake No. 1 kama Territorial President.

Wakajua na mengine mengi mfano kuwa mipango yote ya safari ya Nyerere UNO 1955 ilifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu ndipo kilipokuwa kituo kikuu cha mikakati.

Mkusanyaji wa fedha za safari hiyo alikuwa Iddi Faiz Mafungo kadi yake ya TANU No. 24 na ndiye alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama alichounda Kleist Sykes 1933 na Mweka Hazina wa TANU 1954.

Kwa nini historia hii haikuwa sehemu ya historia ya Nyerere na TANU?

Sababu ni kuwa Nyerere alikuwa kimya, wanahistoria pia walikuwa kimya na TANU yenyewe ilikuwa kimya.

Leo hawa wote niliowataja ni sehemu ya historia ya Tanganyika.

Rajabu Ibrahim Kirama leo ni sehemu ya historia ya Wachagga.

Shule na msikiti aliojenga Machame vyote vipo hadi leo na kizazi cha Waislam Kilimanjaro kinamfahamu na kila mwaka wanasoma khitma kubwa kumkumbuka.
 
62% hiyo umeitoa wapi?? Lini uliwahi kuulizwa dini yako? Nani alifanya sensa ya kujua Idadi ya Waislam Na Wakristo?
Wikipedia ni tovuti na hata wewe unaweza kuibadili tu.
Wikipedia ni tovuti reliable, hili liwekwe hivyo ukiweza kuwapinga kwa facts hakuna tatizo ila huwezi kuwapinga kwa blah blahs au kwa sababu za kiushabiki.
Weka facts zako ili uwakosoe kwani kuna tovuti haziwezi kuharibu credibility wanayokuwa wemeijenga kwa gharama,muda na maarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…