Ijue siri na sababu za malalamiko ya Teuzi kwa hoja za Udini katika Awamu hii ya Sita

Ijue siri na sababu za malalamiko ya Teuzi kwa hoja za Udini katika Awamu hii ya Sita

Akili hawana wanaoabudu fundi seremala na kupiga magoti kuomba sanamu lake
Mimi sijataka kwenda huko maana huwa napata shida kukashifu Imani ya mwingine na nafanya hivyo pale inapobidi.

Kuhusu watu kupiga magoti kuomba sanamu usiishie hapo tu, vipi na wale wanaokizunguka kile kijumba cheusi kule maka? Nao hawana akili?
 
Kuna Taasisi inaratibu hizo chuki .
Ndo maana unaona Dr Slaa sasa taratibu anatoka CCM kurudi Chadema kuongeza nguvu...
Dr Slaa alikuwa katibu zamani wa Taasisi husika...
Nawe ulimpinga magu kwa dini yake,naona mnajitekenya tu.
Wadini ninyi nyote hamfai
 
VIONGOZI WA NECTA TANGIA KUANZISHWA KWAKE 21/11/73
1
1973 - 1977
P. MSEKWA
MKRISTO

2
1977 – 1980
I.M KADUMA
MKRISTO

3
1980 - 1988
N. A KUHANGA
MKRISTO

4
1988 - 1992
G. R. N.MMARI (prof)
MKRISTO

5
1992 - 1999
M.L LUHANGA
MKRISTO

6
1999 – 2004
G.R.V MMARI (prof)
MKRISTO

7
2004 - 2007
E. MWAIKONDO (PROF)
MKRISTO

8
2007 - 2018
R.S MKANDALA (PROF)
MKRISTO

9
2018 – to date
W.A.L. ANANGISYE (PROF)
MKRISTO

10
SECONDARY KUTOKA (DED)
EMANUEL BARIDI
MKRISTO

11
PRIMARY KUTOKA (DED)
ESTHER THOMAS
MKRISTO

12
UALIMU NA UTAALAM KUTOKA (DED)
JOSEPH KAMILI
MKRISTO
Mmepewa ninyi sasa,shule zenu za madrasa ziongoze mpaka mia bora,isiwepo hata ya wagalatia hata moja
 
Niongea ukweli kutoka moyoni, tukiwa wadogo tulifundishwa chuki,
kuwatukana Waisilamu na Mtume wao. kuna wakati tuliambiwa kuna watu wamekamatwa kanisani walitumwa na ASAS kwenda kulipua kanisa, na mtu uliongea kwa kujiamini kabisa.

Wakati sisi tunaenda kucheza mpira siku ya jmamosi na jmapili, wenzetu walikuwa wanaenda Madrasa, Sisi tulikuwa tunasoma mafundisho kipindi maalum tu, kama ni ubatizo au kipaimara, ukimaliza unajiona unaijua Dini na umaweza kujenga hoja na mwenzako.

Baba yangu aliambiwa asilimu atajengewa nyumba, sababu alikuwa mtu mwenye ushawishi pale tunapoishi, lakini alikataa kwa kuona alipo yuko sawa, leo nimeslim bila kulazimishwa na mtu.

Naupenda Uislamu Dini ya haki, inafundisha usimtukane mtu wala kumdharau huwezi kujua kesho unaweza kumuitaji hata kama angekuwa mbaya wako, wala usimuhukumu mtu kwa rangi au Imani yake na mambo mengi.

Nikikumbuka nilikotoka wakati mwingine naishia kulia kwa uchungu.
Wewe utakuwa umejengewa nyumba maana sio kwa hao ndugu zako wa imaan wanavyopenda kuongeza idadi
 
Mimi sijataka kwenda huko maana huwa napata shida kukashifu Imani ya mwingine na nafanya hivyo pale inapobidi.

Kuhusu watu kupiga magoti kuomba sanamu usiishie hapo tu, vipi na wale wanaokizunguka kile kijumba cheusi kule maka? Nao hawana akili?
Kuzunguka 'kijumba' na kupiga goti kuliomba sanamu ulilotengeneza mwenyewe unaona kitendo kipi kinaashiria ndani ya kichwa Kuna mushkeli/tatizo!?
 
Mimi sijataka kwenda huko maana huwa napata shida kukashifu Imani ya mwingine na nafanya hivyo pale inapobidi.

Kuhusu watu kupiga magoti kuomba sanamu usiishie hapo tu, vipi na wale wanaokizunguka kile kijumba cheusi kule maka? Nao hawana akili?
Wameamrishwa na Mungu kufanya hivyo.
 
Tangu Rais Samia aingie madarakani amefanya teuzi nyingi tu na katika teuzi hizo wapo watu wamekaa standby kuangalia majina ya Kizungu (isomeke Kikristo) na Kiarabu (isomeke Kiislamu) ili waone kuwa watu wanaoendana nao kiimani "wameula" zaidi au la!

Nataka nieleze sababu za hivyo:

1. Mosi, kuna sense of entitlement.
Kwa miaka mingi sana nchini tangu Uhuru mpaka leo hii, nafasi za Utumishi wa Umma na Serikali zimekaliwa zaidi na Wakiristo kuliko Waislamu. Teuzi nyingi kuanzia Nyerere hadi leo hii Rais Samia, teuzi nyingi zinakwenda kwa Wakiristo.

Hali hii imelalamikiwa sana na Waislamu kwa miaka mingi, kuwa, hili jambo lina ukakasi. Iweje teuzi ziende kwa watu wa mrengo mmoja tu kila wakati wakati nchi hii ni yetu sote, na watu wenye vigezo wapo pande zote? Majibu ambayo watu hawa wamekuwa wakipata ni kejeli, kuwa nyie hamjasoma, kuwa nyie mnaendekeza elimu dunia lakini hoja yao hiyo imekuwa proven wrong.

Hasa ikafikia hadi Sheikh Khalifa kutoa orodha ya Waislamu wasomi mamia kwa mamia, lakini licha ya hivyo wamekuwa wakifumbiwa macho. Sasa leo, Samia licha ya bado kuendelea kuteua Wakiristo wengi zaidi lakini angalau kidooogo waislamu nao wanaonekana kwa mbali.

Hili limeshtua wale waliozoea kuona teuzi za mrengo mmoja, wanahaha, wamepandwa na ghadhabu, wanataka waendelee kuteuliwa watu wa imani yao kwa wingi uleule (over representation) kama zamani.

2. Sababu ya pili ni kuwa, Siyo kweli kuwa baadhi ya hawa wanaolalamikia udini katika teuzi hawajui kuwa Samia bado anateua Wakiristo wengi zaidi kuliko Waislamu.

Bali wanataka kumblackmail ili asije akazoea kuteuateua Waislamu. Wanampa meseji kuwa, ukijaribu kubadili status quo katika nchi hii ya kuwapa nafasi watu wa imani nyingine katika Utumishi wa Serikali kwa wingi kama sisi basi tutakusagia kunguni kwa watu wa imani yetu ili upate wakati mgumu kisiasa.

Kwa hiyo hizi kelele kimsingi ni fitina ya kumchonganisha Rais na Wakiristo ili Rais aogope kuwapa Waislamu nafasi na kwa hiyo Status quo ya Wakiristo kuendelea kudominate Utumishi wa Umma na Serikali, uendelee kama ilivyokuwa tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi leo.

3. Sababu ya tatu ni chuki tu, na ufia dini.

Islamophobia is real, kuna watu wanaamini kuwa, kwa kuwabagua watu wa dini nyingine na kuwapendelea watu wa dini yao ni kumfanyia Mungu Ibada!

Wapo watu makazini wakiona kuna wafanyakazi wanavaa hijabu, muda wa swala umefika wanaenda kuswali, au Salamu ya "Assalam Aleikum" imekuwa nyingi katika korido za ofisi wanaanza kuchukia, wanajenga hila mioyoni mwao na kibaya zaidi kuna baadhi wanakwenda mbali hadi ku collude na like minded people ili kuwaletea fitina wenzao n.k.

Enzi hizo wakati nasoma katika chuo kikuu kimoja hapa nchini, wanafunzi Waislamu waliomba chumba kimoja kilicho idle ili wafanye ibada wakazunguushwa mno, wengine wakawa wanapewa vitisho vya siri kuwa wawe makini na ajenda yao hiyo kwamba wachague chuo au dini (yaani ni kitisho cha kupigwa fitina hadi wafukuzwe chuo).

Lakini at the same time, kila siku jioni na siku za Jumamosi na Jumapili madarasa ya chuo hichohicho Wakiristo wameruhusiwa kuyatumia kusali na kuabudu. Umeona aina hii ya chuki, choyo na roho mbaya?

Ushauri wangu:
1. Watanzania tuachane na habari za kutaka upendeleo katika ajira na teuzi. Hii nchi ni yetu sote. Si vizuri kunung'unika watu wa imani nyingine pia wakipata fursa za kuhudumu katika nchi.

2. Lakini kama tunaona upendeleo wa dhahiri katika teuzi, hapo kweli tuseme na tupige kelele. Kuna wakati nchi hii Rais mmoja aliunda Baraza la Mawaziri la watu zaidi ya 20 akaweka Waislamu watatu. Sasa katika situation kama hiyo kweli hapo jamii nzima haipaswi kukaa kimya.

Hivyo hivyo leo hii Samia akiunda Baraza la Mawaziri akaweka Wakiristo watatu tu hata mimi sitokaa kimya. Tusiwe na double standard, kwamba teuzi zikifavour watu wetu tunanyuti, ila wengine wakianza kuchomoza basi tunakuja hapa JF kuanzisha nyuzi lukuki za udini. Hiyo siyo fair.

3. Tuzidi kuimarisha, Umoja, Amani na Mshikamano. Nchi hii Wakiristo are here to stay, Waislamu are here to stay. Yesu hakuoni mfuasi wake bora kwa kuwa mbaguzi na wala Mtume Muhammad hakuoni mfuasi wake bora kwa kuvunja amana za watu wote. Tupendeane mazuri.

Nawasilisha.
Bora ungelinganisha teuzi wapwani na wabara. Wapwani bado elimu hawajachangamkia. Huku mikoa ya pwani mtwara, lindi, pwani na tanga, ndio wenyeji karibu wote au wengi waislaam. Huko bara japo bado waislaam elimu hawajaichangamkia vya kutosha tofauti imepungua sana. Kuna sehemu kama mkoa wa kilimanjaro huwezi kusema kwa sasa eti wakristo wamesoma zaidi. Kwa mfamo jamii ya wapare mwanga na same wote wamechangamkia elimu wala hii dhana haipo. Wilaya nyingine kilimanjaro yenye waislamu wengi ni hai. Hawa jamaa wako tu vizuri. Kwa ufupi huku bara hakuna hiyo kitu ya kusema eti waislamu hawajasoma.
Tatizo linakuja muislamu wa pwani akipata nafasi kubwa kwa kisingizio kupromote waislamu anaweka udini na kuweka jamaa zake watu mabogus kwenye vyeo. Tuliona nssf awamu ya jk jinsi walijazana waswahili na kuendeleza udini mkali hadi kutenga vyumba vya kusali kazini.
Mambo ya kushindana wakristo wangapi, waislaam wangapi historia inaonesha kila akitokea rais muislaam ndio linazuka. Lakini kwa hakika rais mkristo mkapa ndio alimaliza tatizo. Kipindi chake waislamu wasomi wengi waliwekwa sehemu za uongozi kwenye utumishi wa umma kuliko kipindi chochote. Lakini alipoingia jk tukaona malalamiko kichinichini ila yeye haku entertain hilo swali alijali uwezo na utendaji. Alipoingia samia tumeona mtu akiorodhesha idadi ya wakurugenzi wakristo na waislaam eti mama arekebishe wakristo ni wengi. Akili za hivi hazina tija na havitatupeleka popote ila kupanda mbegu mbaya tu.
Nchini kwetu hatujagawanyika kidini tu kuna mikoa na kuna makabila. Kwa nini mtu aone dini tu kama sio anatafuta pa kupenyea. Hivi wasukuma na wanyamwezi wakisema wanabaguliwa nafasi za uongozi tutasemaje. Maana wao kwa pamoja ni theluthi moja ya watanzania. Kuna kabila zingine kwenye uongozi pengine hawajawahi kua na mtu yoyote maarufu.
 
Mleta mada ameleta vizuri. Mbona sisi jumamosi hatufanyi kazi. Nawapongeza ndugu zetu nao wa ijumaa. Hii ndio real battle, kwa maana unatakiwa ufanye ibada katika wakati ambao unahitajika kwa kazi za watu au kibinafsi sio kama jumapili imepoa sana yaani huna changamoto.

Ijumaa naivulia kofia maana muda wa ibada ndio unakuta kikao kimekolea.
Missile of a nationn andiko kali

Nafuu wavaa kobazi kuliko nyie wa Jmosi.
Shida kubwa ya wa Jmosi ni unafiki tuuu
 
Sawa kabisa. Sio kwa sababu Amos "Sakalla" ni mchizi wake JK na mtoto wa mjini, wanakaa wote kwenye club wakinywa mivinyo na kutengeneza madili basi anazawadiwa tu u_RC Dsm.
Nani alikudanganya Kikwete anakunywa mvinyo?
 
Listen, hata hiki ulichoandika hapa kwangu ni muendelezo wa fikra duni, ujinga; sioni kama taifa tunaweza vipi kupiga hatua kimaendeleo ikiwa bado tutakuwa tunatazamana kwa jicho la dini, kabila, au rangi.

Wewe umekuja hapa kuwatetea wale wa dini yako, simply umekuja kuongeza tatizo, hukumbuki wapo wasio na dini, wakina Kiranga na wenzake wao wamenyamaza kimya, hawana msemaji wao, na wala hawana hivi viherehere mlivyonavyo wengine.

We need to stop this kind of ignorance, kwasababu kutaka watu wa dini yako wawepo kwenye mamlaka hakutakusaidia chochote kama hutakuwa na mahusiano nao ya moja kwa moja, zaidi, kinachowafanya wengi wazungumzie hii issue ni kama ulevi tu, usio na tija kwao wala kwa taifa.

Huu upuuzi una extend mpaka pale anapokuwepo kiongozi fulani, halafu wale wa dini yake wanakuwa hawaoni baya lolote toka kwake, huu nao ni ujinga mwingine mkubwa zaidi, kusifia/tetea kila linalofanywa na yule wa dini yako upuuzi.
Nadhani kwa uelewa wangu, suala la dini kwenye uteuzi lisitugawe, ila, nasema tena ila, tuwe waangalifu sana kwa ndugu zetu hawa , nasema ndugu zetu hawa’ sababu ya kurudia hivyo ni kama wanakitu fulani hivi mioyoni kwao kuhusu hiki wanachokifanya,

Nimesema hapo ndugu zetu hawa kwa kurudia sababu kubwa ni kwamba hata kwenye mafundisho Yao huwa wanasema kama wewe sio muislam basi sio ndugu yao,

Na mifano ni mingi, hata kwenye uongozi wa juu kama ni mwislam hata Ako see Huns haki ya kukosoa na ukikosoa utashambuliwa vibaya sana.

Yote kwa yote sioni ubaya wa kuchagua mtu wa dini yoyote mradi snags ya kazi yake vizuri na Ana vigezo vya kutosha,

NB. Kuna huu Maemo wa kusema sasa ni zangu yetu, huu ni Maemo wa kutoa hasira sana watu.
 
Suluhisho ni serikali za majimbo, watu watapunguza kujikita kutolea macho na udenda nafasi za kuteuliwa na Rais.
Tangu Rais Samia aingie madarakani amefanya teuzi nyingi tu na katika teuzi hizo wapo watu wamekaa standby kuangalia majina ya Kizungu (isomeke Kikristo) na Kiarabu (isomeke Kiislamu) ili waone kuwa watu wanaoendana nao kiimani "wameula" zaidi au la!

Nataka nieleze sababu za hivyo:

1. Mosi, kuna sense of entitlement.
Kwa miaka mingi sana nchini tangu Uhuru mpaka leo hii, nafasi za Utumishi wa Umma na Serikali zimekaliwa zaidi na Wakiristo kuliko Waislamu. Teuzi nyingi kuanzia Nyerere hadi leo hii Rais Samia, teuzi nyingi zinakwenda kwa Wakiristo.

Hali hii imelalamikiwa sana na Waislamu kwa miaka mingi, kuwa, hili jambo lina ukakasi. Iweje teuzi ziende kwa watu wa mrengo mmoja tu kila wakati wakati nchi hii ni yetu sote, na watu wenye vigezo wapo pande zote? Majibu ambayo watu hawa wamekuwa wakipata ni kejeli, kuwa nyie hamjasoma, kuwa nyie mnaendekeza elimu dunia lakini hoja yao hiyo imekuwa proven wrong.

Hasa ikafikia hadi Sheikh Khalifa kutoa orodha ya Waislamu wasomi mamia kwa mamia, lakini licha ya hivyo wamekuwa wakifumbiwa macho. Sasa leo, Samia licha ya bado kuendelea kuteua Wakiristo wengi zaidi lakini angalau kidooogo waislamu nao wanaonekana kwa mbali.

Hili limeshtua wale waliozoea kuona teuzi za mrengo mmoja, wanahaha, wamepandwa na ghadhabu, wanataka waendelee kuteuliwa watu wa imani yao kwa wingi uleule (over representation) kama zamani.

2. Sababu ya pili ni kuwa, Siyo kweli kuwa baadhi ya hawa wanaolalamikia udini katika teuzi hawajui kuwa Samia bado anateua Wakiristo wengi zaidi kuliko Waislamu.

Bali wanataka kumblackmail ili asije akazoea kuteuateua Waislamu. Wanampa meseji kuwa, ukijaribu kubadili status quo katika nchi hii ya kuwapa nafasi watu wa imani nyingine katika Utumishi wa Serikali kwa wingi kama sisi basi tutakusagia kunguni kwa watu wa imani yetu ili upate wakati mgumu kisiasa.

Kwa hiyo hizi kelele kimsingi ni fitina ya kumchonganisha Rais na Wakiristo ili Rais aogope kuwapa Waislamu nafasi na kwa hiyo Status quo ya Wakiristo kuendelea kudominate Utumishi wa Umma na Serikali, uendelee kama ilivyokuwa tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi leo.

3. Sababu ya tatu ni chuki tu, na ufia dini.

Islamophobia is real, kuna watu wanaamini kuwa, kwa kuwabagua watu wa dini nyingine na kuwapendelea watu wa dini yao ni kumfanyia Mungu Ibada!

Wapo watu makazini wakiona kuna wafanyakazi wanavaa hijabu, muda wa swala umefika wanaenda kuswali, au Salamu ya "Assalam Aleikum" imekuwa nyingi katika korido za ofisi wanaanza kuchukia, wanajenga hila mioyoni mwao na kibaya zaidi kuna baadhi wanakwenda mbali hadi ku collude na like minded people ili kuwaletea fitina wenzao n.k.

Enzi hizo wakati nasoma katika chuo kikuu kimoja hapa nchini, wanafunzi Waislamu waliomba chumba kimoja kilicho idle ili wafanye ibada wakazunguushwa mno, wengine wakawa wanapewa vitisho vya siri kuwa wawe makini na ajenda yao hiyo kwamba wachague chuo au dini (yaani ni kitisho cha kupigwa fitina hadi wafukuzwe chuo).

Lakini at the same time, kila siku jioni na siku za Jumamosi na Jumapili madarasa ya chuo hichohicho Wakiristo wameruhusiwa kuyatumia kusali na kuabudu. Umeona aina hii ya chuki, choyo na roho mbaya?

Ushauri wangu:
1. Watanzania tuachane na habari za kutaka upendeleo katika ajira na teuzi. Hii nchi ni yetu sote. Si vizuri kunung'unika watu wa imani nyingine pia wakipata fursa za kuhudumu katika nchi.

2. Lakini kama tunaona upendeleo wa dhahiri katika teuzi, hapo kweli tuseme na tupige kelele. Kuna wakati nchi hii Rais mmoja aliunda Baraza la Mawaziri la watu zaidi ya 20 akaweka Waislamu watatu. Sasa katika situation kama hiyo kweli hapo jamii nzima haipaswi kukaa kimya.

Hivyo hivyo leo hii Samia akiunda Baraza la Mawaziri akaweka Wakiristo watatu tu hata mimi sitokaa kimya. Tusiwe na double standard, kwamba teuzi zikifavour watu wetu tunanyuti, ila wengine wakianza kuchomoza basi tunakuja hapa JF kuanzisha nyuzi lukuki za udini. Hiyo siyo fair.

3. Tuzidi kuimarisha, Umoja, Amani na Mshikamano. Nchi hii Wakiristo are here to stay, Waislamu are here to stay. Yesu hakuoni mfuasi wake bora kwa kuwa mbaguzi na wala Mtume Muhammad hakuoni mfuasi wake bora kwa kuvunja amana za watu wote. Tupendeane mazuri.

Nawasilisha.
 
Takwimu gani rasmi zinasema kuwa huku Tanganyika Wakiristo ni wengi zaidi?
Hii iko obvious, umejitahidi kuandika topic yako in a sensible way hapa tena unakuja kuuliza swali la kijinga kabisa. Labda topic yako ilikuwa na hidden agenda ndani yake, fanya utafiti usio rasmi wa kujua idadi ya watu maeneo yote ya nchi na asilimia za watu wa dini zenu hizi mnazopigia kelele(Christians and Muslims) kiurahisi sana utapata majibu.
 
Serikali za majimbo zitapunguza au kumaliza kabisa huu ukakasi.
Mimi ni mkristu lakini katika suala la uteuzi au hata kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali katika Idara zote za Serikali yetu lazima kuwepo UWIANO kwa kuzingatia sifa na uzoefu.

kwa kufanya hivyo itasaidia sana kujenga UMOJA na MSHIKAMANO ktk kuijenga nchi yetu.

nakubaliana na mtoa hoja kuwa ni kweli sisi wakristu tulikuwa tumeshika nafasi nyingi ktk Idara za Serikali tangu nchi ipate uhuru na hilo linatokana na sababu za kihistoria,

Ila kwa zama hizi hakuna sababu ya kushindwa kuweka UWIANO.
Kujaza watu wa aina moja ni hatari.

Ni kweli nchi hii ni yetu sote na itajengwa na waislam, wakristu na wasio na dini.
 
Zanzibar haiwezi kuwa sawa na Tanganyika.
Mkuu kwa Dunia. ya sasa jambo hilo japo sio Sheria lkn lazima lizingatiwe, ni kama ilivyo ktk suala la Uongozi wa juu kwamba miaka 10 Rais anatoka Bara miaka kumi mingine lazima atoke znz, hakuna Sheria inayo lazimisha hilo lkn ni jambo muhimu ktk kuimarisha muungano wetu, vivohivyo katika teuzi zingine mbalimbali UWIANO wa dini zote ni muhimu katika kujenga umoja wa nchi yetu.
Pongezi kwa Rais Samia anajitahidi sana kubalance.
 
Hii iko obvious, umejitahidi kuandika topic yako in a sensible way hapa tena unakuja kuuliza swali la kijinga kabisa. Labda topic yako ilikuwa na hidden agenda ndani yake, fanya utafiti usio rasmi wa kujua idadi ya watu maeneo yote ya nchi na asilimia za watu wa dini zenu hizi mnazopigia kelele(Christians and Muslims) kiurahisi sana utapata majibu.
Nimeuliza swali ili kupata data sahihi kutokana na mchango wa member aliouweka. Sisi wengi tunapenda sana data ili kuelewa demography ya nchi.
Mimi ninachojua Waislamu waliomba kipengele cha dini kiwekwe ktk sensa, serikali na viongozi wa dini ya kikristo wakakataa..Sasa leo mtu akisema wakiristo ni wengi kuliko waislamu au waislamu ni wengi kuliko wakiristo, tunajiuliza hizo data kazipata wapi?
 
Back
Top Bottom