Ijue siri na sababu za malalamiko ya Teuzi kwa hoja za Udini katika Awamu hii ya Sita

Ijue siri na sababu za malalamiko ya Teuzi kwa hoja za Udini katika Awamu hii ya Sita

Ipo siku watu wataelewa vizuri
ndiyo sababu chadema wanapigania serikali za majimbo. Nafasi za kisiasa watu wachaguliwe na wananchi na teuzi zote za watendaji ziombwe kama ajira ya mkataba. Siyo kuwaachia kundi la watu wanakaa club na konyagi eti wanafanya vetting wanawapa watu wao.

Keki za taifa zinatakiwa kugombaniwa na kila mtu kwa uwazi kabisa
 
Kanisa gani hilo lilikofundisha kuchukia Waislamu?
Huu ndo ukweli mi nimesoma nursery kanisani najua jinsi wanavyofundishwa kuchukua waislamu ... Alhamdulliah Leo mm ni muislamu hakuna kitu sikijui kutoka kwa hao watu Wana chuki sana
 
Nani aliwafundisha hiyo chuki?
Niongea ukweli kutoka moyoni, tukiwa wadogo tulifundishwa chuki,
kuwatukana Waisilamu na Mtume wao. kuna wakati tuliambiwa kuna watu wamekamatwa kanisani walitumwa na ASAS kwenda kulipua kanisa, na mtu uliongea kwa kujiamini kabisa.

Wakati sisi tunaenda kucheza mpira siku ya jmamosi na jmapili, wenzetu walikuwa wanaenda Madrasa, Sisi tulikuwa tunasoma mafundisho kipindi maalum tu, kama ni ubatizo au kipaimara, ukimaliza unajiona unaijua Dini na umaweza kujenga hoja na mwenzako.

Baba yangu aliambiwa asilimu atajengewa nyumba, sababu alikuwa mtu mwenye ushawishi pale tunapoishi, lakini alikataa kwa kuona alipo yuko sawa, leo nimeslim bila kulazimishwa na mtu.

Naupenda Uislamu Dini ya haki, inafundisha usimtukane mtu wala kumdharau huwezi kujua kesho unaweza kumuitaji hata kama angekuwa mbaya wako, wala usimuhukumu mtu kwa rangi au Imani yake na mambo mengi.

Nikikumbuka nilikotoka wakati mwingine naishia kulia kwa uchungu.
 
Sahihi kabisa
Muhimu ni suala la kuteua watu wengi halina afya sana twende na katiba mpya nafasi zipunguzwe na uteuzi ukome watu waombe kazi kutokana na kusugua kitabu.

Hivi vyeo vya kupeana vipungue mtu kama mwesiga akateuliwa DG wa Tpdc mara akatenguliwa hivi yuko wapi chawa mwesiga alikuwa ana kiherehere mambo ya ccm naona toka ile issue kazama kusikojulikana.
 
Kusalimiana:
-Salaam alleikum
-Bwana asifiwe
-Tumsifu Yesu Kristo
Maofisini na maeneo yote ya kazi kwa ujumla wake hakuna tofauti na kuongea lugha za makabila ya kwenu maofisini mnapokutana watu wa kabila moja, kwa kifupi ni udini.
 
Tunahitaji serikali za majimbo.
naona tunarudi kulekule awamu ya nne ya JK alivyoyumbishwa na jamaa fulani mpaka kufikia hatua ya kuitwa dhaifu..

Muda si mrefu tutaanza kusikia na matamko kutoka kila kona...

Hii nchi ipo siku itaingia kwenye mgogoro mkubwa sana wa kidini, chanzo cha mgogoro ni dini fulani kuamini yenyewe ndio kila kitu..
 
Sahihi kabisa
Kusalimiana:
-Salaam alleikum
-Bwana asifiwe
-Tumsifu Yesu Kristo
Maofisini na maeneo yote ya kazi kwa ujumla wake hakuna tofauti na kuongea lugha za makabila ya kwenu maofisini mnapokutana watu wa kabila moja, kwa kifupi ni udini.
 
Nimeuliza swali ili kupata data sahihi kutokana na mchango wa member aliouweka. Sisi wengi tunapenda sana data ili kuelewa demography ya nchi.
Mimi ninachojua Waislamu waliomba kipengele cha dini kiwekwe ktk sensa, serikali na viongozi wa dini ya kikristo wakakataa..Sasa leo mtu akisema wakiristo ni wengi kuliko waislamu au waislamu ni wengi kuliko wakiristo, tunajiuliza hizo data kazipata wapi?
Mkuu angalia mikoa ambayo majority ni wakristo au angalau wanamajina ya kikristo(sababu wote mnaweka kundi la wakristo) ni mingi na ina idadi kubwa ya watu mfano kanda ya ziwa katika watu kumi utakao kutana nao muislamu ni mmoja na hapo ni mjini, vijijini ndio kabsa na ina theluthi ya watu wote tz. Ila kwa mikoa yenye waislamu wengi ina idadi ndogo ya watu mfano hiyo mikoa ya pwani ambayo majority ni waislamu.
 
Wa kulaumiwa ni Nyerere ambaye alileta muungano wa kipuuzi akitarajia Zanzibar na Wazanzibari kwa ujumla watatawaliwa na Mtanganyika miaka yote kwa maana lazima Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania atatoka Tanganyika lakini leo tumepigwa na kitu kizito kichwani tunalalamika.
Ilikuwaje wakasema mgombea urais akitoka bara basa makamu atoke Zanzibar. Hapa ndo palitumaliza kabisa. Ndo haya leo Rais kafa, then makamu ndo rais.Wangekuwa na akili wangesema makamu awe rais kwa miezi mitatu then uchaguzi mkuu ufanyike.
 
Tatizo hawa wavaa makubanzi hawaaminiki kabisa wakipata nafasi mbona mtaona chamoto sio rungu huko mitaani wanasema maadili. Mara hakuna kula mwezi mzima sijui wanauita mwezi nani yani ni balaaa.Mara watu wamwagiwe tindikali.
Asee hawa jamaa ni kuwasigia kunguni tu sio waugwana kabisa wakatili mno.
 
Mkuu angalia mikoa ambayo majority ni wakristo au angalau wanamajina ya kikristo(sababu wote mnaweka kundi la wakristo) ni mingi na ina idadi kubwa ya watu mfano kanda ya ziwa katika watu kumi muislamu ni mmoja na hapo ni mjini, vijijini ndio kabsa na ina theluthi ya watu wote tz. Ila kwa mikoa yenye waislamu wengi ina idadi ndogo ya watu mfano hiyo mikoa ya pwani ambayo majority ni waislamu.
Mimi ninachojua ni kwamba sensa ya mkoloni ya mwaka 1957 iliyokuwa na kipengele cha dini Waislamu nchini Tanganyika walikuwa wengi zaidi wakifuatiwa na Wapagani.
Tena mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa ndo ilikuwa na wapagani wengi zaidi.
 
Mimi ninachojua ni kwamba sensa ya mkoloni ya mwaka 1957 iliyokuwa na kipengele cha dini Waislamu nchini Tanganyika walikuwa wengi zaidi wakifuatiwa na Wapagani.
Tena mikoa hiyo ya Kanda ya Ziwa ndo ilikuwa na wapagani wengi zaidi.
Uko sahihi kabisa lakini kwa sasa wakristo hiyo kanda ni wengi.
 
Tangu Rais Samia aingie madarakani amefanya teuzi nyingi tu na katika teuzi hizo wapo watu wamekaa standby kuangalia majina ya Kizungu (isomeke Kikristo) na Kiarabu (isomeke Kiislamu) ili waone kuwa watu wanaoendana nao kiimani "wameula" zaidi au la!

Nataka nieleze sababu za hivyo:

1. Mosi, kuna sense of entitlement.
Kwa miaka mingi sana nchini tangu Uhuru mpaka leo hii, nafasi za Utumishi wa Umma na Serikali zimekaliwa zaidi na Wakiristo kuliko Waislamu. Teuzi nyingi kuanzia Nyerere hadi leo hii Rais Samia, teuzi nyingi zinakwenda kwa Wakiristo.

Hali hii imelalamikiwa sana na Waislamu kwa miaka mingi, kuwa, hili jambo lina ukakasi. Iweje teuzi ziende kwa watu wa mrengo mmoja tu kila wakati wakati nchi hii ni yetu sote, na watu wenye vigezo wapo pande zote? Majibu ambayo watu hawa wamekuwa wakipata ni kejeli, kuwa nyie hamjasoma, kuwa nyie mnaendekeza elimu dunia lakini hoja yao hiyo imekuwa proven wrong.

Hasa ikafikia hadi Sheikh Khalifa kutoa orodha ya Waislamu wasomi mamia kwa mamia, lakini licha ya hivyo wamekuwa wakifumbiwa macho. Sasa leo, Samia licha ya bado kuendelea kuteua Wakiristo wengi zaidi lakini angalau kidooogo waislamu nao wanaonekana kwa mbali.

Hili limeshtua wale waliozoea kuona teuzi za mrengo mmoja, wanahaha, wamepandwa na ghadhabu, wanataka waendelee kuteuliwa watu wa imani yao kwa wingi uleule (over representation) kama zamani.

2. Sababu ya pili ni kuwa, Siyo kweli kuwa baadhi ya hawa wanaolalamikia udini katika teuzi hawajui kuwa Samia bado anateua Wakiristo wengi zaidi kuliko Waislamu.

Bali wanataka kumblackmail ili asije akazoea kuteuateua Waislamu. Wanampa meseji kuwa, ukijaribu kubadili status quo katika nchi hii ya kuwapa nafasi watu wa imani nyingine katika Utumishi wa Serikali kwa wingi kama sisi basi tutakusagia kunguni kwa watu wa imani yetu ili upate wakati mgumu kisiasa.

Kwa hiyo hizi kelele kimsingi ni fitina ya kumchonganisha Rais na Wakiristo ili Rais aogope kuwapa Waislamu nafasi na kwa hiyo Status quo ya Wakiristo kuendelea kudominate Utumishi wa Umma na Serikali, uendelee kama ilivyokuwa tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi leo.

3. Sababu ya tatu ni chuki tu, na ufia dini.

Islamophobia is real, kuna watu wanaamini kuwa, kwa kuwabagua watu wa dini nyingine na kuwapendelea watu wa dini yao ni kumfanyia Mungu Ibada!

Wapo watu makazini wakiona kuna wafanyakazi wanavaa hijabu, muda wa swala umefika wanaenda kuswali, au Salamu ya "Assalam Aleikum" imekuwa nyingi katika korido za ofisi wanaanza kuchukia, wanajenga hila mioyoni mwao na kibaya zaidi kuna baadhi wanakwenda mbali hadi ku collude na like minded people ili kuwaletea fitina wenzao n.k.

Enzi hizo wakati nasoma katika chuo kikuu kimoja hapa nchini, wanafunzi Waislamu waliomba chumba kimoja kilicho idle ili wafanye ibada wakazunguushwa mno, wengine wakawa wanapewa vitisho vya siri kuwa wawe makini na ajenda yao hiyo kwamba wachague chuo au dini (yaani ni kitisho cha kupigwa fitina hadi wafukuzwe chuo).

Lakini at the same time, kila siku jioni na siku za Jumamosi na Jumapili madarasa ya chuo hichohicho Wakiristo wameruhusiwa kuyatumia kusali na kuabudu. Umeona aina hii ya chuki, choyo na roho mbaya?

Ushauri wangu:
1. Watanzania tuachane na habari za kutaka upendeleo katika ajira na teuzi. Hii nchi ni yetu sote. Si vizuri kunung'unika watu wa imani nyingine pia wakipata fursa za kuhudumu katika nchi.

2. Lakini kama tunaona upendeleo wa dhahiri katika teuzi, hapo kweli tuseme na tupige kelele. Kuna wakati nchi hii Rais mmoja aliunda Baraza la Mawaziri la watu zaidi ya 20 akaweka Waislamu watatu. Sasa katika situation kama hiyo kweli hapo jamii nzima haipaswi kukaa kimya.

Hivyo hivyo leo hii Samia akiunda Baraza la Mawaziri akaweka Wakiristo watatu tu hata mimi sitokaa kimya. Tusiwe na double standard, kwamba teuzi zikifavour watu wetu tunanyuti, ila wengine wakianza kuchomoza basi tunakuja hapa JF kuanzisha nyuzi lukuki za udini. Hiyo siyo fair.

3. Tuzidi kuimarisha, Umoja, Amani na Mshikamano. Nchi hii Wakiristo are here to stay, Waislamu are here to stay. Yesu hakuoni mfuasi wake bora kwa kuwa mbaguzi na wala Mtume Muhammad hakuoni mfuasi wake bora kwa kuvunja amana za watu wote. Tupendeane mazuri.

Nawasilisha.
Kiongozi kumbuka hii nchi haina hizo dini mbili tu.
 
Haya mambo ni legacy ya Wakoloni yasitufanye tuchukiane, tujenge Taifa jipya ambala halitakuwa na UBAGUZI wa aina yoyote ile kupitia Katiba mpya.
 
Sasa Christians ni 62% Ukiona sehemu kuna 50 50 by default huo unaitwa udini
 
Sasa Christians ni 62% Ukiona sehemu kuna 50 50 by default huo unaitwa udini
62% hiyo umeitoa wapi?? Lini uliwahi kuulizwa dini yako? Nani alifanya sensa ya kujua Idadi ya Waislam Na Wakristo?
Wikipedia ni tovuti na hata wewe unaweza kuibadili tu.
 
Back
Top Bottom