Wahenga walisema,Mdharau mwiba umchoma,ilianza mzaa mzaa akakaa kimya,marehemu akatukanwa nchi nzima akakaa kimya,Pengine ilikuwa turufu yake Mwenyekiti,licha ya kwamba yapaswa kuheshimu "privacy" ya familia iliyopatwa na msiba,na pia kutetea heshima ya nchi kwa Marehemu aliyewahi kuwa Kiongozi wa nchi,
Mambo yakahania kwenye dini,akakataa kusalimia Wakristo kwa salamu ya Bwana Yesu asifiwe,au tumsifi Yesu kristo,mtangulizi wake haikuwa shida kwake alisalimia Assalamualaikum,Bwana Yesu asifiwe,Tumsifu Yesu Kristy,akaongezea na salamu za kabila zaidi ya ishirini alianza na amsindile,Subhai takwenya,na makabila mengine thelathini,
Athari yake tumeanza kuiona sasa udini umeingia,mkataba mbovu wa bandari unatetewa na Waislamu na kupingwa na Wakristu,hii ni "nightmare" ambayo hatutaki itokee katika maisha ya Watanzania,lakini yupo aliyekaa kimya matokeo yake bomu linalipuka,
Nini kifanyike,aingie kanisani na kusali nao hao aliokataa kuwasalimia Bwana Yesu asifiwe na Tumsifu Yesu kristo,aingie msikiti asali nao hao na kuwasalimia assalamualaikum,halafu aende bungeni akasalimie Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.