mwanafyale
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 1,641
- 538
UPDATES: Kijana Aliyejiua Mwanza Alikuwa na Pesa, Alizidiwa na Stress*
Na Blogu ya Jamii, Mwanza
Saa chache baada ya kijana aliyejiua Mwanza, marafiki wa karibu wameshangazwa na polisi Mwanza kushindwa kufuatilia ukweli wa sababu za kijana aliyejiua katika jengo la Rock City Mall na kutaja tu masuala ya ajira.
Sasa ukweli kamili umeanza kujitokeza baada ya marafiki wa karibu kumueleza marehemu kama mtu ambaye chuoni hakuwa na mambo ya mabinti.
"Ila mwaka wa mwisho akawa na mpenzi, akazama sana katika mapenzi," ameeleza rafiki yake mmoja akihofia kutaja jina asihusishwe na masuala ya upelelezi.
Kama miezi miwili iliyopita inaelezwa baada ya marehemu kupata dili flani kikazi na kusafiri kwa muda, aliporejea alipata sms kutoka kwa mpenzi wake kuwa ameshaolewa na wasijuane tena.
"Kusema ajira ni kuzuga tu, jamaa alichanganyikiwa na hilo penzi lake la kwanza na tangu aambiwe kaachwa kila kazi anayofanya akipata hela analewa sana sana.Tulimuonya hakuelewa," aliongeza rafiki huyo akishauri ni vyema kwa sasa taasisi mbalimbali zikaweka vitengo vya ushauri wa mahusiano, vijana wengi mahusiano yanawamaliza.
"Pale alipolazwa polisi akionekana mlevi tu kwanza alikuwa na hela anakazi zake mwenyewe alikuwa anapata kuendesha maisha yake, kwa hiyo issue sio ajira, lakini polisi wangekuwa na washauri wa kisaikolojia huyu kijana wangemsikiliza na kumweka kwenye tiba maalum na kumwokoa na yaliyokuja kumkuta, jamii pana ina wajibu wa kufanya," aliongeza mmoja wa marafiki zake wakiwa na huzuni eneo la Furahisha.
__Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe_