Tetesi: Ijue siri ya muhitimu wa UDSM kujiua.

Tetesi: Ijue siri ya muhitimu wa UDSM kujiua.

Nilichomwelewa mtoa habari ni kuwa Polisi wanahitaji kuwa na vitengo vya saikolojia ili kutambua matatizo ambayo yanahitaji msaada wa kisaikolojia badala ya kuwaweka lock up na kuwaachia bila ushauri.
 
Muacheni ajiuwe bwana kwan ana nn cha maana
Akapambane na Sir God huko
 
UPDATES: Kijana Aliyejiua Mwanza Alikuwa na Pesa, Alizidiwa na Stress*

Na Blogu ya Jamii, Mwanza

Saa chache baada ya kijana aliyejiua Mwanza, marafiki wa karibu wameshangazwa na polisi Mwanza kushindwa kufuatilia ukweli wa sababu za kijana aliyejiua katika jengo la Rock City Mall na kutaja tu masuala ya ajira.

Sasa ukweli kamili umeanza kujitokeza baada ya marafiki wa karibu kumueleza marehemu kama mtu ambaye chuoni hakuwa na mambo ya mabinti.

"Ila mwaka wa mwisho akawa na mpenzi, akazama sana katika mapenzi," ameeleza rafiki yake mmoja akihofia kutaja jina asihusishwe na masuala ya upelelezi.

Kama miezi miwili iliyopita inaelezwa baada ya marehemu kupata dili flani kikazi na kusafiri kwa muda, aliporejea alipata sms kutoka kwa mpenzi wake kuwa ameshaolewa na wasijuane tena.

"Kusema ajira ni kuzuga tu, jamaa alichanganyikiwa na hilo penzi lake la kwanza na tangu aambiwe kaachwa kila kazi anayofanya akipata hela analewa sana sana.Tulimuonya hakuelewa," aliongeza rafiki huyo akishauri ni vyema kwa sasa taasisi mbalimbali zikaweka vitengo vya ushauri wa mahusiano, vijana wengi mahusiano yanawamaliza.

"Pale alipolazwa polisi akionekana mlevi tu kwanza alikuwa na hela anakazi zake mwenyewe alikuwa anapata kuendesha maisha yake, kwa hiyo issue sio ajira, lakini polisi wangekuwa na washauri wa kisaikolojia huyu kijana wangemsikiliza na kumweka kwenye tiba maalum na kumwokoa na yaliyokuja kumkuta, jamii pana ina wajibu wa kufanya," aliongeza mmoja wa marafiki zake wakiwa na huzuni eneo la Furahisha.

__Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe_
Kwani kama tatizo lilikuwa ni kutokuwa na ajira kuna tatizo? Inaonekana kana kwamba ilivyojulikana kuwa ni tatizo la ajira inawatisha? Hahaaaa, eti marafiki zake!!! Ambao hata majina yao hayapo!!? Umetumia nguvu nyingi kukanusha kana kwamba kuna kitu kina ogopwa?! Ukweli utabaki pale pale tu
 
Mimi siungi mkono kuwa amejiua sababu ya maisha magumu, pia sikuungi mkono wewe unaposema wabongo uwezo watu wa kufikiri ni mdogo, wewe husikiagi mtu ameacha ujumbe kuwa kajiua sababu ya kitu fulani? Au wewe ulitaka wote waliojiua sababu ya mapenzi nao wangekutana thelathini na kujiua pamoja ndo uamini, maisha ni magumu kwa mtu na mtu,kwani huko nyuma hatukuwa na watu waliojiua sababu ya maisha?tatizo langu kwako pale unapohoji uwezo wa kufikiri wa mtu
Soma tena nilichoandika. Hapo kuna utata. Kama unafuatilia hili tukio ni kuwa kila mmoja amekuja na maelezo yake. Mtaa ambao polisi wanasema anaishi majirani na viongozi wanasema hawamjui na hawajawahi kusikia hilo jina. Concern yangu ni kuona baadhi ya members hapa wakilazimisha kuwa amejiua kwasababu ya kukosa ajira na hawataki kusikia vinginevyo! Yaani wanafurahia na kushangia kitendo cha kusema kuwa amejiua kwa kukosa ajira! Kulikoni?
 
kawaida tu hata asingekufa siku ile bado ipo siku angekufa, kwangu mimi katika kitu ambacho huwa sisikitiki wala kuona hata tone la chozi au kuwa na huzuni ni kuhusu mtu kufa-huwa naona ni hali ya kawaida tu.
 
Mm nilijiuliza hela ya kulewa alikuwa anatoa wapi yani huna ajira unapataje nguvu za kulewa kweli kama mapenzi hapo yaweza kuwa kweli.
miaka yako plzzzz

nani kakwambia kulewa kunahitaji milioni kadhaa, tusio na hela tunalewa kwa mia 2-5 f

izo hela tunapata kupitia mizinga ama kufadhiriwa kwenye baa. wengi hatulewi bia udhaniavyo unaijua pombe inaitwa "futika'
 
UPDATES: Kijana Aliyejiua Mwanza Alikuwa na Pesa, Alizidiwa na Stress*

Na Blogu ya Jamii, Mwanza

Saa chache baada ya kijana aliyejiua Mwanza, marafiki wa karibu wameshangazwa na polisi Mwanza kushindwa kufuatilia ukweli wa sababu za kijana aliyejiua katika jengo la Rock City Mall na kutaja tu masuala ya ajira.

Sasa ukweli kamili umeanza kujitokeza baada ya marafiki wa karibu kumueleza marehemu kama mtu ambaye chuoni hakuwa na mambo ya mabinti.

"Ila mwaka wa mwisho akawa na mpenzi, akazama sana katika mapenzi," ameeleza rafiki yake mmoja akihofia kutaja jina asihusishwe na masuala ya upelelezi.

Kama miezi miwili iliyopita inaelezwa baada ya marehemu kupata dili flani kikazi na kusafiri kwa muda, aliporejea alipata sms kutoka kwa mpenzi wake kuwa ameshaolewa na wasijuane tena.

"Kusema ajira ni kuzuga tu, jamaa alichanganyikiwa na hilo penzi lake la kwanza na tangu aambiwe kaachwa kila kazi anayofanya akipata hela analewa sana sana.Tulimuonya hakuelewa," aliongeza rafiki huyo akishauri ni vyema kwa sasa taasisi mbalimbali zikaweka vitengo vya ushauri wa mahusiano, vijana wengi mahusiano yanawamaliza.

"Pale alipolazwa polisi akionekana mlevi tu kwanza alikuwa na hela anakazi zake mwenyewe alikuwa anapata kuendesha maisha yake, kwa hiyo issue sio ajira, lakini polisi wangekuwa na washauri wa kisaikolojia huyu kijana wangemsikiliza na kumweka kwenye tiba maalum na kumwokoa na yaliyokuja kumkuta, jamii pana ina wajibu wa kufanya," aliongeza mmoja wa marafiki zake wakiwa na huzuni eneo la Furahisha.

__Bwana Alitoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe_
Acha uongo we kipeperushi cha watekaji.Issue hapa ni kukosa ajira haya mengine ya kwako
 
Huo ni uongo wa wazi kabisa. Taarifa hii ingekuwa ni kweli endapo tatizo la ajira kweli lisingekuwepo. Pia isingekuwa ngumu mtu ajiuaye kushindwa kusema anajiua kwa sababu ya mapenzi
 
Duuh Kinapotokea Kifo kila mtu husema lake lakini Mwisho wa siku marehemu ndo anajua siri ya Kifo chakee...!! Unaweza kuta mzee ana stress za mke wake za mapenzi lakini kwenda kazini Boss akamzingua tu kidogo jamaa akajinyongaaa... So mwisho wa siku Boss sio chanzo ila ni cause ya kifo..

Apumzike kwa amani
 
Uwa nikitazama crime and Investigation uwa nina conclude TZ kuna kesi nyingi polisi uwa wana conclude kuwa watu wamejiua au kufa kwa bahati mbaya wakati wameuawa. Narudia tena kuna kesi nyingi watu uwa wana get away with murder
Sawa kabisa!!!! Kuna watu wanauawa then wanatundikwa kwenye mti basi wao mara moja wanadai kajinyonga bila kufanya uchunguzi. Au anakutwa mtu kwenye maji wanasema tu amezama. Nakumbuka kifo cha kada mmoja hivi wa Chadema alishinda udiwani huko Geita baada ya muda akakutwa amekufa kwenye shimo la maji, polisi hapohapo wakasema aliteleza akatumbukia kitu ambacho sidhani kama ilikuwa kweli.
 
Kwakuwa mimi na wewe ni marehemu watarajiwa, basi tuambizane tu, maumivu ya kuachwa sio mchezo, ila tambua wapo wazuri na bora kuliko huyo aliyekuacha. Kama uliweza kumpata huyo, basi tambua utampata na mwingine.
 
Nawashangaa wanaosema eti hela ya pombe alikuwa anapatia wapi. Club za kienyeji Hizi unaenda bila hata pesa na unalewa
Nimeshangaa ulivyo andika bukuu unalewa hivi gongo kumbe haina gharama
 
Umekuja kuisafisha...

Tunaomba kanusho kwa njia ya maandishi na isainiwe na yule mkurugunezi wa nanilii...

Cc: mahondaw
 
Wana ccm wanadai amejiuwa kwa sababu ya mapenzi

Chadema nao wanadai ukosefu wa ajira...sasa sijui nani tumuamini!
 
Back
Top Bottom