Ijue tafsiri ya neno mnyonge

Ijue tafsiri ya neno mnyonge

Kwa mujibu wa kamusi mnyonge Ni " mtu siye na haki hadi mwenye nguvu aamue"

Nilikuwa najiuliza kwanini viongozi wa CCM wanapenda kuwaita machinga, mama ntilie, wakulima, wafugaji na watu wa kada hizi wanyonge kumbe wanamaanisha "WATU WASIO NA HAKI HADI VIONGOZI YAANA WANA CCM VIGOGO WAAMUE KUWAPA HAKI"

Basi sawa endeleeni kuhudumia wanyonge 🤣😂🤗
 
Mnyonge / mɲɔngɛ / nomino

Wanyonge (plural)

Ngeli za nomino: a-, wa-

MAANA YA NENO:
1. mtu dhaifu; mtu asiyekuwa na nguvu Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni (ms) Synonyms: mnyela
2. mtu mwenye tabia ya upole na ya kunyenyekea
3. mtu wa hali ya chini Mnyonge kupata haki ni mwenye nguvu kupenda (methali)

Synonyms (Neno mfanano) : kabwela

MY TAKE:
Hapo kwenye neno mfanano ndiyo pamenichosha kabisa KABWELA? Kwa hiyo mtu akituita sie Wanyonge katuita nyie MAKABWELA?!!

Wanasiasa tuache kutumia neno hili halipendezi na linatweza utu wa Mtanzania.

Nyadikwa

Kwani Kabwela kwa maana yako wewe ni nani??

Kwa maana ya hiyo kamusi uliyotuwekea Kabwela ni Mnyonge, mnyela, mtu mpole, dhaifu, mnyenyekevu nk,

Kwahiyo wanasiasa wanapoita watu Wanyonge maana yake pia ni Watu wanyenyekevu.
 
Kabwela ni mkataufuta! Asie na uhakika baadae atakula nini
 
Governor_Kaduma_on_Instagram:_“Tukikuwa_tunaitwa_hivi_ili_tuendelee_kujiona_sie_wahivyohivyo_t...jpg
 
Sisi wanyonge tunajijua wenyewe hizo maana zenu ni za kujitungia sifa zenu mnazotaka.
Wanyonge wote tunatumia magufuli bus terminal.
Wanyonge wote tunasubiri umeme wa rea.
Wanyonge wote tunasubiri maji ya dawasco.
Wanyonge wote tunasomesha shule za magufuli.
Wanyonge tunatumia hospitali za umaa.
Wanyonge tunapanda mwendokasi.
Wanyonge hatuweki na hatuna akiba ya vyakula au pesa.
Wanyonge tupo. Tunajua na tunaona wanaotujali.
 
Shule za magufuli ni zipi ...

Wewe una akili kweli mkuu ??

Ninawasiwasi na ubongo wako aisee ..
 
Mnyonge imetumika kisisasa.
Hakuna policy yoyote ya kuwainua hao wanaitwa wanyonge.
Myonge anatumika kujipatia kura nyingi na ni source of imaginary political support.

Zaidi ya kuwaacha barabarani hakuna financial support kwz machinga, mama ntilie bodaboda na hata wenye bajaji.

Ni utapeli mtupu kujiita mtu wa wanyonge maana ni jaribio la kujitafutia umaarufu bila jasho.
 
Na kadri Watanzania watakavyoendelea kulikumbatia hilo jina ndio tunazidi kujifukia kwenye lindi la dhiki unafiki uchawi husda kuombaomba nk nk.
 
Back
Top Bottom