Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Mnyonge / mɲɔngɛ / nomino
Wanyonge (plural)
Ngeli za nomino: a-, wa-
MAANA YA NENO:
1. mtu dhaifu; mtu asiyekuwa na nguvu Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni (ms) Synonyms: mnyela
2. mtu mwenye tabia ya upole na ya kunyenyekea
3. mtu wa hali ya chini Mnyonge kupata haki ni mwenye nguvu kupenda (methali)
Synonyms (Neno mfanano) : kabwela
MY TAKE:
Hapo kwenye neno mfanano ndiyo pamenichosha kabisa KABWELA? Kwa hiyo mtu akituita sie Wanyonge katuita nyie MAKABWELA?!!
Wanasiasa tuache kutumia neno hili halipendezi na linatweza utu wa Mtanzania.
Nyadikwa
Kabwela ni mkataufuta! Asie na uhakika baadae atakula niniKwani Kabwela kwa maana yako wewe ni nani??
Kwa maana ya hiyo kamusi uliyotuwekea Kabwela ni Mnyonge, mnyela, mtu mpole, dhaifu, mnyenyekevu nk,
Kwahiyo wanasiasa wanapoita watu Wanyonge maana yake pia ni Watu wanyenyekevu.
Shule za magufuli ni zipi ...Sisi wanyonge tunajijua wenyewe hizo maana zenu ni za kujitungia sifa zenu mnazotaka.
Wanyonge wote tunatumia magufuli bus terminal.
Wanyonge wote tunasubiri umeme wa rea.
Wanyonge wote tunasubiri maji ya dawasco.
Wanyonge wote tunasomesha shule za magufuli.
Wanyonge tunatumia hospitali za umaa.
Wanyonge tunapanda mwendokasi.
Wanyonge hatuweki na hatuna akiba ya vyakula au pesa.
Wanyonge tupo. Tunajua na tunaona wanaotujali.
Haaa! Rais wawayonge Nomino yake ikoje
😆😆😆Haaa! Rais wawayonge Nomino yake ikokje