Ijue teza ya Pineal

Ijue teza ya Pineal

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,692
pineal gland, ni tezi liyoko ndani ya mwili wa mamalia eneo la kichwani ambayo inaunda mfumo wa ufahamu katika kategori ya endocrine gland.

Tezi hii hutoa kemikali aina ya melatonin ambayo hutolewa na tryptophan na ni maalumu kwaajili ya ku simamia saiko ya ulalaji. ( circardian rhythm, sleep cycle). Ingawa tezi hii ni ndogo sana kiasi cha cm 0.8 na huweza kuwa na uzito wa gm 0.1. Tezi hii ni muhimu sana kwa aajili ya kutusababishia usingizi kwa sababu hutengeneza homoni iitwayo melatonin ambayo kazi yake ni kusimamia tabia zote mtu alalapo ingawa zipo homoni zaid ya tatu zinazotengenezwa na hii tezi kama vile somatostatin, norepinephrine na serotonin

Kwa watoto tezi hii ni kubwa zaidi lakin ukubwa huu hupungua kadiri mtoto anapozidi kukua na hasa akishafikia umri wa balehe na kubaki na ukubwa nilioutaja hapo juu. na hii ndio sababu watoto wadogo hulala zaid kuliko watu wazima.

maajabu ya homoni ya melatonin ni kwamba huzalishwa zaidi mtu akiwa eneo lenye giza kuliko eneo lenye mwanga na ndio maana wengine hawawez kupata usingizi wakiwa kwenye mwanga hata kama ni usiku.

kazi nyingine ambazo zimeonekana kufanywa na melatonin ni pamoja na kuzuia utenegenezwaji wa gonadotropin releasing hormone (GTRH) kutoka kwenye sehem ya ubongo iitwayo hypothamus. hii husabbaisha kushuka kwa kiwango cha lutenizing hormone (LT) pamoja na follicle stimulating hormone (FSH) kutoka kwenye pituitary gland.

Kwa binadamu kazi halisi ya melatonin bado haijajulikana zaid ingawa kiwango chake ni kikubwa zaid kwa watoto ukilinganisha na kwa watu wazima. Kiwango kikubwa cha homoni hii kwa watoto ndicho huchangia kuwepo na kuchelewa kwa sexual development.
 
Ubarikiwe kwa useful Info.

asante sana ni muhimu sana kufundishana kuhusu mambo ambayo yako kimya katikati yetu.
endocrine system iko kimya sana yaani utakuta wengi wanaingolea kuhusu insulin tu na labda ovary na testes lakin nyingine zote hatujaweza kujifunza na kuzielewa.
 
Shukran gfsonwin, hii tezi ina unauhusiano wowote na vitu vyenye caffeine? Mimi nikinywa redbull au kahawa usingizi hauji kabisa, ndio kusema nikinywa vitu hivyo inazuia uzalishwaji wake?
 
Last edited by a moderator:
asante sana ni muhimu sana kufundishana kuhusu mambo ambayo yako kimya katikati yetu.
endocrine system iko kimya sana yaani utakuta wengi wanaingolea kuhusu insulin tu na labda ovary na testes lakin nyingine zote hatujaweza kujifunza na kuzielewa.

Endless knowledge, tunahitajia waungwana methalio !
 
Shukran gfsonwin, hii tezi ina unauhusiano wowote na vitu vyenye caffeine? Mimi nikinywa redbull au kahawa usingizi hauji kabisa, ndio kusema nikinywa vitu hivyo inazuia uzalishwaji wake?
Ndg.Utafiti.. Mie nikinywa hata maji kabla ya kuenda kulala basi usingizi hupotea kwa mda wa masaa!! je, kuna uhusiano na glands hizo?
 
Ndg.Utafiti.. Mie nikinywa hata maji kabla ya kuenda kulala basi usingizi hupotea kwa mda wa masaa!! je, kuna uhusiano na glands hizo?

Mimi siongelei ule muda wa kulala, mimi nikinywa ata mida ya jioni basi usiku wake inaweza kufika asubuhi bila kusinzia....kuhusu swali lako subiri dokta hapo atatoa jibu....
 
Shukran gfsonwin, hii tezi ina unauhusiano wowote na vitu vyenye caffeine? Mimi nikinywa redbull au kahawa usingizi hauji kabisa, ndio kusema nikinywa vitu hivyo inazuia uzalishwaji wake?

ahsante sana kakaa sasa iko mhivi caffeine inastimulate epinephrine and norepinaphrine na hizi ni hormone zinazotolewa na sehem ya ya kortex ya adrenal gland ingawa pia pineal gland huzizalisha kama hormone za nyongeza. Kazi kubwa ya hizi homone ni kustimulate mwili ikiwemo kungeza kiwango cha oksjeni kinachopatikana kwenye ubongo, kuongeza msukumo wa damu kwenye misuli na pia kuchangamsha mwili.

sasa caffeine hufanya kazi ya kustimulate uzalishwaji wa adrenaline hormone kwa kiwango kikubwa na hivyo kuufanya ubongo uwe na oksijeni ya kutosha na hivyo usingizi unapotea.

kumbuka kwamba ili ulale lazima melatonin iwe kwa kiwango kikubwa na sasa hii homone huzalishwa pale mwili unapokuwa uko katiika resting position, pia kama oksijen kwenye ubongo ni ndogo na kama kuna giza.
 
Ndg.Utafiti.. Mie nikinywa hata maji kabla ya kuenda kulala basi usingizi hupotea kwa mda wa masaa!! je, kuna uhusiano na glands hizo?
unapokunywa maji tayari mwili wako unajua kwamba kuna kitu kimeingia na maji huongeza hewa ya oksijen mwilini na hivyo hufanya mwili kuchangamka zaid. ndio maana usingizi hupaa.

sasa wewe siku jaribu hii kama uko kazini na unajihisi umechoka sana chukua maji ya baridi kabisa alafu changanya na maji ya moto yaliyochemka kisha unywe uone utapata uzima usio wa kawaida. sababu kubwa ni umeongezsa kiwango kingi cha oksijeni kilicho na molecules ambazo zinaweza kuelea kwa wepesi na hivyo zikasafiri haraka zaidi.
 
Mimi siongelei ule muda wa kulala, mimi nikinywa ata mida ya jioni basi usiku wake inaweza kufika asubuhi bila kusinzia....kuhusu swali lako subiri dokta hapo atatoa jibu....

mimi sio daktari ni mwalimu na hapa natumia uzoefu wangu wa kufundisha
 
unapokunywa maji tayari mwili wako unajua kwamba kuna kitu kimeingia na maji huongeza hewa ya oksijen mwilini na hivyo hufanya mwili kuchangamka zaid. ndio maana usingizi hupaa.

sasa wewe siku jaribu hii kama uko kazini na unajihisi umechoka sana chukua maji ya baridi kabisa alafu changanya na maji ya moto yaliyochemka kisha unywe uone utapata uzima usio wa kawaida. sababu kubwa ni umeongezsa kiwango kingi cha oksijeni kilicho na molecules ambazo zinaweza kuelea kwa wepesi na hivyo zikasafiri haraka zaidi.
Indeed, hiyo nimethibitisha 100%.
 
Wewe una inversation kwenye mwili wako,feel back jinsi ulivyokuwa miezi 3 na sasa ukoje
 
Back
Top Bottom