gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,692
pineal gland, ni tezi liyoko ndani ya mwili wa mamalia eneo la kichwani ambayo inaunda mfumo wa ufahamu katika kategori ya endocrine gland.
Tezi hii hutoa kemikali aina ya melatonin ambayo hutolewa na tryptophan na ni maalumu kwaajili ya ku simamia saiko ya ulalaji. ( circardian rhythm, sleep cycle). Ingawa tezi hii ni ndogo sana kiasi cha cm 0.8 na huweza kuwa na uzito wa gm 0.1. Tezi hii ni muhimu sana kwa aajili ya kutusababishia usingizi kwa sababu hutengeneza homoni iitwayo melatonin ambayo kazi yake ni kusimamia tabia zote mtu alalapo ingawa zipo homoni zaid ya tatu zinazotengenezwa na hii tezi kama vile somatostatin, norepinephrine na serotonin
Kwa watoto tezi hii ni kubwa zaidi lakin ukubwa huu hupungua kadiri mtoto anapozidi kukua na hasa akishafikia umri wa balehe na kubaki na ukubwa nilioutaja hapo juu. na hii ndio sababu watoto wadogo hulala zaid kuliko watu wazima.
maajabu ya homoni ya melatonin ni kwamba huzalishwa zaidi mtu akiwa eneo lenye giza kuliko eneo lenye mwanga na ndio maana wengine hawawez kupata usingizi wakiwa kwenye mwanga hata kama ni usiku.
kazi nyingine ambazo zimeonekana kufanywa na melatonin ni pamoja na kuzuia utenegenezwaji wa gonadotropin releasing hormone (GTRH) kutoka kwenye sehem ya ubongo iitwayo hypothamus. hii husabbaisha kushuka kwa kiwango cha lutenizing hormone (LT) pamoja na follicle stimulating hormone (FSH) kutoka kwenye pituitary gland.
Kwa binadamu kazi halisi ya melatonin bado haijajulikana zaid ingawa kiwango chake ni kikubwa zaid kwa watoto ukilinganisha na kwa watu wazima. Kiwango kikubwa cha homoni hii kwa watoto ndicho huchangia kuwepo na kuchelewa kwa sexual development.