Unaposoma biblia zingatia kuwa unasoma kitabu kilichoandikwa kwa kuzingatia mila na desturi za kiarabu!
unaposoma utamaduni wa waarabu zingatia pia matumizi ya namba na maana zake!!
mfano katika biblia kuna matumizi ya namba 40 mara nyingi sana
utumwani misri miaka 40 mara 10
waisrael jangwani miaka 40
waisrael waliofika israel toka misri elfu 40
Yesu akafunga jangwani siku 40
roho mt. alishuka baada ya siku 40 baada ya ufufuko.
matumizi ya 40 katika fasihi ya kiarabu ina maana kwamba " Ni kipindi kirefu cha wakati kati ya tukio moja katika historia na tukio jingine "
Rejea "siku za mwizi ni 40 "
hii ni nahau ya kiswahili yenye asili ya kiarabu.
ikiwa haina maana kwamba mwiz siku ya 40 lazima akamatwe!!
ila, hata kama utaiba siku alfu, ipo siku utakamatwa!
athari hizi za matimizi ya namba ni pamoja na namba 3 na namba 7.
pia utamaduni huu hauishii hapo bali utamaduni wa kiarabu na mtazamo wa mwanamke kama kiumbe duni na mnyonge unaonekana ndani ya biblia na upo uarabuni pia hadi leo.
Tunaona mwanamke hana mamlaka sana ndani ya biblia ila kwa kiwango kidogo sana (rejea Esta) . mwanamke yupo kimya! MTAZAMAJI ASIYE HAKI.
Wana wa yakobo walikuwa 13 (akiwemo Dina) lakin tunatajiwa 12 tu wa kiume.
Maria Magdalena baada ya kupona kupigwa mawe baada ya kuzini na kukamatwa( utamaduni wa kiarabu pia) alikuwa mfuasi mzuri sana wa yesu, na aliambatana nae kila mahali alipoenda yesu ( rejea : nyumbani kwa zakayo na ufufuko wa yesu "alikuwa wa kwanza kuwasili kaburini " )
Yote hayo yapo ndani ya biblia na kumbuka.
"USOMAPO BIBLIA ZINGATIA MAANA YA NAMBA KWA UTAMADUNI WA WAARABU "