Ijumaa Kuu na katazo la kula nyama

Ijumaa Kuu na katazo la kula nyama

Ntozi

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2021
Posts
226
Reaction score
300
Naombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo kula nyama siku ya Ijumaa kuu.

Najua ni suala la kiimani, lakini msingi wa Imani ya kikristo ni Biblia, hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia.
 
Naombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo Kula nyama siku ya Ijumaa kuu.Najua ni suala la kiimani,lakini msingi wa Imani ya kikristo,ni Biblia,hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia
inaitwa KUENZI! sawa na kuenzi karume Day!
 
Siku ya huzuni unaanzaje kula vinono?Anateswa,kutwezwa,kutokwa damu na kusulubiwa msalabani hadi kufa.Kula nyama ni kiashiria cha furaha na ufahari.Kwa nini ulie huku unacheka?Halafu ni siku moja tu/masaa machache nini kinakushinda?Kwani kila siku huwa unakula nyama?
 
Siku ya huzuni unaanzaje kula vinono?Anateswa,kutwezwa,kitokwa damu na kusulubiwa msalabani hadi kufa.Kula nyama ni kiashiria cha furaha na ufahari.Kwa nini ulie huku unacheka?Halafu ni siku moja tu/masaa machache nini kinakushinda?Kwani kila siku huwa unakula nyama?
Kunywa mvinyo inaruhusiwa?
 
Kufa kwa Yesu kristo msalabani ni jambo la furaha, shangwe na ushindi katika imani ya Kikristo maana ndio lilizaaa ukombozi, sasa kwanini watu wakae na huzuni, unyonge na kujinyima?

Wakristo kuleni vinono leo.
 
Naombeni anaelijua andiko linalokataza wakristo Kula nyama siku ya Ijumaa kuu.Najua ni suala la kiimani,lakini msingi wa Imani ya kikristo,ni Biblia,hivyo tujuzane hilo andiko liko kitabu gani ndani ya Biblia
KUTOKULA nyama IJUMAA KUU ni Mojawapo ya AMRI YA KANISA(KATOLIKI)!

"SHIRIKI LITURUJIA JUMATANO YA MAJIVU, NA IJUMAA KUU ILIYO SIKU YA KUACHA KULA NYAMA"
 
Siku ya huzuni unaanzaje kula vinono?Anateswa,kutwezwa,kutokwa damu na kusulubiwa msalabani hadi kufa.Kula nyama ni kiashiria cha furaha na ufahari.Kwa nini ulie huku unacheka?Halafu ni siku moja tu/masaa machache nini kinakushinda?Kwani kila siku huwa unakula nyama?
Kwa iyo misibani tunavyokula nyama inakuaje?
 
Back
Top Bottom