Mpaka unganganie sabato iliokomeshwa na Mungu mwenyewe na kutangazwa kama ilikuwa ni kivuli cha mambo ya kale. '(KIVULI HAKIVALISHWI SUTI JOANNAH)
tuangalie kama kweli Paulo alibadilisha sabato. Je ni kweli kwamba Paulo aliibadilisha sabato? Au yeye Paulo hakutunza sabato? Kwani desturi yake ilikuaje?
“Na Paulo kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu.” Matendo 17:2
Wengine bado watasema, “hamna alikutana na Wayahudi pekee siku ya sabato, lakini Wayunani alikutana nao Jumapili.”
Je ni kweli kwamba Paulo hakukutana na watu wa mataifa siku ya sabato? Au Je alikutana nao siku ya Jumapili?
“(Paulo) Akatoa hoja zake katatika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.” Matendo 18:4
Wayahudi walipomshitaki Paulo, wakidai amevunja sheria. Je Paulo mwenyewe alisemaje? Aliposingiwa kuwa amevunja sheria Paulo Alisema.
“Ila neno hili naungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.” Matendo 24:14
Kwa hiyo Paulo aliiamini torati na manabii, na tofauti kati yake na Wayahudi ilikuwa ni imani ya Yesu, na siyo sheria au torati. Kwa hakika Paulo mwenyewe alipojitetea juu ya shitaka la kuvunja shelia alisema.
“…Mimi sikukosa neno juu ya sheria ya Wayahudi…sikuwakosa Wayahudi neno, kama wewe ujuavyo sana.” Matendo 25:8, 10
Hata walipomfikisha Rumi, Paulo aliendelea kusema wazi kuwa hajakosa katika sheria yoyote ile, alisema.
“…Ndugu zangu, ingawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa, tokea Yerusalemu.” Matendo 28:17