Sabato ya siku ya saba ilitolewa kwa watu wa Mungu wakati wa uumbaji. Hii ina maana kwamba Sabato ilikuwepo kabla dhambi haijaingia ulimwenguni, na hivyo basi kabla ya sheria za kafara na maagizo kuwa zimewekwa. Hivyo, Sabato ya kila juma ya Mungu isingekuwa sehemu ya sheria za maagizo, na isingekuwa imegongomelewa msalabani samabamba na sheria za maagizo.
Kutokana na kwamba wengi wana shida kutofautisha baina ya sheria za maagizo zilizoandikwa na Musa, na Sheria takatifu ya amri 10 iliyonenwa na Mungu, hebu na tuchunguze tofauti za wazi baina ya hizi mbili.
Sheria za maagizo zinahesabiwa kama “sheria ya amri iliyo ya jinsi ya mwili” (Waebrania 7:16); na Sheria takatifu ya Mungu, imesemwa, “Twajua ya kuwa torati asili yake ni rohoni.” Warumi 7:14. Moja ni sheria ambayo “hapana budi sheria nayo ibadilike.” Waebrania 7:12. Sheria takatifu ni sheria ambayo Kristo husema, “Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” Mathayo 5:18.
Sheria ya maagizo ilikuwa ni “kivuli cha mema yatakayokuwa” (Waebrania 10:1), na iliwekwa tu “hata wakati wa matengenezo mapya.” Waebrania 9:10. Lakini nyingine ilikuwa ni sheria takatifu, ambayo inasemwa na Yohana, “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi [wa sheria].” 1 Yohana 3:4. Moja ni nira isiyoweza kubebwa (angalia Mdo 15:10); nyingine ni ile “sheria ya uhuru” ambayo kwayo tutahukumiwa (angalia Yakobo 2:8-12).
Sheria ya maagizo ni ile ambayo Kristo “aliiondoa katika mwili wake” (angalia Waefeso 2:15); sheria takatifu ni ile ambayo hakuja kuiondoa (angalia Mathayo 5:17). Moja inahesabiwa kama “hati ya kutushitaki kwa hukumu” “iliyokuwa na uadui kwetu,” ambayo iligongomelewa msalabani na kuondolewa kwa kifo cha Kristo (angalia Wakolosai 2:14); nyingine ni ile Sheria ambayo alikuja kutimiliza na kuitukuza (angalia Isaya 42:21) na ambayo Yakobo hueleza kama “sheria ya kifalme” ambayo ni dhambi kuiasi (angalia Yakobo 2:8-12). Moja ilikuwa ni sheria ya muda ambayo ilibatilishwa “kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake” (Waebrania 7:18); nyingine ni Sheria isiyobadilika ya milele ambayo haiwezi kutanguliwa: “Basi, je twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.” Warumi 3:31.
Sheria ya maagizo ni sheria ambayo ilikuwa ni ukuta wa katikati wa kiambaza baina ya Wayahudi na Mataifa (angalia Waefeso 2:14); nyingine ni Sheria ile, kazi ya hiyo hata mataifa wanasemwa kuwa imeandikwa katika mioyo yao (angalia Warumi 2:14-15). Moja ni sheria ya amri iliyo katika maagizo (angalia Waefeso 2:15); Sheria takatifu ni amri za Mungu, ambazo ni wajibu wa jamii ya wanadamu kuzitunza (angalia Mhubiri 12:13).
Hii Sheria kuu takatifu ya amri 10 inaletwa mbele na ujumbe wa malaika wa tatu (angalia Ufunuo 14:9-12). Hii ni Sheria ambayo masalio wa mbegu ya mwanamke walikuwa wanatunza wakati joka alipofanya vita juu yao (angalia Ufunuo 12:17). Sheria hii takatifu itawahakikishia, wale wote wanaoitunza, haki kuingia mbinguni na kula mti wa uzima (angalia Ufunuo 22:14).
Hakika, sheria hizi mbili hazitakiwi kuchanganywa. Sheria takatifu ilitimilizwa, kutukuzwa, kuadhimishwa, na ni takatifu, ya haki, ya kiroho, njema, na ya kifalme; wakati nyingine ni ya mwilini, kivuli, mzigo, na iliondolewa, kuvunjwa, kufutwa, kugongomelewa msalabani, kubadilishwa, na kubatilishwa kwa sababu ya udhaifu wake na kutofaa kwake.