Ijumaa ya leo ikukumbushe tu Sabato ni Jumamosi

Mimi Ni mfuasi wa Mungu ndio maana natetea kuhusu kufuata amri zake na kuzitunza, Hakuna sehemu Mungu amebatilisha Sabato ...Hakuna amendment ya amri kumi Hakuna!Amri zitabaki kuwa kumi na amri mpya iliyotolewa katika agano jipya Ni UPENDO basi.
 

Je, Mungu alijua kuwa kuna taasisi inayompinga ambayo ingejaribu kufanya badiliko hilo?​

“Naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.” Dan. 7:25.

Taasisi hii ingediriki kubadili majira (muda) aliyopanga Mungu pamoja na Sheria zake. Zingatia kuwa “atanena maneno kinyume chake Aliye juu.”


 
Daah yaani hapa kailezea fresh Ila watabisha...Unajua watu Ni wavivu kutafuta ukweli Ila Kuna vitu vingi Sana tunafanya ambavyo tunaenda ndivyo sivyo....@ Beyond the infinity
KUSOMA VITABU KUNAFAIDA KUBWA SANA....
ONA HII ..HII NI KATEKISIMU YA WAKATOLIKI WAMEJIELEZA WAZI

SHIDA YA WAKATOLIKI NI KWAMBA HAWASOMI HATA VITABU VYAO NDIYO MAANA WANADANGANYWA KIRAHISI..
View attachment 2188967
 
Mpaka unganganie sabato iliokomeshwa na Mungu mwenyewe na kutangazwa kama ilikuwa ni kivuli cha mambo ya kale. '(KIVULI HAKIVALISHWI SUTI JOANNAH)
tuangalie kama kweli Paulo alibadilisha sabato. Je ni kweli kwamba Paulo aliibadilisha sabato? Au yeye Paulo hakutunza sabato? Kwani desturi yake ilikuaje?

“Na Paulo kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu.” Matendo 17:2

Wengine bado watasema, “hamna alikutana na Wayahudi pekee siku ya sabato, lakini Wayunani alikutana nao Jumapili.”
Je ni kweli kwamba Paulo hakukutana na watu wa mataifa siku ya sabato? Au Je alikutana nao siku ya Jumapili?

“(Paulo) Akatoa hoja zake katatika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.” Matendo 18:4

Wayahudi walipomshitaki Paulo, wakidai amevunja sheria. Je Paulo mwenyewe alisemaje? Aliposingiwa kuwa amevunja sheria Paulo Alisema.

“Ila neno hili naungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.” Matendo 24:14

Kwa hiyo Paulo aliiamini torati na manabii, na tofauti kati yake na Wayahudi ilikuwa ni imani ya Yesu, na siyo sheria au torati. Kwa hakika Paulo mwenyewe alipojitetea juu ya shitaka la kuvunja shelia alisema.

“…Mimi sikukosa neno juu ya sheria ya Wayahudi…sikuwakosa Wayahudi neno, kama wewe ujuavyo sana.” Matendo 25:8, 10

Hata walipomfikisha Rumi, Paulo aliendelea kusema wazi kuwa hajakosa katika sheria yoyote ile, alisema.

“…Ndugu zangu, ingawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa, tokea Yerusalemu.” Matendo 28:17
 
Mbali na yote, nashukurigi sama mola we Catholics hatujawahigi kutikiswa na lolote[emoji23][emoji23] sisi amani tunazo. Ila wap wanateseka juu yetu. Haya kazi iendelew

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
“Swali-Siku ya Sabato ni ipi?

Jibu-Jumamosi ni siku ya Sabato.

Swali-Kwanini tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi?

Jibu-Tunatunza Jumapili badala ya Jumamosi kwa sababu kanisa la katoliki, katika balaza la Laodikia (364 B.K.), liliihamisha kutoka Jumamosi kwenda Jumapili.

Swali-Kwanini kanisa la katoliki liliweka Jumapili badala ya Jumamosi?

Jibu-Kanisa liliweka Jumapili badala ya Jumamosi, kwa sababu Kristo alifufuka kutoka kwa wafu

Jumapili, na Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume Jumapili.

Swali-Kwa mamlaka gani kanisa liliweka Jumapili badala ya Jumamosi?

Jibu-Kanisa liliweka Jumapili badala ya Jumamosi kwa ukamilifu wa ule uwezo wa Uungu ambao Yesu Kristo aliutoa kwake.” –

The Convert Catechism of Catholic Doctrine, Peter Geiermann, C.SS.R., (1946), p 50
 
Reactions: Ilu
Shukraaan kwa kuwajibu mkuu. Mimi wala siwezi tumia nguvu zangu kuwaelezea yote haya. Tupewe tuzo ya civilization katika dini. Sisi hatujawahi kaa tukiwafikiria ila wao daima wanatuwazia sisi. Sijawahi jiumiza juu yao

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Reactions: Ilu
Wewe jamaa kuwa mwelewa basi,Yesu kabla ya ufufuko wake alisali siku ya sabato km Myahudi mwingine yeyote, ilikuwa ni desturi yao, kulikuwa hakuna Kanisa la Jumapili,Lkn kwa kufufuka kwake siku ya kwanza ya juma yaani Jumapili ndio inatufanya tusherehekee siku hiyo Ufufuko wake hivyo kila Jumapili ni Pasaka ndogo, Ufufuko wa Yesu Kristo ni kitu kikubwa sana kuliko hiyo sabato mnayoing'ang'ania.Hata hivyo Yesu hakuwa Msabato km ninyi bali alifuata taratibu za dini ya Kiyahudi,ili kutimiza taratibu za Agano la kale na ili kuwapata watu ambao aliwahubiria Neno la MUNGU.Hivyo sasa hivi hatuishi kadiri ya Agano la kale Bali kadiri ya Agano jipya maana Agano jipya ni Kuu kuliko Agano la kale, rejea Waebrania 8:8-13.
 
kwahio siku ya sabato hutakiwi kufanya kazi yoyote?
Yesu aliwashushua hao wanaojidai sabato ndiyo msingi, akamponya mgonjwa. Hiyo yote kuwakomesha kuwaonyesha, kwenye Hilo Mungu yupo flexible, haiwezekani mnyama atumbukie kwenye shimo, usimuokoe kisa sabato, au usiwanyweshe maji kisa Sabato,

Huu ufarisayo na usadukayo upo mpaka kizazi cha dot com.

Wasabato wanawake wasisuke, waafrika hao, kina wazungu minywele hiyo, yaani Mie nawakubali wazee wa Mila. Hizi dini zilizokuja na merikebu, baguzi na zinanyanyasa na kunyanyapaa Sana!

Dini zihubiri upendo, Amani na matumaini n.k
 

Mkuu vipi kuhusu sheria ya kutokula nguruwe nayo ni kivuli cha mambo yajayo?
 
utumwa upo kila mahali mkuu ni mtu mwenyewe ndio mwenye maamuzi ya kujinasua, mbali na hizi dini zilizokuja kwa meli hata imani za mababu zinamambo flani ya ki-utumwa pia.

unachukua mazuri yanayokufaa (kmf. mafundisho ya namna bora ya kuishi na jamii) unawaachia mabaya (kmf. masharti yasiyo na msingi wowote)
 
Kweli kabisaaaah!
Nilikuwa na boss Polish, mzungu, kipindi Fulani hakuwa na dini wala dhehebu, Ila alikuwa na wema uliopitiliza, hajui biblia, kurani wala Buddha Ila alikuwa mwema Sana.
Hakasiriki, anaongea facts, Hana unafiki sijui fitina za kumsema mtu pembeni hadhulumu, alikuwa mtu wa haki na msaada Kwa wote alioweza kuwafikia.

Sijui huko aliko Ka mzima au alishatangulia mbeleni. Mungu hawezi kuacha mtu kama Yule kumuingiza katika ufalme wake.
 
Ukianza fikiri kwa akili yako ukaacha kufikiri kwa mapokeo uliyopokea urudi usome tena ulichoandika alafu ujiulize huyo Mungu wako anataka umuabudu jumamosi TU au anahitaji Kila siku na Kila wakati umuabudu,
 
Kasome Matendo ya mitume 20:7 alafu urudi tena tuendelee kuelimishana
 
We mkuu nimesoma comments zako nyingi humu
nina uhakika tukikaa tukijadiliana kwa kina unaweza ukasilimu kabisaaa
 
Ukianza fikiri kwa akili yako ukaacha kufikiri kwa mapokeo uliyopokea urudi usome tena ulichoandika alafu ujiulize huyo Mungu wako anataka umuabudu jumamosi TU au anahitaji Kila siku na Kila wakati umuabudu,
Kuna miss nyingi sana kwenye ufikiri juu ulioutoa.

Mungu ni Mungu WA mahusiano. Ndio maana licha ya siku zote sita kuwa na wewe anajua utakuwa na kazi za kufanya. Alafu wewe ni kiumbe cha mahusiano huwezi kuwa peke yako tu. Akaweka mfumo bora kabisa baada ya yote MWANADAMUaache yote akusanyike na wenzake kufurahia Mungu wake huku akigusa maisha ya wenzake wanaopitia nyakati ngumu.


Mungu amenyooka, naona unataka kumpindisha
 
Haya Bwana leo tumeiona Sabato na Tumeabudu.
 
Wasabato buana mna kazi kweli kweli… sabato sio tiketi ya kuona ufalme wa Mungu abiii!
Ni matendo yako duniani ndio yatakuwezesha kuuona ufalme wa Mungu au tuseme kwenda mbinguni. Aliye na dini asiye na dini Imani ndio kila kitu… Kwa Mungu siku zote ni sawa aliaagiza tutenge siku moja tu ya kumwabudu…. so iwe Jumamosi Jumapili Ijumaa zote ni siku za Bwana msitengeneze utengano…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…