Ikeda air Freshener Vs matatizo ya kifua!

Mchina katuletea fursa bei cheee, Harufu Kali ambayo inasababisha kifua/mafua kila ukiivuta. Chukua tahadhari kabla hujaumaliza mwendo. Asante
Si kila kitu kinapotokea lazima tukitumie.. Tuwe tayari kukubali baadhi ya vitu vitupite. Tangu nilipotambua hili najiona nimekuwa na maisha mazuri sana. Yaani mimi huwa sipelekeshwi na "trends" hata siku moja.
 
Ule mfuniko wake unaufungua kidogo sana ili harufu itoke kidogo kidogo wengi wanakosea wanapotoa mfuniko wote harufu ni kali sana hasa ukifunga na vioo
Ushawahi kujipulizia perfume nyingi(yenye kiwango sio feki) ukaumwa kifua,mafua,kuvimba macho?
 
Mie mpaka kitandani nilikuwa nasikia manukato yake..
Sasa nimeamka usiku na wenge naanza kutafuta harufu ya nini nilijua kuna kitu nimekilalia...

Hatari sana...
Kalivyoisha sijanunua ukichanganya na mafua yalikuwa yananizonga...
Haya nipo hapa nasoma comments turudi kwenye poppy au?
 
Hi kitu nilikua natamani kuiagiza niwekee dukan Na kwenye gari
Biashara ya Ikeda inakwenda kufa kwenye soko la Tanzania.

Nilishaenda kwenye maduka ya urembo wa magari mara kadhaa nikawa kila mara naulizia bei, wengine elfu 25, wengine wanakwambia original elfu 70 nikaachana nazo nikawa nanunua hizi za kawaida za elfu 10, elfu 12 kwenye supermarket.
 
Mimi kuna duka nilienda jamaa aliniambia original elf 90,nikaaga fast...
 
Mimi kuna duka nilienda jamaa aliniambia original elf 90,nikaaga fast...
Wajinga sana hao wafanyabiashara, yaani ninunue air freshener kwa elfu sijui 70, siwezi. Hata elfu 20 siwezi nununua, sanasana ikizidi labda elfu 15.
 
Si kila kitu kinapotokea lazima tukitumie.. Tuwe tayari kukubali baadhi ya vitu vitupite. Tangu nilipotambua hili najiona nimekuwa na maisha mazuri sana. Yaani mimi huwa sipelekeshwi na "trends" hata siku moja.
Hata TOZO haikupelekeshi sio?
 
Iliyonipa mafua jamaa hakutoa mfuniko wote , alitoboa tu vitundu vidogo kama vitatu hivi,
Leo pia nimeingia kwa gari ya jamaa yangu nikaona katoa kabisa na mfuniko wenyewe, asee nimetoa very lame exucuse nikafungua mlango na kutoka nje, akaondoka peke yake
Ule mfuniko wake unaufungua kidogo sana ili harufu itoke kidogo kidogo wengi wanakosea wanapotoa mfuniko wote harufu ni kali sana hasa ukifunga na vioo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…