Ikeda air Freshener Vs matatizo ya kifua!

Ikeda air Freshener Vs matatizo ya kifua!

Mchina katuletea fursa bei cheee, Harufu Kali ambayo inasababisha kifua/mafua kila ukiivuta. Chukua tahadhari kabla hujaumaliza mwendo. Asante
Aisee hii kitu ina ukweli, the very first time niliikuta kwenye gari ya jamaa yangu tulikuwa na roadtrip moro-iringa-dom-mikoa ya kanda ya kati.. zile siku mbili kifua kilikuwa kizito mno.. baada ya safari nikapigwa na mafua makali na maumivu ya kichwa (nikawa na mixed thoughts kuwa labda ni kacovid au niko alergic na yale manukato)

Over time nikaja kuconfirm kile kidude kwangu ni changamoto kuna jamaa yangu aliazima usafiri na akajiongeza akakanunua kile kidubwasha akakiweka, alivyorudisha nikawa napitia hali ya kifua kuwa kizito, mafua feki, kichwa kinagonga na usiku kama nakuwa nawashwa hivi, halafu ile harufu inabaki kwenye mwili..

Yale manukato hayajatengenezwa kwa ajili ya mjumbe kama mimi..
Duh!
Ukute kuna madhara mengine ya kudumu kutokana na hizo vitu🙄
Vitu toxic kama hivyo vingezuiwa tu kuingia nchini..
Sijui mamlaka gani inahusika, TBS, TFDA, nk?!!!
 
asante kwa kunivumbua..jana nlikua namkagulia mdau gari yake.Nilikaa ndani ya gari almost 5mins..hicho kilikua kipo wazi chote kwa juu..Leo ninaumwa sana mafua..na kichwa.nadhani hio ndio sababu.
 
asante kwa kunivumbua..jana nlikua namkagulia mdau gari yake.Nilikaa ndani ya gari almost 5mins..hicho kilikua kipo wazi chote kwa juu..Leo ninaumwa sana mafua..na kichwa.nadhani hio ndio sababu.
Ikeda sio kifua Tu kinaathirika hata nguvu za kiume zinakata wengi wanaotumia ikeda wanachapiwa Sana wake zao
 
Back
Top Bottom