Ikifika 2025, Utajisikiaje ukijua kumbe Lissu naye ni Askari (planted)

Lissu hana misimamo ya kudumu. Msimamo wake dhidi ya ufisadi wa Lowassa bado anao? Kigeugeu tu kama wanafiki wengine wa Lumumba au kama wanafiki wengine wa ufipa.
 
Ni wachache sana watakaokulewe hapa, weng watajib kimihemuko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo wengi mmeanza kusikia habari za TL hivi karibuni.
Tumeanza kusikia zamani sana hadi zikafika nyakati za kati akiweka msimamo Lowassa ni Fisadi kubwa sana, baadae Lowassa msafi, tukafika hapa tulipo anapigania uhuru wa kuongea n.k. Pia anasema tusizuie makinikia tutanyolewa ...... mara MIGA. Kisha tunaona wazungu wanakunywa juice na Le Profeseri Pala mwenye MAGAMBA huku waki negotiate namna ya kucheua mpunga wa kutuchezea rafu kwenye uwanja wa makinikia.
 
Lissu hana misimamo ya kudumu. Msimamo wake dhidi ya ufisadi wa Lowassa bado anao? Kigeugeu tu kama wanafiki wengine wa Lumumba au kama wanafiki wengine wa ufipa.
Cha ajabu Slaa alikua ana misimamo balaa lkn alikua anafungiwa na mkewe kulala ndani ya nyumba anaishia kulala kwenye gari usiku kucha.Hatariii
 
Cha ajabu Slaa alikua ana misimamo balaa lkn alikua anafungiwa na mkewe kulala ndani ya nyumba anaishia kulala kwenye gari usiku kucha.Hatariii
Yeah, Siasa bila unafiki haziendi mkuu.
 
One of the longest inpiratinal Quotes I have never heard no where before...*umesiliba mkuu HEKO!
 
Mkuu umenikuna sana. Wengi hawaelewi ya kwamba ccm ina watu wamesomea siasa nchi mbalimbali za dunia hii hivyo wana mbinu nyingi sana za kuhusiana na swala zima la siasa.

Mfano mzuri ni Lowasa. Kwa miaka mingi mh huyo akiwa mbunge amekuwa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Bunge. Wala hatujiulizi sifa za m'kiti wa kamati hiyo ni zipi. Matikeo yake ndiye kawa lulu ya upinzani.

Tutakumbuka shuka saa 1 asubuhi.
 
Vichwa vyenyewe hivi masiponji na bado unaleta mambo magumu hivi, watakuelewa lini hawa? Kwani za mavideo kwiini hamna?
 

Probably! Unaweza ukawa na Hoja Njema na Nzuri kwa vijana Wapenda mabadiliko! Kuna Mambo hapo Umeeleza ya na sense kabisa! Kulalamika na Kuamini Wanasiasa 100% ni jambo la hatari kwa sababu Wanasiasa hawaaminiki! Wanabadilika ni Tofauti na Wanafalsafa! Leo anaweza akasema Maji sio Kipaumbele chetu! kesho Akasema Tanzania bila maji Haiwezekani!
Kuhusu Tundu A. Lisu! Hujamtendea haki hata kidogo! Unamshuku bila hoja za msingi! Kama una hoja juu ya loyalty ya Tundu Lisu juu ya anayoyapigania weka doubts zako vema zieleweke! Unganisha Matukio ya Historia yake Kisiasa! Kitaaluma! Unapomfikiria Kuwa anawezekana ni Planted! bila kuonesha hizo dalili ya kwamba yeye ni Planted! Unakuwa hujatenda Haki.
 
Leo nimebahatisha kukutana na thread maridhawa, sawasawa na zilizokuwa zikitolewa na gt's siku za mwanzo mwanzo za kuasisiwa jf.
Hii hoja ya moto hakika imetoka kwa mtu makini, msomi na anayejitambua.
Hongera kuibuka ulikotoka na kuja kuwashika jf.
Mtu yeyote anayewaza bila kutumia u-chama, ufusadi na ukabila, hoja yako hii lazima imbambe.
Hoja nyingi zinazotolewa jf sasa hivi ni za mfano wa mashabiki wa mpira uwanjani zichezapo timu hasimu, kutafuta visingizio vya kukataa goli la wazi.
Yaani kuzomea na kukataa jambo la wazi na haki, kisa ni wa upande kinzani!
Mkipatikana watu mfano wako zaidi ya wawili na mkadumbukiza hoja zenu za kujenga namna hii mara kwa mara, hakika tafakuri katika jf zaweza badilika pakubwa na pakawa ni mahali pa kubadilishana mawazo na hoja mbalimbali kama zamani.
Mchango wako kwa hakika nimeupenda, ni wa kujenga.
 
Tundu Lisu katika hoja ametolewa kama mfano tu na muandishi kaweka hilo angalizo.
Maana yake ni kwamba tuache kujenga imani kwa wanasiasa 100%.
Lakini hata katika hali halisi Tundu Lisu alituaminisha kuwa Lowasa fisadi, lakini kalipoenda kakarudi akaja na hoja kuwa Lowasa siyo fisadi!
Mdomo mmoja hoja mbili kinzani, tena kutoka kwa wakili msomi!
Akiyatamka hayo yote ya kuchefua bila hata kuwa na kilevi chochote kichwani mwake, yaani macho makavu!
Utasemaje anaaminika na kwamba kumtolea mfano wa watu vizabizabina wanaoweza kugeuka muda wowote bila kujali maumivu ya mashabiki zao walowaamini kwa 100% ni kutomtendea haki?
 

Nimeona Hoja hapo! Bravo! Brother. Lakini hata katika hali halisi Tundu Lisu alituaminisha kuwa Lowasa fisadi, lakini kalipoenda kakarudi akaja na hoja kuwa Lowasa siyo fisadi!
 
Vichwa vyenyewe hivi masiponji na bado unaleta mambo magumu hivi, watakuelewa lini hawa? Kwani za mavideo kwiini hamna?
Jukumu letu kuwabadilisha mindset hawa watanganyika. Siye tuandike sana humu. Jukwaa limekosa hoja hili kuna wapingaji na wasifiaji. Namalizia kuwashauri wasifiaji
 
Jukumu letu kuwabadilisha mindset hawa watanganyika. Siye tuandike sana humu. Jukwaa limekosa hoja hili kuna wapingaji na wasifiaji. Namalizia kuwashauri wasifiaji
Sio watanganyika peke yao brother hata ndugu zangu wa kule visiwani nao hawana tofauti sana. Kibaya zaidi kule kuna siasa za chuki na visasi, hata ukiwapa hoja zilizowazi watu hawana mda wa kufukiria. Vijana tunaendeshwa na mihemko na ushabiki wa kisiasa bila kuelewa na kuangalia faida au hasara yake katika maisha yetu binafsi

[emoji252]You get what you work for not What you wish for [emoji252]
 
Nimependeza sana signature yako..
 
Nimependeza sana signature yako..
Ahsante mkuu.
Huu ni ukumbusho ili vijana tuache kulalama katika mambo yanayotuhusu.

[emoji252]You get what you work for not What you wish for [emoji252]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…