Ikifika 2025, Utajisikiaje ukijua kumbe Lissu naye ni Askari (planted)

Ikifika 2025, Utajisikiaje ukijua kumbe Lissu naye ni Askari (planted)

Why 2025 not now? Kwanini awe planted askari not other positions. Japo umeacha discuss open lakini ungeanza na kilichokusukuma.
 
Unajaribu kusema nini? Lisu,Lowasa,Sumaye, Magufuli,makamba,Rostam Mo etc ....................Binafsi naona unaweweseka ndio maana hutulii katika hoja na unajaribu kutuaminisha kuwa wewe ni smart sana kwa hiyo hutaki kushughulika na siasa bora ukashughulika na kina Rostam.Angalia maisha katika upana wake utagundua kila kitu hutokea kwa sababu.
 
Sasa ndo tunasubiri tuone askari wakiwakamata waliompiga risasi askari mwenzao
 
"I DON'T TRUST ANYONE EXCEPT THE DEAD ONE, BECAUSE THE DEAD ONE WILL NEVER BETRAY ME"

Kwahiyo hata wewe uliyeandika Uzi huu siwezi kukuamini kwa hichi ulichokiandika..
 
Tatzo humu ndan kuna watu wanajikuta wajuaji hafu wengine wanapenda kukaza ubongo yaaaniii MTU utakuta katoa fact ye atapinga tuuuuu huo ni ujinga na upuuzi sijamtaja mtu

usisahau vya kusahau kabla kusahau hAkujakusahau wewe uliye sahau
 
Boss chipa GM Wapinzani wengi wametokea Serikalini au CCM. Wachache sana ndio hawajatokea huko.

So swali lako, sisi Wananchi haijalishi 2020 tukute Mh. Lissu ni Askari aka MwanaUsalama. Kikubwa tunataka Mtu atakayesimama na Wananchi. Tunataka Mtu atakayetusikiliza. Tunataka Mtu atakayefuata Katiba na Sheria za Nchi.

So far ni Mh. Lissu pekee aliyeonyesha kutokuogopa. Ndie mwiba wa sasa kwa Serikali na CCM. Ndio karata turufu ya Wapinzani.


Mungu asante sana kwa utukufu wako na uhai unaotupa watoto wako.

'Acha kulalamika, umechelewa, muda haukungoji, majadiliano ya siasa huleta uchomvu wa akili na upofu wa fursa'


Nilikuwa nawaza kwa sauti kubwa sana Leo asubuhi. Ivi ilikuwaje maadui wawili wa muongo mmoja ( lowasa na Sumaye) kupatana ndani ya wiki moja na kuhamia chadema? Tunajua kabsa Lowasa alikuwa anautaka Urais, lakin swali la kujiuliza Lowasa alikuwa hajui hawez kuwa Rais wa Nchi bila tume huru ya Uchaguzi.

Na Sumaye alikatwa kwenye kura za maoni. Kilichompeleka Sumaye Chadema ni nini? Yaani Sumaye amfate adui yake wa siku nyingi Upinzani. Sisi wadaganyika tukafurahia kuwa two retired senior government officers ktk chama chetu. what happened? tukaaminishwa uchaguzi tulishinda, vijana wakawa tayari, tukaambiwa tusubili kwanza viongozi wa chama wanaenda kushitaki ughaibuni ( wajanja tukajua shughuli imeisha..na kweli imeisha), kule Zanzibar Seif akaanza kuzunguka zunguka mara BBC,CNN, mara UN. SEIF AKASEMA MIPANGO INAANDALIWA YA YEYE KUPEWA HAKI YA KUWA RAIS WA ZANZIBAR, Mtu anapewa urais wa mezani..Kama Simba tu point za mezani TFF walikataa kuwapa sembuse Urais, shughuli nayo ikaishia hapo.

tukaambiwa elimu elimu elimu (Mission done)

'Acha kulalamika, umechelewa, muda haukungoji, majadiliano ya siasa huleta uchomvu wa akili na upofu wa fursa
'

Kila MTU alimuamini sana Dr. Slaa. Tunajua kilichotokea. Wengi tuliamini mzee slaa hakuwa na bei. Hayo ni 2015.

Tu project 2025. Itakuwaje kumbe na huyu tunaye muabudu sana kwa sasa kumbe naye planted. Tutajisikiaje wana mabadiliko tukiona huyu mwanasheria wetu nguli kumbe ni planted. Sahau kuhusu rasha rasha za mahabusu na mahakamani. Hizo n njia za kumuaandaa mtu awe relevant na aminike sana.

Ushauri:

1- vijana tunalaumu sana na kuponda kila kitu.

Mfano mdogo, Serikali inakusanya only 1.1 trillion kwa mwezi. Mishahara kwa watumishi wa umma ni 570 bilioni. Inayobaki ni 530 bilioni. Ebu inyambue hiyo pesa kwa matumizi ya mwezi kwa serikali alafu uone kwann Magu anakuwa mkali sana. Najua kuna Grants na Loan but upatikanaji wako siyo reliable sana.

2- Vijana tuache kujadili pet issues ambazo hazisaidii jamii yetu.
Mfano: kwenye tukio la bomba la mafuta vijana tumejikita kujadili Ruge na Makonda badala ya fursa iliyopo kwenye bomba hilo individually na Nchi pia. Nilitegemea vijana tujikite kujadili jins gani tupata ajira hapo na jins gani tutaenda kuuza vitu kwenye mradi huo. Tegemea mradi huu utawanufaisha sana wakenya na waganda.
Kuna kipind mitandao ili jam kwa habari za Bashite..kila mtu bashite..nikawa najiuliza ni kukosa kazi au watanzania tuna upeo mdogo sana wa kung'amua mambo.

3- mwisho, Magufuli ndiyo Rais, ndiyo Baba. Kila mtu acheze ngoma yake, yeye ndiyo the most powerful man kwa Ardhi yetu ya Tanzania. Yeye ndiye namba moja. Hata akiwa angani, anga lote linajua namba 1 yupo angani. Ana mazuri yake na anaubaya wake. Hatukuchagua malaika atuongoze.

Cha msingi tushauri, tukosoe but tusikebehi, tusitukane MTU...vision ya Namba 1 kasema Nchi ya viwanda. Jukumu letu wananchi ni kushauri vipambaule viwe wapi kwenye viwanda..mfano kilimo, uvuvi n.k. Serikali IPO pale kukuwezesha tu kufanikiwa siyo kukupa mtaji na pesa za kuishi. Nilimsikia waziri wa kilimo akisema China kuna soko kubwa sana la mihogo, hizi ndizo information ambazo zinatusaidia wananchi siyo za makonda na Ruge.

Vijana tumekuwa wajuaji na wakosoaji sana. Tunasema huyu wa sasa ni dikteta, kwani mauaji ya Arusha ambayo lema alisema anayo video, Singida na Morogoro yalitokea kipind gani. Kwan Ulimboka, kibanda walitekwa kipind gani?
Unakumbuka suala la Mwangosi limetokea kipindi gani? Kipindi cha Mkapa na Vurugu mwembechai ( masuala ya kiimani) au awamu ya 3; na vurugu za uchaguzi Zanzibar?.

Bila kubadili mindset zetu hata chadema waje watawale hatutakuwa na maendeleo. Tuwe logic oriented na siyo emotional.

2025; utajisikiaje moyoni kama kamanda lisu kumbe naye alikuwa planted. Who know? Unajua historia Lisu vizuri. Huu ushauri kwa vijana wenzangu wa Ukawa. Next time ntawashauri vijana wa Lumumba. Pambana na hali yako. wenzetu wakina Lema wanalipwa kwa kazi hiyo. Sisi bado maskini sana hatuwezi kufika uchumi kati ikiwa wengi tunaishi mlo mmoja. serikali ni kama mwalimu darasani, mwalimu anajikumu la kufundisha tu suala la kufaulu mitihani ya necta ni jukumu la kwako wewe, wewe unajukumu la kusoma tuition, kukesha. Serikali ina jukumu la kuhakikishia miundombinu ya kiuchumi na kijamii inakuwepo, sisi wana Nchi tunajukumu la kutumia fursa za kimiundombinu kupambana na hali yetu.

Kuwafanya sana wakina Lisu, Lema, Zito, Mbowe, Sugu ( wakina makamba, POLEPOLE siwataji leo, ntawataja kwenye ushauri wa Lumumba) ndiyo ma model wetu tunapoteza na muda na tutakuwa maskini wa akili na mali. tunafatilia maisha ya wanasiasa ambayo hayatusaidii. Leo Nape tulimiwita Vuvuzela Kisa katofautiana na Bosi wake leo amekuwa na yeye Kamanda. are we serious?

Ali Mufuruki, Rostam, Said Bahkressa, Mo dewji, Manji, Mengi hawa ni watanzania ambao tunabidi tuwafanye wawe ma model wetu na mijadala yetu ijikite kwao kwa jinsi gani wameweza kuwa matajiri Tanzania. Mfano umeona Tanzania hakuna ajira, je umeshwahi kufikiria kutafuta Kazi Nchi za Jirani;; kwann wakenya wapo Tanzania na sisi hatwendi Nchi zao. Biashara ngumu Tanzania mfano umeshawahi kusoma demand ya malawi wananunua vitu gani ambavyo kwa mtaji wako wa milioni 5 waweze supply. Au story nzuri ni zile Lisu amjibu Magufuli..Au daimond afumaniwa. We are not cheap to that.

'Acha kulalamika, umechelewa, muda haukungoji, majadiliano ya siasa huleta uchomvu wa akili na upofu wa fursa'

pambana na hali yako.

Sijasema Lisu ni Askari but utajisikiaje kumbe ni planted; usiamini MTU. Trust No Body.
Binafsi nampenda sana Lieu kwa anavyochallenge serikali..sijamuona mwana ccm anayeweza kumjibu..



Mungu asante kwa utukufu wako, Bongo siyo bahati mbaya.
 
Mkuu uliona mbali....

Kauli ya Rais juzi akipokea makinikia inanifikirisha sana... Juu ya kupandikiza askari upande wa maadui na akasisitiza wakijulikana wanuawa..

Akajitapa kuwa na taarifa zote...akatuonyesha na flash..

Kumbe huku wanaume wanaload risasi.

... Wacha tuendelee kusubiri.

BTW Lowassa kashaongea kitu!!?
 
Hao mnaowadhania kuwa ni planted mmejiridhisha kweli kuwa ni planted au ndio kila linalosemwa ndilo hata kama ni la kufichiana aibu na kuzuga watu kama wewe mleta mada
 
Ukweli hua mgumu kuupokea kwa mara ya kwanza. Ila ukikaa na kuufikiria taratibu utakuingia tu.

[emoji252]You get what you work for not What you wish for [emoji252]


wataupokea taratibu tu..
 
Back
Top Bottom