KERO Ikifika jioni Daladala za Mwenge–Bunju zinaishia Tegeta kisha zinatoza tena nauli ya Tegeta Bunju

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nina hoja kuhusu baadhi ya daladala zinazofanya safari kati ya Mwenge na Bunju, hasa nyakati za jioni. Kuna baadhi ya magari ambayo yamekuwa na utaratibu wa kuwatangazia abiria kuwa yanaishia Tegeta, hivyo abiria wanaosafiri hadi Tegeta hushuka hapo.

Pia soma ~ LATRA: Tumeanza kufunga ving'amuzi vya VTS kufuatilia Daladala zinazokatisha ruti na kuzidisha nauli

Baada ya abiria wa Tegeta kushuka, magari hayo huanza tena kupakia abiria wengine wanaokwenda Bunju, hali inayofanya safari moja kugeuka kuwa kama safari mbili. Abiria wanaolipia nauli ya kwenda Bunju wanaonekana kuathirika kwa sababu wanakuwa wameshalipa lakini wanalazimika kubadilishiwa utaratibu wa safari.

Tunaomba mamlaka zinazohusika na usafiri wa umma hasa LATRA na Askari wa Usalama Barabarani kufuatilia suala hili na kuhakikisha abiria wanapata huduma inayolingana na nauli wanazolipa. Kama gari limepewa kibali cha kufanya safari ya Mwenge–Bunju, ni muhimu kufuata utaratibu huo na kuepuka vitendo vinavyoweza kuwaumiza wananchi.

Soma pia:
 
Mamlaka zinajua kupandisha tu mapato ya kwenye mafuta, hiyo kazi yenu raia kama mnaweza pambaneni nalo
 
Mkuu kuna watu watakuja kukuambia hapa kwann usipambane ununue usafiri wako uachane na hiyo adha ya kugombana na ma konda wa daladala
 
Na nauli inalipwa ya Tegeta au ya Bunju?

Mwendokasi ikiwa introduced tutashirikiana nao kujenga nao hoja ya kwanini waachwe kusaidia usafiri

Ila muda huu wanaleta uzenge.
 
Hilo ndio tatizo la Dar pote. Halafu kuna inteligensi ya serikali kutatua kero za wananchi
 
Naunga mkono hoja, hali ni hiyohiyo kwa njia za kawe kuelekea Gongo la mboto na Buza, hasahasa siku za ibada za Mwamposa gari zinapakiwa Kawe Magomeni Kanisani mwisho, halafu zinajeuka au zinaenda kunza upya pale studio. LATRA kama kawaida yao wako busy kukatiwa ticket za ndege kuhudhiria vikao na warsha mbalimbali as long as tozo na faini zinatuna kwenye account zao abiria watajijua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…