Ikitokea dada yangu na kaka yangu wamesalitiwa na wenza wao nitamuonea huruma zaidi kaka yangu kuliko dada

prida

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2026
Posts
1,297
Reaction score
2,596
.

Leo ngojea nijaribu kuandika kwa kifupi.

Kaka zangu,kama una mke/familia ambae unampenda,unamjali na kumlinda kwa namna zote zinazomaanishwa na haya maneno na ikiwa kula yake,mavazi yake,malazi yake na huduma zote anazohitaji binadamu anazipata kutoka kwako halafu ikatokea mke huyu akachit piga chini mshenzi huyo ambae biblia imemuita mpumbavu kisha tafuta mwanamwali mpya atakayethamini mateso na stress unazopitia ili yeye/na watoto aishi vizuri kisha uweke ndani.

Wamama wenzangu,kama mumeo ni kama huyo niliyemuelezea hapo juu imetokea akachit USIMUACHEπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ.πŸƒβ€β™‚οΈβ€βž‘οΈπŸƒβ€β™‚οΈβ€βž‘οΈπŸƒβ€β™‚οΈβ€.
Kama unataka kuwa yule mwanamke mpumbavu anayeongelewa kwa biblia muache ila kama hutaki .mpe jamba jamba za moto ili asirudie tena na hakikisha haiwi tabia yake ila usimuache.

Kaka yangu akisalitiwa nitamchukia huyo wifi na roho itaniuma sana kila nikiwaza kaka yangu anateseka/jinyima ajili yake halafu shukrani ya kukunawirisha ukapendeza ni kumsaliti?!No way.

Ila πŸ˜ƒπŸ˜ƒkama shemeji kakamatwa na kamchepuko ila hakuna kilichopungua pale nyumbani kwao nitamshauri sista aongee vizuri na mumewe aache hiyo tabia asije akamletea maradhi ila sitamchukia shemeji yangu.

Kama mwanamke wewe ndo unahudumia huyo baba au wewe baba ndo unahudumiwa hiyo ni kesi nyingine ila kwa maisha ya kawaida ambayo wanaume ndio wamebeba mzigo wa kuhudumia, mtazamo wangu ndio huu.

Namaanisha mwanaume akisalitiwa anaumia zaidi kuliko mwanamkeπŸ˜ƒ.Na mwanamke ukitaka kushindana na mwanaume kwenye ishu za usaliti sijui kachit na mim namlipa kwa kumchit au usikie wanaume wanasema msaliti hasamehewi na wewe mumeo akuchit ujitie msaliti asamehewi ondoka.

Nb:Kiranga alivyoona naongelea sana haya mambo akauliza kama nimewekeza hata kwenye hisa nikamdanganya ndio nimewekeza kwenye hisa na sehemu nyingine nyingi ila ukweli ni kwamba sijawekeza popote zaidi ya kwenye ndoa yangu.Mimi productive day yangu inajumuisha kufua boxer za mume wangu,kubuni mapishi mapya na kujiremba ili kila jion akirud anikute ninavotia.
 
Kazia hapo kwenye productive day ya mke anayejielewa inakuwaje
Inajazwa na matendo yenye kuashiria utii kwa mume wake.Chochote kinachokinzana na utii kwa mume hakipaswi kuwepo kwenye ratiba ya siku.Najua watu wananiona kichaa,desparate,sijui thamani yangu n.k lkn ukweli ni kwamba kama utamaduni wa dunia ktk mahusiano ungekua ule ambao biblia inautaka,wa mwanamke kuwa na jukumu moja tu,kutii mume wake na mwanaume kama ataweza kupenda kama biblia inavyotaka naamini maisha yasingekua na stress tulizonazo leo.

Ndoa za leo zina stress sbb hatusimami kwenye nafasi zetu.Hajulikani mwanamke nani mwanaume nani.Wote tunapambania kiti cha kiume.
 
Prida kuna muda unakwama pabaya, unatupa vibe ya pick me fulani hivi. (Mwanamke anayeshusha vigezo ili iwe rahisi kuchaguliwa) Aina ya wanawake ambao mnawaweka wanaume juu mnawakandamiza wanawake wenzenu chini.

Maumivu ya usaliti kwa watu wenye commitment ni yale yale kwa KE au ME,

Out here, wanawake wengi ni kama mmechanganyikiwa kwa kusalitiwa kila siku na kusamehe/kupotezea.

Usaliti una destroy a soul.

Usaliti una sababisha insecurities, ndio maana wengi mnachukia wanawake wenzenu sababu the moment mkisalitiwa mnaanza kujiuliza huyu ana nini, mimi sina nini.

Usaliti unaleta magonjwa ya ngono ndani ya ndoa, hakuna exception kwamba mmoja ataleta magonjwa mwingine hataleta.

There’s no better!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…