Ikitokea Ghafla Ukakutana na Mh Raisi Magufuli

Nitamuulza Mzee "kwa nini unapenda kukurupuka"
 
ntamwambia aliowatumbua ni wachache safari hii atumie panga kutumbua mpaka tunyooke.pia ntamwambia abadili katiba atawale mpaka 2045 kwani sasa ndiyo tunaye rais.pia waficha sukari wanyongwe kwa kuhujumu uchumi
 
Mie ningemwambia afanye maamuzi haraka ya kwenda kuchunga ndege maana anakoipeleka Tanzania siko ni majanga matupu. Akachunge ndege salama badala ya kuendelea kuiangamiza nchi yeu na kupandikiza chuki za kutisha kwa udikteta wake na sera za kukurupuka.
 
La kumshauri papo kwa papo sinalo mana hata nikimshauri sidhani kama hata atashaurika,sanasana ntamuomba selfie moja chapchaap km basi la mwendokasi
 
Mimi ningemshauri arudie zile pushapu alizokuwa anapiga wakati wa kampeni zina maslai kwa sasa. Wakati tunafuturu uji usio na sukari ?
 
Ntamwambia arudie lile tangazo la TRA la kutoa kodi, maana alichapia, " UKIEMBA DUKANII" aseme "UKIENDA DUKANI"
 
1) Ilikuwaje Jeska alifika chuo kikuu?
2) ulisema Hapa Kazi tu mbona sijapata hio kazi mpaka leo.
3) Najua wakati wa kampeni uliogopa kupanda chopa sasa na ndege pia unaiogopa?

Kwani chopa sio ndege?
 
Maswali yoote hayo alishauliza na ushauri woote alishapewa hata leo maaskofu wamemshauri tena. Btw Baba Jesca hajui msimamo wa kanisa katoliki kuhusu ulokole? Kitendo cha kutoka kusali kwa paroko halafu ukaenda kwa upako hakikuwa poa kwa kanisa. Wameshamdiss
 
Mimi ningemshauri ili kuleta tija, mashirika yanayofanya kazi zinazofanana yaunganishwe; mfano Ngorongoro na TANAPA ziwe shirika moja, Vyuo vya ufundi kama Mbeya, Arusha, DIT viwe taasisi moja; Mweka Wildlife na Pansiansi viwe taasisi moja; na mengineyo mengi
 
Ningemshauri aimarishe kilimo sayansi na technologia ndio tuanze viwanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…