Hii sekta ikiwekwa vizuri inaweza pia kuingiza pesa nyingi katika nchi na pia ni heritage ya watanzania. Tanzania ni nchi ya pekee sana katika utajiri wa mali asili na culture mpaka tupo kwenye world wonders kuu za dunia.
Tatizo utawala wake una miaka zaidi ya 16 sasa, madirector hawabadilishwi, sekta ya mali asili na sekta ya makumbusho hazina ushirikiano, tafiti za mambo kale hazipewi kipaumbele, ajira kwa vijana wa mali asili na mambo kale ni ndogo, miradi ya makumbusho kuu za Ngorongoro pesa zinachezewa, kila mkoa ulipaswa kuwa na nyumba ya makumbusho kuonyesha uhifadhi wa mali asili na mambo kale yake kwa kila mwananchi na wageni kuona na kujifunza, sylabus ya History haijabadilishwa kuendana na tafiti za sasa, wanyama wanasafirishwa, kampuni zilizokatazwa kuwinda wanyama katika nchi za Africa huku kwetu Tanzania bado wanaendelea kuwinda na kuna videos youtube wanashare ujinga wao, n.k