GTs,
Nimekuwa kimya sana kwa sababu nililamba uteuzi, na mimi sasa nafaidi keki ya taifa, tusisumbuane.
Kwa kilichotokea kwa ndugu yetu Ndejembi, ina maana kamati kuu ya CCM inaweza kukutana na kama koramu ikikamilika basi wanaweza kumfuta Dkt Samia uanachama wa CCM na hatimaye kupoteza urais na CCM inaweza pendekeza rais mwingine na Bunge kumpitisha kwa kumpigia Kura za ndiyo 100%.
Nilichojifunza kumbe inawezekana.
Yaani wanasubiri kasafiri then anayekaimu uenyekiti anaitisha fasta kamati kuu ya CCM wanamvua uanachama baada ya hapo bungeni fasta linapelekwa jina la rais mpya.
Naomba Mungu isitokee maana tuliokwenye mfumo wa Dkt Samia tunafaidi sana na hali ni nzuri mno.