GE2025 Ikitokea kesi ikafutwa sababu ya ushahidi dhaifu au kwa kubambikiwa, haki ya mtuhumiwa inarejeshwaje?

GE2025 Ikitokea kesi ikafutwa sababu ya ushahidi dhaifu au kwa kubambikiwa, haki ya mtuhumiwa inarejeshwaje?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Blessed Tajiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2023
Posts
284
Reaction score
870
Kuna msemo unasema 'Justice delayed is justice denied' na huu ndio uhalisia unaojitokeza kwenye mifumo yetu ya Haki Jinai.

Mtu anakamatwa, anafunguliwa kesi, lakini upelelezi haujakamilika—maombi ya muda yanaendelea. Shauri likifika mahakamani, bado upande wa mashitaka unaomba muda zaidi, au tathmini mpya inafanyika kabla ya kuamua kuendelea au kufuta kesi.

Hali hii inaacha taswira gani kwa wananchi? Inajenga au inavunja imani kwenye mfumo wa haki?

Kama kesi ikifutwa kesho kwa sababu ya ushahidi dhaifu au kubambikiziwa, haki ya mtuhumiwa inarejeshwaje?

Kuna tofauti kubwa kati ya mahakama kumwachia mtu baada ya kusikiliza kesi na DPP kuamua kufuta mashtaka. Hili pamoja na tabia ya Polisi na waendesha mashitaka kushughulikia kesi zenye mapungufu ya kisheria ni uvunjaji wa haki za binadamu.

Wengine walilazimishwa plea bargain ili serikali ifichw aibu (au uovu) ya kushindwa kesi. Hii siyo haki.

Kabla ya 4Rs kupata heshima ya kweli, mfumo wa Haki Jinai unahitaji kurekebishwa haraka. Hili ni jambo linaloewela pamoja na kuheshimu misingi ya haki.
 
Kuchelewesha kwa haki ni sawa na kumnyima haki Lissu. Mfumo unahitaji marekebisho ya haraka ili kuzingatia misingi ya haki na utawala wa sheria.
 
Back
Top Bottom