Ikitokea umekutana na mtu aliyepotea, mwenye tatizo la afya ya akili; utamsaidiaje ili kuwapata ndugu zake?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kuna video clip huwa zinasambazwa zenye kuonesha watu wenye matatizo ya akili ambao wamepotea au kutojielewa kwa wakati huo. Video hizo huonesha mahojiano kati ya mwenye tatizo na mchukua video.

Je, ni sahihi kufanya hivyo?
Je, ikitokea sasa mwenye hili tatizo akawa sawa, na kuiona video hiyo haitamsababishia msongo wa mawazo?
Tusaidiane mawazo ya namna ya kuwasaidia watu wa hali kama hizo.
Cc: Dkt. Gwajima D
 
Vipi, hakuna mrejesho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…