Ikitokea umepata milioni 100, utaifanyia nini?

Ikitokea umepata milioni 100, utaifanyia nini?

Naenda salon najiweka sawa kila mahali, natoka hapo naingia gym after gym nafanya full body scub and full body massage without happy ending😜

naingia sauna na steam bath...
Nikitoka hapo naenda 5star Hotel...nqpiga simu maduka ya nguo kali na viatu waje waniletee hapo nifanye shopping nikiwa hapo hotelini....

Nikishaoga na kupendeza naenda kupata dinner pamoja na wine expensive kuliko zote inayopatikana hapo....

Narudi zangu room narelax kitandani nikiperuzi jf kuwasoma watu wenye shida zao nikiwafariji na kuwapa pole.

Kesho yake natafuta financial advisor aje tuongee....
Kesho yake zitakuwa zimebaki ngapi?
 
Habari wana jamvi, poleni kwa harakati za hapa na pale. Kwa wanaoteswa na MAPENZI hii pole haiwahusu, wanawake wapo 31M wanaume 30M iweje uteswe na mtu mmoja?

Nirudi kwenye lengo husika la huu uzi

Niliwahi kushuhudia watu fulani wakizozana, mada ilikuwa "Ukipata 100M utaifanyia nini?" Mmoja akasema nitajenga nyumba nzuri nikae na familia yangu, mwengine akasema nitatafuta namna ya kuzungusha hio pesa. Mzozo ukaanzia hapo...

Wa kujenga nyumba anamuona mwenzake hana akili na wakuzungusha pesa anamuona mwenzake Mirembe day scholar. Kila mtu alikuwa na hoja zake na zina mashiko kwa kila mmoja.

Kwa kawaida mizozo/mijadala ya namna hii inafanywa na watu masikini pengine hawana hata 1M lakini ni mijadala mizuri sana. Kwani inajenga na inapanua ubongo namna ya kufikiria linapokuja swala la pesa. Binafsi nilijifunza mambo mengi sana siku hiyo.

Ni siku ambayo kwa kweli niliifurahia na nilipata kitu kipya. Ni siku ilijiyojenga misingi mipya linapokuja swala la fedha, ni siku iliyonipa mtazamo mpya na positive.

Vipi wewe ndugu yangu... "UKIPATA MILLIONI 100 LEO UTAIFANYIA NINI? UTAJENGA AU UTAIZUNGUSHA?"

Usijiulize hiyo 100M utaipataje.. mambo yatakuwa mengi[emoji23][emoji23] wewe anza kufikiria ushaipata kwa namna yoyote ile tayari upo nayo hapo. Tupe mawazo yako

KAMA UTAJENGA: utajenga nyumba ya gharama kiasi gani? Utajengea yote? Je kiwanja unacho au hiyo hiyo utanunulia kiwanja?

KAMA UTAIZUNGUSHA: Utaizungusha kwa misingi gani? Utaanzisha biashara ipi? Ni biashara moja au biashara mbali mbali? Utaitumia pesa yote kwenye biashara? Utaanzisha biashara mpya au unayo biashara utakayoiendeleza?

KARIBUNI
Nachukua nyumba ya kupangisha vyumba visivyopungua 10 kila chumba kilete kodi ya shilingi elf 40.kwa vyumba kumi nina laki 4.
gharama ya hyo nyumba milioni 20 isizidi.

natafuta nyumba ya kuishi isiyozidi milioni 20.
natafuta shule ya primary nawekeza kuuza pipi na vitu mbali mbali vya watoto kwa milioni 5.
milioni 5 zinakaa kwa emergency.

50 milioni zinazobaki naweka fixed ambayo napata riba ya kutosha kwenye bank yyte ambayo kwa mwezi si chini ya laki tano kama faida kwa fixed deposite.

Faida baada ta uwekezaji.

1. 400,000/= kodi kwa mwezi.
2.450,000/= faida ya duka shule
3.500,000/= faida fixed deposite.

Total faida kwa mwezi. 1,350,000/= kwa miaka 2. unapata milioni 32,400,000/=
unakuwa umerudisha hela ya nyumba ya kuishi. na faida milioni 12,400,000/=

chukua milioni 2,409,000/= weka mfukoni.
milioni 10,000,000/= na zile 20. zirudishe bank Jumla unakuwa na milioni
80.

vumilia tena miaka 2.
unapata tena milioni 32,400,000/=
rudisha bank milioni 30. weka mfukoni milioni 2 laki 4.

Total amount unayo sasa milioni
110,000,000/=
kwa uvumilivu wa miaka isiyopungua mitano.

Uvumilivu na comitment itakutoa.

Ila kwa vile hutaweza kuvumilia peleka kwa wadada wataila kwa muda wa siku 10 tu.
 
Nitaziweka mezani na kuziangalia tu daily huku nakunywa maji.Pesa ikiwepo hata ukilalia ndizi choma lakini IPO bas unajinenepea tu
 
Nanunua Ng'ombe
Nafungua Bucha
Nauza Maziwa
Nauza Nyama
Nauza Supu ya Kongolo na Mkia

Nanunua Kitimoto wa Kutosha
Natotolesha
Nafungua Bucha
Nauza nyama
Nawauzia na Ndizi 2

Piga pesa baada ya mwaka nmezalisha milioni 300 kutoka kwenye million 100

Hivyo ndio vipaumbele vyangu,
Sio rahisi hivyo..kila mtu mfuga ng'ombe na nguruwe angekua tajiri.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nachukua nyumba ya kupangisha vyumba visivyopungua 10 kila chumba kilete kodi ya shilingi elf 40.kwa vyumba kumi nina laki 4.
gharama ya hyo nyumba milioni 20 isizidi.

natafuta nyumba ya kuishi isiyozidi milioni 20.
natafuta shule ya primary nawekeza kuuza pipi na vitu mbali mbali vya watoto kwa milioni 5.
milioni 5 zinakaa kwa emergency.

50 milioni zinazobaki naweka fixed ambayo napata riba ya kutosha kwenye bank yyte ambayo kwa mwezi si chini ya laki tano kama faida kwa fixed deposite.

Faida baada ta uwekezaji.

1. 400,000/= kodi kwa mwezi.
2.450,000/= faida ya duka shule
3.500,000/= faida fixed deposite.

Total faida kwa mwezi. 1,350,000/= kwa miaka 2. unapata milioni 32,400,000/=
unakuwa umerudisha hela ya nyumba ya kuishi. na faida milioni 12,400,000/=

chukua milioni 2,409,000/= weka mfukoni.
milioni 10,000,000/= na zile 20. zirudishe bank Jumla unakuwa na milioni
80.

vumilia tena miaka 2.
unapata tena milioni 32,400,000/=
rudisha bank milioni 30. weka mfukoni milioni 2 laki 4.

Total amount unayo sasa milioni
110,000,000/=
kwa uvumilivu wa miaka isiyopungua mitano.

Uvumilivu na comitment itakutoa.

Ila kwa vile hutaweza kuvumilia peleka kwa wadada wataila kwa muda wa siku 10 tu.
Hesabu za Sadiki na Chitemo.
 
Epuka sana marafiki wanaodhani milioni 100 ni pesa nyingi [emoji276]
 
Mimi iyo 100M nitaponda raha Yote kwanza 30M nachukua zangu Harrier mpyaaa afu inabak 70M nachukua appartment ya gorofa ya 9M kwa mwaka nalpia miaka miwili 18M afu 2M nachukua pamba kali na bak na 50M iyo n ya kula raha miaka miwili kwa mwez nakula 2M miaka miwili 48M kwisha inabak 2M nauza harrier 20M najumlsha inakua 22 hapo narud zangu kijijini nikaendelee kuteseka tayar nmefuta mkosi nmejipa raha
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji28][emoji28]
 
Back
Top Bottom