Habari wana jamvi, poleni kwa harakati za hapa na pale. Kwa wanaoteswa na MAPENZI hii pole haiwahusu, wanawake wapo 31M wanaume 30M iweje uteswe na mtu mmoja?
Nirudi kwenye lengo husika la huu uzi
Niliwahi kushuhudia watu fulani wakizozana, mada ilikuwa "Ukipata 100M utaifanyia nini?" Mmoja akasema nitajenga nyumba nzuri nikae na familia yangu, mwengine akasema nitatafuta namna ya kuzungusha hio pesa. Mzozo ukaanzia hapo...
Wa kujenga nyumba anamuona mwenzake hana akili na wakuzungusha pesa anamuona mwenzake Mirembe day scholar. Kila mtu alikuwa na hoja zake na zina mashiko kwa kila mmoja.
Kwa kawaida mizozo/mijadala ya namna hii inafanywa na watu masikini pengine hawana hata 1M lakini ni mijadala mizuri sana. Kwani inajenga na inapanua ubongo namna ya kufikiria linapokuja swala la pesa. Binafsi nilijifunza mambo mengi sana siku hiyo.
Ni siku ambayo kwa kweli niliifurahia na nilipata kitu kipya. Ni siku ilijiyojenga misingi mipya linapokuja swala la fedha, ni siku iliyonipa mtazamo mpya na positive.
Vipi wewe ndugu yangu... "UKIPATA MILLIONI 100 LEO UTAIFANYIA NINI? UTAJENGA AU UTAIZUNGUSHA?"
Usijiulize hiyo 100M utaipataje.. mambo yatakuwa mengi[emoji23][emoji23] wewe anza kufikiria ushaipata kwa namna yoyote ile tayari upo nayo hapo. Tupe mawazo yako
KAMA UTAJENGA: utajenga nyumba ya gharama kiasi gani? Utajengea yote? Je kiwanja unacho au hiyo hiyo utanunulia kiwanja?
KAMA UTAIZUNGUSHA: Utaizungusha kwa misingi gani? Utaanzisha biashara ipi? Ni biashara moja au biashara mbali mbali? Utaitumia pesa yote kwenye biashara? Utaanzisha biashara mpya au unayo biashara utakayoiendeleza?
KARIBUNI
Nachukua nyumba ya kupangisha vyumba visivyopungua 10 kila chumba kilete kodi ya shilingi elf 40.kwa vyumba kumi nina laki 4.
gharama ya hyo nyumba milioni 20 isizidi.
natafuta nyumba ya kuishi isiyozidi milioni 20.
natafuta shule ya primary nawekeza kuuza pipi na vitu mbali mbali vya watoto kwa milioni 5.
milioni 5 zinakaa kwa emergency.
50 milioni zinazobaki naweka fixed ambayo napata riba ya kutosha kwenye bank yyte ambayo kwa mwezi si chini ya laki tano kama faida kwa fixed deposite.
Faida baada ta uwekezaji.
1. 400,000/= kodi kwa mwezi.
2.450,000/= faida ya duka shule
3.500,000/= faida fixed deposite.
Total faida kwa mwezi. 1,350,000/= kwa miaka 2. unapata milioni 32,400,000/=
unakuwa umerudisha hela ya nyumba ya kuishi. na faida milioni 12,400,000/=
chukua milioni 2,409,000/= weka mfukoni.
milioni 10,000,000/= na zile 20. zirudishe bank Jumla unakuwa na milioni
80.
vumilia tena miaka 2.
unapata tena milioni 32,400,000/=
rudisha bank milioni 30. weka mfukoni milioni 2 laki 4.
Total amount unayo sasa milioni
110,000,000/=
kwa uvumilivu wa miaka isiyopungua mitano.
Uvumilivu na comitment itakutoa.
Ila kwa vile hutaweza kuvumilia peleka kwa wadada wataila kwa muda wa siku 10 tu.