Salaam Wakuu,
Jana katika picha za Rais Samia na viongozi wa Yanga na Simba, Gharib alikuwepo kwa upande wa viongozi wa Yanga, sasa je, siku ikitokea Pamba, Singida, Mashujaa, Namungo na wenyewe wakiitwa huko Ikulu, GSM ataenda kama kiongozi wa hizo Timu?
Kama hatoenda, inakuwaje watu wanakubali udhamini wa vilabu vinane (8) vya Ligi Kuu na GSM ambaye ni kiongozi wa Yanga kwa ushahidi wa picha na press ya Ikulu kuwa Rais Samia amekutana na Viongozi wa Yanga & Simba?
Je, kama GSM ni kiongozi wa Yanga na wakati huo huo kupitia Kampuni ambayo yeye ni Mwenyekiti anadhamini vilabu vingine vya Ligi Kuu, hatuoni kuwa kuna uwwezekano wa Upangaji wa Matokeo kwa kupendelea Timu ambayo GSM ni kiongozi?
Swali la mwisho, kama GSM ameenda kama kiongozi wa Yanga kwa ushahidi wa picha, ana cheo gani pale Yanga?