Ikitokea Yanga kachukua kombe la Caf. Je, atashiriki klabu bingwa au atashiriki CAF ili kulitetea?

Mwanachama wa CAF ni Shirikisho la Soka la nchi na si klabu. Ukishakuelewa hilo utajua ni kwani mwaka ule Bakuli FC ya Mwinyi Zahera ilipotolewa na Lipuli ya Matola kwenye nusu fainali ya FA, Lipuli ilicheza fainali na Simba, Simba akawa bingwa wa nchi na FA Cup.
Simba akashiriki CAF CL, kwanini CAF CC jina halikupelekwa la Lipuli ambae ndio makamo bingwa wa FA na ndie alimtoa Yanga kwenye nusu fainali badala yake jina likapelekwa la YANGA ambae alikuwa makamo bingwa wa nchi.
Mashindano ya FA Cup yalitoa mwakilishi gani mwaka ule?
Tumia akili basi hata kwa 0.0000000000000001%
 
Nadhani wataangalia kwenye unafuu, (ni shirikisho) kule kwingine ni kwa wakubwa sio saizi Yao, [emoji15]. Japo hawatachukua Hilo kombe
Kwa Uto hii inavyopenda sifa, watahiyari wasitetee kombe lao waende huku kwenye hadhi kubwa zaidi, wakafyeke vichaka vya KUFA KIUME kwenye robo fainali.
 
Wewe bora ushabikie rede tu mpira kwako hamna kitu. Bingwa wa CAF shirikisho msimu uliopita ni Berkane je umemuona kwenye hayo mashindano?
 
Muuliza swali umeuliza swali zuri mno,ila ukitaka kuona JF ina wapumbavu wengi na wajinga wa kutosha nadhani komenti zimekuthibitishia hilo.

Mpaka sasa hakuna aliyejibu swali lako ila wengi wameonyesha namna walivyo wajinga vichwani.

JIBU.

Yanga anaendelea kushiriki kwenye michuano ya kombe la shirikisho(CAF CONFEDERATION CUP) na hivi sasa yupo hatua ya nusu fainali.

Endapo ikatokea akawa bingwa(Kama ndicho unachomaanisha),Je atashiriki mwaka unafuata kama bingwa mtetezi kwenye kombe hilohilo la shirikisho au atashiriki kwenye ligi ya mabingwa Afrika?

Hapa jibu ni Hili,Kama akiwa Bingwa wa ligi kuu ya Tanzania(Tayari ni Bingwa) basi moja kwa moja atashiriki kwenye hatua za mtoano au awali klabu bingwa Afrika ili aingie kwenye makundi,na endapo akifeli kwenye hatua za mtoano au awali basi atarudi kushiriki kwenye kombe la shirikisho kwenye hatua ya mtoano ili apate nafasi ya kupangwa kwenye makundi.
 
Kuna vilaza JF hudhani kushabikia mpira ndio kuwa na akili. Hadi sasa nilipofika sijaona jibu ila kazi kutukana, mara wengine wanasema mleta mada akashabikie rede, ubishi usio na majibu. Nikajua mnavyokuwa mnakabana koo kwa kushabikia hizo timu zenu basi mmeiva kwenye mpira kumbe mbumbumbu tu na nyinyi hamjui kitu ni kama mimi. Afadhali kwangu vitu nashabikia najua kuvielezea
 
Hapa sasa nimeelewa. Mashabiki wengi sana wa mpira wanakuwa na ubishi usio wa msingi, kutoa maelezo hawawezi. Hata kama mtu anatetea hoja haweki facts anaishia maneno ya uswahilini
 
Hawa Ndiyo utopolo Sasa, mazuzu ya hapo jangwani.

Kwamba hata MALIMAO FC anaweza akapendekezwa kwenda kucheza Cafcl. Kwamba CAF hawana kanuni. Tff Ndiyo wanaamua.

Tena unaandika kwa kujiamini kabisa.
 
Jamii Forum siku hizi bora ya Facebook
 
Naomba ufafanuzi juu ya Hilo.
We jamaa nadhani unazungumzia iwapo wakishinda confederation cup. Jibu ni kuwa Yanga wakiwa mabingwa wa hilo kombe watafuzu klabu bingwa moja kwa moja.

Yaani ni kama bingwa wa Europa hufuzu kwenda UCL.

Yanga wakitaka mwakani watetee hilo kombe la losers basi wakatolewe mtoano Champions League. Kinyume na hapo watakutana tuu na moto wa kweli kwa wakubwa ambako Simba huonesha ukubwa wake kila mwaka.

Hakuna janja janja kujibanzia kombe la futuhi hilo
 
Hawa Ndiyo utopolo Sasa, mazuzu ya hapo jangwani.

Kwamba hata MALIMAO FC anaweza akapendekezwa kwenda kucheza Cafcl. Kwamba CAF hawana kanuni. Tff Ndiyo wanaamua.

Tena unaandika kwa kujiamini kabisa.
Kuna msimu Egypt ligi haikuisha mapema na al ahaly hakuwa kwenye position ya kwenda club bingwa ila jina lake liliwasilishwa badala ya pyramids
 
We jamaa Huna ujualo kuhusu football yaani Hadi Aibu.. [emoji28]
 
Kwanza ieleweke kuwa Yanga sio kwamba anaenda kucheza champions league kwavile kabeba kombe la caf confederation cup, hapana Yanga atacheza klabu bingwa kutokana na nafasi aliyonayo kwenye ligi kuu ya NBC.

Kulingana na taratibu za CAF, kubeba kombe la CAF confederation, haikufanyi ucheze kombe la klabu bingwa bali kigezo kikubwa ni nafasi ya timu katika ligi kuu yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…