Ikiwa Israel ataendelea kufanya mashambulizi Gaza bila ukomo, ni kipi kitatokea

IIS

Member
Joined
Jun 11, 2024
Posts
89
Reaction score
171
Habari za wakati huu ndugu na jamaa popote mnakopatikana.

Leo baada ya kusoma habari ya vifo vya watu takribani 46 huko Gaza baada ya shambulizi la Israel kuna maswali nimejiuliza hapa ambayo ningependa kupata majibu kwa mwenye kujua.

Toka mwaka 2023 kumekuwa na mapigano kati ya jeshi la Israel na kikundi cha wanamgambo wa Hamas huko mashariki ya kati.Israel amekuwa na matumizi makubwa ya siraha nzito kwa lengo la kukomboa mateka ambao ni raia wa taifa lake na mataifa mengine pia.

Vita imeambatana na vifo vya raia wengi sana katika maeneo ya Gaza bila kikomo sasa.Swali langu ni je,Gaza inawakazi wangapi?(maana nikiangalia matukio mengi waliyoripoti aljazeera inaoneka vifo ni vingi sana)

Swali jingine ni hili,itatokea nini ikiwa Israel ataendelea kufanya mashambulizi kila wakati na kufanya mauaji?

Je,Hamas wakiachia mateka huu mzozo unaweza kuisha?

Ni hayo tu kwa leo.
 
Toka mimi nakua ni mwendo wa vita Kati ya Israel na upande wa Gaza,waache waendelee kudundana waki choka watapumzika,wakipata pumzi wanaendelea tena!!!
Sema hii naona inakuwa hatari kwa wakazi wa Gaza maana wanauliwa vibaya sana kwa kisingizio cha mateka
 
Dunia kuuuubwa namna hii, ikang'ang'anie mahala palipojaa matatizo kisa nini???
Yan just for ancestoral background reasons ndio watu wakomalie hapo gaza kwa gharama ya mauti yao na wapendwa wao??

Siwez fanya hio kitu.
 
Dah kwahiyo waondoke pale Gaza sio kiongozi
 
Mbona hiyo serikali ya CCM.imekuwa inawaua wananchi wanaohojia mambo yasiyikwenda sawa ndani ya nchi.?
 
  • Thanks
Reactions: IIS
Washaambiwa waachie mateka lakini hawataki ......wamebembelezwa sana kurudisha maiti lakini hawataki basi kifuatacho nadhani mnakijua ..........hakuna kuwaonea huruma ndio maana hata waarabu wenzao wako kimya ................rudisheni mateka wao mbona kama mnataka kutumia mabavu wakati hizo mbavu tu za kutunisha hamna basi wache wabondwe mpaka waishe............ na mimi nasapoti wapigwe tu sababu wanayo maiti ya mtanzania mpaka leo hawataki kuiachia mpaka wazazi wa yule kijana waliomba kwa hamas bado wamekaza fuvu......na mwisho tuangalie vita congo ........gaza mbali sana wana majirani zao kule sio nyinyi kobazi wa namabengo...........
 
Achieni watoto wa Wayahudi ili muishi kwa amani, mlichinja watoto wao huku mkiimba Allah Akbar ila msichokijua kabla ujio wa allah kulikua na miungu wengine waliojaribu kufuta Wayahudi kwenye ardhi yao ila wakashindwa akina miungu Baal wa wafilisiti.
Hao wote Baal, Allah, Krishna n.k. hawawezi kumzidi Mungu muumba wa Dunia, Jehovah Mungu aliyewabariki Israel tangu mwanzo.
 
NImeongea personally like mimi ningekua mkazi wa gaza. Nisingebaki hapo. Na nina amini kuwa waliondoka wakaangalie ustaarabu wa maisha mahala pengine.
Shida nani yuko tayari kukupokea ikiwa utaondoka pale? Na je maisha huko unakoenda itakuaje?
 
Mbona hiyo serikali ya CCM.imekuwa inawaua wananchi wanaohojia mambo yasiyikwenda sawa ndani ya nchi.?
Hii ya CCM ni mpya kiongozi lakini hapa najaribu kuwaza kama Israel ataendelea hivi Gaza si patabaki patupu
 
Achieni watoto wa Wayahudi ili muishi kwa amani, mlichinja watoto wao huku mkiimba Allah Akbar ila msichokijua kabla ujio wa allah kulikua na miungu wengine waliojaribu kufuta Wayahudi kwenye ardhi yao ila wakashindwa akina miungu Baal wa wafilisiti.
Hao wote Baal, Allah, Krishna n.k. hawawezi kumzidi Mungu muumba wa Dunia, Jehovah Mungu aliyewabariki Israel tangu mwanzo.
Lakini mateka wengine sio wayahudi kaka,kuna hadi mtanzania ambaye nadhani alipoteza maisha (RIP)
 
Washaambiwa waachie mateka lakini hawataki ......wamebembelezwa sana kurudisha maiti lakini hawataki basi kifuatacho nadhani mnakijua ..........hakuna kuwaonea huruma ndio maana hata waarabu wenzao wako kimya ................rudisheni mateka wao mbona kama mnataka kutumia mabavu wakati hizo mbavu tu za kutunisha hamna basi wache wabondwe mpaka waishe............ na mimi nasapoti wapigwe tu sababu wanayo maiti ya mtanzania mpaka leo hawataki kuiachia mpaka wazazi wa yule kijana waliomba kwa hamas bado wamekaza fuvu......na mwisho tuangalie vita congo ........gaza mbali sana wana majirani zao kule sio nyinyi kobazi wa namabengo...........
Kwahiyo mateka wakirejeshwa hii vita inaweza malizika sio
 
Hilo ndio jibu ambalo hao jamaa hawataki kusikia wanaona bora wafe tu
Basi watakuwa wanawasaliti ndugu zao wanaomalizwa na mashambulizi ya Israel kila siku.Hakuna logic yoyote ya kubaki na mateka huku maelfu ya jamaa zako wanamalizwa
 
Wewe jiulize maiti ya mtanzania inawasaidia nini mpaka leo wamegoma kuirudisha ...........hizo za Israel wacha wabaki nazo ya mtanzania inafanya nini kule???????
 
Toka mimi nakua ni mwendo wa vita Kati ya Israel na upande wa Gaza,waache waendelee kudundana waki choka watapumzika,wakipata pumzi wanaendelea tena!!!

Israel anataka wapalestina wakimbie Gaza, ili settlers wao wachukue ardhi.

Na dunia inaangalia tu. Kama hakuna kinachoendelea.

Kweli dunia hadaa na ulimwengu shujaa
 
Back
Top Bottom