Habari za wakati huu ndugu na jamaa popote mnakopatikana.
Leo baada ya kusoma habari ya vifo vya watu takribani 46 huko Gaza baada ya shambulizi la Israel kuna maswali nimejiuliza hapa ambayo ningependa kupata majibu kwa mwenye kujua.
Toka mwaka 2023 kumekuwa na mapigano kati ya jeshi la Israel na kikundi cha wanamgambo wa Hamas huko mashariki ya kati.Israel amekuwa na matumizi makubwa ya siraha nzito kwa lengo la kukomboa mateka ambao ni raia wa taifa lake na mataifa mengine pia.
Vita imeambatana na vifo vya raia wengi sana katika maeneo ya Gaza bila kikomo sasa.Swali langu ni je,Gaza inawakazi wangapi?(maana nikiangalia matukio mengi waliyoripoti aljazeera inaoneka vifo ni vingi sana)
Swali jingine ni hili,itatokea nini ikiwa Israel ataendelea kufanya mashambulizi kila wakati na kufanya mauaji?
Je,Hamas wakiachia mateka huu mzozo unaweza kuisha?
Ni hayo tu kwa leo.