Ikiwa Kanisa lina mlinzi ambaye ni mwanadamu iweje Watu waombe Ulinzi kwa mungu aliyeshindwa kulinda nyumba yake?

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Moja ya mambo yaliyozidi kunipa mashaka kwenye suala la dini ni pamoja na suala la ulinzi na usalama.

Ukienda Kanisani sio ajabu ukakuta Milango. Na kama utaenda siku ambayo sio ya ibada sio ajabu ukakuta Milango imefungwa na kufuli kabisa.
Kama hiyo haitoshi, Makanisa makubwa huwekwa Walinzi wa kulinda Kanisa na mali zilizomo Kanisani.

Sijui ni lini swali hili lilizuka akilini mwangu. Na sijui kwa nini lilizuka.
Ikiwa Mungu wa majeshi, kwake kuna ulinzi na usalama kwa nini Watu waweke Walinzi kwenye nyumba za miungu yao wakati mungu anauwezo wa kulinda nyumba yake mwenyewe?

Je mwanadamu anauwezo wa kulinda nyumba ya mungu wake ili vitu vya Mungu wake visiibiwe na mwanadamu mwenzake?

Nafahamu Mungu ni Mkuu, Muweza wa yote. Lakini hana nyumba duniani na Mungu hana makazi kwa sababu yeye sio kiumbe.

Ijumaa Kareem
 
Dini ni fiksi tu!

Papa wa Wakatoliki ana walinzi wenye mabunduki!

Ina maana hauamini ulinzi wa mungu, siyo?

Ukitumia akili kuyafikiria hayo mambo ya mungu, utaona hayaingii kabisa akilini.

Na ndo maana kwenye dini kuna ‘dogma’.

We amini tu lakini usihoji.
 
Kwema Wakuu!

Moja ya mambo yaliyozidi kunipa mashaka kwenye suala la dini ni pamoja na suala la ulinzi na usalama.

Ukienda Kanisani sio ajabu ukakuta Milango. Na kama utaenda siku ambayo sio ya ibada sio ajabu ukakuta Milango imefungwa na kufuli kabisa.
Kama hiyo haitoshi, Makanisa makubwa huwekwa Walinzi wa kulinda Kanisa na mali zilizomo Kanisani.

Sijui ni lini swali hili lilizuka akilini mwangu. Na sijui kwa nini lilizuka.
Ikiwa Mungu wa majeshi, kwake kuna ulinzi na usalama kwa nini Watu waweke Walinzi kwenye nyumba za miungu yao wakati mungu anauwezo wa kulinda nyumba yake mwenyewe?

Je mwanadamu anauwezo wa kulinda nyumba ya mungu wake ili vitu vya Mungu wake visiibiwe na mwanadamu mwenzake?

Nafahamu Mungu ni Mkuu, Muweza wa yote. Lakini hana nyumba duniani na Mungu hana makazi kwa sababu yeye sio kiumbe.

Ijumaa Kareem
Halafu kuna ulinzi wa majini misikitini
 
Mungu ametupa akili, maarifa na ufahamu.
Siku zote Mungu huwa anafanya kuanzia pale uwezo wa binadamu unapoishia.

Mungu ana utaratibu wake na hafanyi vitu kwa mtazamo na fikra duni za mwanadamu.

Unadhani Mungu alishindwa kutelemsha hekalu toka juu hadi amwambie Daudi ili mwanae amjengee Mungu hekalu?.

1 Kor 1:25​

Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

Isa 55:8-9​

Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
 
.
JamiiForums-772586512.jpg
 
Mbna hata pesa🤣🤣

Hivi unajua fungu la sadaka linaendaga mpaka vatcan🤣🤣

Halafu unaenda kwa padri akuombee uwe tajiri

Hata zaka ndio maana wanasisitiza kinoma kitoa ile majesuit wa vatcan wasilale njaa

Hujawai jiuliza kwanini kujenga shule kanisa wanachangisha waumim shule ikamilika km huna ada husomi shule io
 
Mkuu nenda ka google kitu kinaitwa,"TERROR MANAGEMENT THEORY" najua wewe sio mvivu wa kusoma, utapata majibu yote ya maswali yako ukiielewa hiyo nadharia ya mtu aliyewahi kujibu swali lako tuletee thread ingine kwa kiswahili ili walio wengi waelewe ni ombi lakini
 
Lzm kanisa lilindwe Tena na kampuni pendwa ya g4s security solution au Garda warda

Una taka mashetanj waje wanye na kujisadia kanisani na kutupa matakataka Yao

Kimara korogwe wapo walinzi na camera za CCTV iko kila Kona

Na bado kanisa linajaribiwa mno

Ni muhimu kumlindia mungu nyumba yake
Periods
 
Hii mada umeanzisha ili tuu uendelee kupata popularity au ni kweli hujui the concept behind your qns?

You have typically based on material things. Na juu ya mwamba huu nitajenga kanisa langu. Umeelewqje hapo? Kanisa is not all about majengo na materials inside it. It's spiritual. Ulinzi wa Mungu ni wa kiroho. Hizo Mali za kushikika mtazilinda wenyewe
 
Kwema Wakuu!

Moja ya mambo yaliyozidi kunipa mashaka kwenye suala la dini ni pamoja na suala la ulinzi na usalama.

Ukienda Kanisani sio ajabu ukakuta Milango. Na kama utaenda siku ambayo sio ya ibada sio ajabu ukakuta Milango imefungwa na kufuli kabisa.
Kama hiyo haitoshi, Makanisa makubwa huwekwa Walinzi wa kulinda Kanisa na mali zilizomo Kanisani.

Sijui ni lini swali hili lilizuka akilini mwangu. Na sijui kwa nini lilizuka.
Ikiwa Mungu wa majeshi, kwake kuna ulinzi na usalama kwa nini Watu waweke Walinzi kwenye nyumba za miungu yao wakati mungu anauwezo wa kulinda nyumba yake mwenyewe?

Je mwanadamu anauwezo wa kulinda nyumba ya mungu wake ili vitu vya Mungu wake visiibiwe na mwanadamu mwenzake?

Nafahamu Mungu ni Mkuu, Muweza wa yote. Lakini hana nyumba duniani na Mungu hana makazi kwa sababu yeye sio kiumbe.

Ijumaa Kareem
Ulisema mwenyewe hukulelewa na baba na mama yako. Akili zako zina walakini.
Lini ulimwona Mungu amekuja duniani anajenga majumba yake?
Nyumba za Mungu tunajenga sisi wanadamu na tunaweka samani na tunazilinda. Wewe endelea kuteseka na ukuu wa Mungu ukingojea siku umkute kakaa kwenye kila kanisa au msikitini analinda.
 
Back
Top Bottom