Ikiwa Kanisa lina mlinzi ambaye ni mwanadamu iweje Watu waombe Ulinzi kwa mungu aliyeshindwa kulinda nyumba yake?

Sasa watahudumiwa na nani? Uliona wapi Mlawi akawa na shamba?
 
Vitu vingine si vyakuongea kwa sauti Mungu anaweza kukubadilisha ghafla mpaka ukashangaa

Mungu wangu na wako hawafanani.

Mungu wangu hana nyumba, miungu yenu inanyumba na imejengewa nyumba.
mungu wenu anuani yake iko mbinguni. Wakwangu hana anuani kwa sababu yeye sio kiumbe. Yupo pote muda wote.

Mungu wangu hawezi kunifanya lolote kwa sababu chochote atakachofanya juu yangu ni mpango wake kabla sijazaliwa.

Miungu yenu ikikerwa kidogo ndio inaweza kufanya kwa mihemko ya kijinga kwa sababu ni miungu na sio MUNGU Mkuu
 
Sio makosa yako
 
Sasa watahudumiwa na nani? Uliona wapi Mlawi akawa na shamba?
Hizo pesa ndio zinaleta kiburi vatcan .....kuanza kupitisha agenda rainbow .....fikiria dunia nzima kuna makanisa mangap?
 
Dini ni fiksi tu!

Papa wa Wakatoliki ana walinzi wenye mabunduki!

Ina maana hauamini ulinzi wa mungu, siyo?

Ukitumia akili kuyafikiria hayo mambo ya mungu, utaona hayaingii kabisa akilini.

Na ndo maana kwenye dini kuna ‘dogma’.
Naunga mkono hoja
 
Ni wakati wa kugundua dini ni miradi ya watu. Nyakati za mwisho, au roho inapotengana na mwili utagundua mengi. "Utashtuka,! Kumbe nilikuwa namuabudu shetani!!".
 
Kinachofanya makanisa yafungwe ni kuepuka unajisi wa madhabahu, waonekana bado mchanga kiimani ukikuwa utanielewa.
 
Kinachofanya makanisa yafungwe ni kuepuka unajisi wa madhabahu, waonekana bado mchanga kiimani ukikuwa utanielewa.

Kwamba miungu inashindwa kuzuia unajisi wa kimadhabahu?
Embu kasome Torati uone ambaye sio mtakatifu akifika madhabahu ya patakatifu pake patakatifu nini kinatokea
 
Kuna mshkaji wangu mmoja kaiba gitaa kanisani kwetu juz kati.
 
Mungu wenu mmemjengea nyumba,mnatoa fungu la kumi,maana Hana hata mia,mnatoa sadaka ya kuteketeza..anapenda nyama choma,mnalinda nyumba yake..hawezi Linda mwenyewe
 
Mkuu naomba kujua kwanza imani yako kama ni mkristo au muislam Kisha nikupe jibu kama hutojali
 
Kwamba miungu inashindwa kuzuia unajisi wa kimadhabahu?
Embu kasome Torati uone ambaye sio mtakatifu akifika madhabahu ya patakatifu pake patakatifu nini kinatokea
Akasome torati sura ya ngapi na mstari wa ngapi? Maana torati imeelezea mambo mengi
 
Ni wakati wa kugundua dini ni miradi ya watu. Nyakati za mwisho, au roho inapotengana na mwili utagundua mengi. "Utashtuka,! Kumbe nilikuwa namuabudu shetani!!".
Inategemea unaabudu dini gani ndugu. Angalia usije ukajuta mbele ya safari
 


We aliekwambia Mungu anahitaji jengo nan.. unajua maana ya kanisa...

Imeandikwa.. wakutanapo watu wawili au watatu wakayanena na kufundishana niliyowaagiza kuyafanya na kuomba pamoja kwa kulitaja jina langu basi mimi nipo katikati yao..

Kanisa sio jengo hata mkikaaa chini ya mti mkasali hilo ni kanisa.. binadam ndo mmeamua kujenga majengo na kuweka mali ndan mnaweka walinzi sababu mna hofu ya mali zenu.. vilivyopo ndan ya kanisa sio mali ya Mungu ni zenu nyie

Mungu alipompa binadam Maarifa ya kuitawala dunia maana yake alimpa
Uwezo wa kutambua mema na mabaya..
Sasa ni swala La binadam Kuamua akengeuke ama awe safi..

Unachosema ni sawa na mwalimu amfundishe mwanafunzi na kumpa maarifa kisha siku ya mtihan mwalimu aamue kumsaidia mwanafunzi kufanya mtihan ili Asifeli
 
Muombe roho Mtakatifu akufunulie mambo magumu badala ya kuandika ujuaji hadharani.

Usipoelewa huu ufafanuzi basi una tatizo kubwa la uelewa:

Kwanza, unatakiwa utambue kinachotukutanisha au kuwakutanisha watu kanisani sio jengo ni Imani maana Mwenyezi Mungu amesema kwamba wakutanikapo watu wawili au zaidi Kwa jina lake yupo katikati yao. Kwa hiyo ni Imani.

Pili, mlinzi anawekwa kulinda Mali za kanisa au misikiti na Mwenyezi Mungu analinda Imani za waamini wake. Imani haiwezi kuibiwa.

Tatu, sio Kila anayeingia kanisani ni mwema kiasi hicho wengine wana nia ovu za kibinadamu ndio maana wanawekwa Walinzi wakisaidiwa na ulinzi wa Roho Mtakatifu tunaamini watasaidia kudhibiti na kufifisha nia ovu za wengine.

Nne, Kanisa inakuwa nyumba ya Mungu pale waamini wanapokutana Kwa Imani kufanya ibada ndio maana muda huo ulinzi unakuwa ni Kwa Mungu lakini muda mwingine wowote kanisa ni jengo ambalo linahitaji ulinzi wa ziada pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…