Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Polisi Tanzania, nadhani kwa sasa ndio Taasisi inayotia aibu zaidi duniani, Walimkamata Mbowe na wenzake kwa kuandaa kongamano la Katiba mpya, mitaa yote ya Mwanza walimwagwa polisi na hotel kulikopangwa kufanyika kongamano hilo ikiwekwa chini ya Ulinzi mkali kuanzia ndani hadi nje na kuzungushiwa utepe wa hatari.
Viongozi kadhaa walidakwa na kupelekwa rumande hadi dakika hii (Dunia nzima inajua), sasa leo wanakuja na ngonjera za kiwango cha chini kwamba Mh Mbowe hakukamatwa kwa sababu ya kongamano hilo , bali alikamatwa kwa tuhuma za ugaidi na kupanga njama za kuua viongozi wa serikali.
Sasa swali ni hili: Wale wengine waliokamatwa sambamba na Mbowe walikamatwa kwa sababu zipi?