Ikiwa msajili msaidizi wa vyama hazingatii Sheria za usalama barabarani (Hakuvaa helmet) atawezaje kusimamia ipasavyo sheri za vyama vya siasa?

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Kuna video inazunguka kwenye mitandao ya kijamii.

Video hiyo inamuonesha msajili msaidizi wa vyama vya siasa akiwa Hana helmet akielekea ofisi za Chadema!
Je; Utii wa Sheria bila shuruti huwa ni kwa ajili ya nani ikiwa viongozi wakubwa Kama huyu hawazingatii Sheria?

Ikiwa Sheria za barabarani tu kashindwa kuzifuata je; ataweza kweli kusimamia ipasavyo Sheria za vyama vya siasa?
 
Atakua anaamini u-ccm wake ni usalama tosha.
 
Wewe unazifuata sheria zote? by the way, kutovaa helmet sio kosa kama ameandikiwa kibali na daktari au waziri wa mambo ya ndani, ulimuuliza kibali?
ujuaji Sasa! hata ujinga unatetea
 
Wewe unazifuata sheria zote? by the way, kutovaa helmet sio kosa kama ameandikiwa kibali na daktari au waziri wa mambo ya ndani, ulimuuliza kibali?
WaTz kwa kuendekeza ujinga! Helmet na siasa za waziri ni wapi na wapi? Waliotengeneza pikipiki ni wajinga kwa kubuni kifaa cha kuwakinga watumiaji wakati wa ajali?
Tabibu gani mpumbavu atakayetaka mpanda pikipiki asivae hiyo kofia?
 
Je wanaomsindikizaga na mapikipiki Lissu wamebebana wanne mpaka watano bila helmet na mabendera wao wanafata sheria za nch gani?
Tunamuongelea kiongozi mwandamizi hapa, usihamishe mjadala kwa Lissu. Je watu wa Lissu wakija na sababu kama yako ambayo haina mashiko utasema nini, au kwa sababu ni wa Lissu basi kosa litakuwa palepale?
 
WaTz kwa kuendekeza ujinga! Helmet na siasa za waziri ni wapi na wapi? Waliotengeneza pikipiki ni wajinga kwa kubuni kifaa cha kuwakinga watumiaji wakati wa ajali?
Tabibu gani mpumbavu atakayetaka mpanda pikipiki asivae hiyo kofia?
Ujinga ni ugonjwa Mkuu Kama magonjwa mengine ni vile hakuna tiba yake ndio maana unaona majibu ya ajabu kila kukicha..
 
Reactions: Auz
Helmet,condom,barakoa nk ni vifaa kinga , si wote hutumia na kuzingatia hasa condom ndio maana takwimu za ukimwi haziteremki
 
Tumuonee tu huruma maana kwa pressure aliyonayo angeweza hata kufungua mlango akidhani boda ni vx
 
Wewe unazifuata sheria zote? by the way, kutovaa helmet sio kosa kama ameandikiwa kibali na daktari au waziri wa mambo ya ndani, ulimuuliza kibali?
Duu kwahiyo kumbe ana kibali maalum ?
 
Hakuna binadamu aliyekamilika kwa 100% kila mmoja ana mapungufu yake pamoja na kujisahau.
 
Wewe unazifuata sheria zote? by the way, kutovaa helmet sio kosa kama ameandikiwa kibali na daktari au waziri wa mambo ya ndani, ulimuuliza kibali?
Above all, Hakuna binadamu aliyekamilika kwa 100% kila mmoja ana mapungufu yake pamoja na kujisahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…